Hakuna chanjo ya lazima Mkuu. Elewa hivyo.
Halafu watu hawafanani kinga. Kuna watu dunia hii, hii hata UKIMWI ni kama mafua tu na kuna wanakufa kwa Mafua tu.
Mimi sipingi chanjo, na kwa sehemu nilipo nadhani nitachanjwa ila sioni ulazima wowote wa kuchanja kila mtu.
Kwanza sidhani kama kila nchi imefanya hivyo.
Pili, nchi hii ina watu karibia 60M lakini serikali imeagiza chanjo 300,000 tu. Ukitoa zitakazoharibika maana miundombinu yetu tunaijua wenyewe.
Mambo mengine yote yatakwama kama nchi itaagiza chanjo za watu 60M.
Hiyo ni akili ya kawaida tu.