#COVID19 Fatma Karume: Hakuna chanjo ya lazima. Haki za Binadamu zinataka faragha hususan wa mwili wako

#COVID19 Fatma Karume: Hakuna chanjo ya lazima. Haki za Binadamu zinataka faragha hususan wa mwili wako

Kisheria statement hii iko sawa. Yaani kinadharia statement hiyo iko sahihi.

Lakini ki afya, kitalaamu na kiserikali (yaani kiutekelezaji) ni lazima watu wengi kwa kadri iwezekanavyo na ikibidi wote wachanjwe. Vinginevyo chanjo (kitalaamu) haitakuwa na maana.

Hiki ndicho Mwamba Mbowe bila shaka alikuwa akikimaanisha.

Kuhakikisha chanjo ni hiari kinadharia lakini si hiari kiuhalisia, ulazima hauko kwenye kulazimishana kwa fimbo au mabunduki kwenda kuchanjwa. Ulazima unakuja hivi:

1. Kusafiri onyesha proof ya chanjo
2. Kusajiliwa mahali onyesha proof ya chanjo
3. Kuingia mahali onyesha proof ya chanjo
4. Nk nk.

Hapo ndipo mzizi wa fitna ulipo.

Utajikuta mwenyewe kwenye fix tu, kama kwenye barakoa ulivyokuwa ambazo pia ni hiari.

Leo hii ofisi, hospitali au sehemu gani serious utaingia bila barakoa? Ndiyo shuruti zenyewe hizo. Hutaki usiingie maana kuingia si lazima pia.

Mwamba Mbowe yuko vizuri kwani kitalaamu njia zote ni lazima zitumike kuwataka watu kuchanjwa kwa hiari ikibidi kwa mjeledi (in the extreme) kwani ni kwa faida yao.

Hata hapa serikali itafuata utaratibu huo huo. Mbowe ni wa kupongezwa kwa kuwa muwazi. Chanjo ni kwa faida yetu.

Cc: denooJ BAK Salary Slip technically
Yalishanenwa lazima yatimie,

Hizo marufuku ruksa ila kulazimisha hayo maungese tutakuja kunyoana mavumbi na chupa
 
Chanjo hazina utata wowote ila hazipaswi kulazimishwa. Serikali haipaswi kuwalazimisha watu wasiotaka chanjo wakati zitakapoanzwa kutolewa.waachwe tu, hiyo ni gharama mojawapo ya demokrasia. Hii sio China au Korea Kaskazini.
Narudia, katika hili, Mbowe kakosea sana na sijui nani kamshauri.

Ni vema arekebishe kauli au aifute.

Hizi chanjo bado zina utata mwingi hivyo si busara kuja na hiyo kauli unless kuna ambazo zineshathibitishwa kuwa hazina madhara kwa walio wengi.
 
Kukataa chanjo wakati wengine wanachanjwa kunafanya ugonjwa uendelee kuwepo
 
Kiukweli Freeman Mbowe amechemka sana ktk hili; nashauri arudi kuomboleza msiba wa kaka yake. Chanjo ya corona haiwez kuwa jambo la lazima. Anayetaka achanje asiyetaja asichanje
Amechemka na alitakiwa aweke maelezo sawa, kwamba iwapo cha njo ni hiari, basi serikali/jamii ijitahidi sana kuhamasisha watu kuchanja, kwani kama mzigo utaletwa halafu wanaochanja wanakuwa wachache ni hasara kiuchumi, na pia kwenye upande wa ugonjwa ni kuwa tutegemee virus huyo kuwa mgumu na hatari zaidi kama huyu wa phase 3 Delta. Chanjo inaleta maana tu, iwapo watu wengi katika jamii wamepata chanjo hiyo.
 
Narudia, katika hili, Mbowe kakosea sana na sijui nani kamshauri.

Ni vema arekebishe kauli au aifute.

Hizi chanjo bado zina utata mwingi hivyo si busara kuja na hiyo kauli unless kuna ambazo zineshathibitishwa kuwa hazina madhara kwa walio wengi.
Kiukweli Freeman Mbowe amechemka sana ktk hili; nashauri arudi kuomboleza msiba wa kaka yake. Chanjo ya corona haiwez kuwa jambo la lazima. Anayetaka achanje asiyetaja asichanje
Kwa mara ya Kwanza Leo umekuwa tofauti na mwamba, duh? Dunia inaenda haraka sana
Hukuwahi kupinga chochote cha mwamba, hata Enzi za Faru John.
Sent from my 5033X_EEA using JamiiForums mobile app
Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake (Freedom of expression) juu ya jambo lolote bila kuvunja sheria...

Mbowe ametoa maoni yake. Na mbowe wala hana maamuzi ya mwisho juu ya jambo hili kwa sababu siyo mamlaka ya maamuzi (serikali) alichofanya ni kutoa ushauri, maoni nk nk kama ambavyo kila mtu anatoa mtazamo wake...

Lakini mwisho wa siku ni lazima mamlaka za maamuzi za wananchi (serikali) zije na mwongozo wa kufuatwa na watu wote..

Na nyie kila mmoja wenu hapa mnatoa maoni yenu bila kujali mko sahihi au siyo sahihi. Hatuwezi kuwaita mmekosea au ni wajinga au wapumbavu kwa sababu maoni, mawazo au mitazamo yenu haifanani au kukubaliana na yetu ..

Tujifunze kuheshimu maoni na mawazo ya wengine. Kukubaliana na kutokukubaliana ni ishu nyingine na inabaki kuwa hivyo...

Ukiniuliza mimi juu ya jambo hili, nitakujibu moja kwa moja (maoni yangu) kuwa, hakuna ulazima wa kumlazimisha mtu kuchanjwa. Watu waende kuchanjwa kwa hiari yao...

Na sababu ni moja tu, nayo ni kuwa, hakuna ukweli (fact) ya moja kwa moja juu ya hiki kinachoitwa UVIKO 19 na hivyo hata chanjo yake kuwa na utata wa mapokezi yake kwa ulimwengu wote...

Hii ni tofauti na chanzo zingine zote tulizowahi kuchanjwa siku za nyuma kv surua, kifua kikuu nk nk
 
Tatizo la Mbowe ni mbumbumbu na kutokwenda shule
Kwa hiyo ikitokea Shangazi Fatma Karume akakosea na Mbowe akamrekebisha, tatizo litakuwa umbumbumbu wa Fatma?
Kukosea ni ubinadamu. Lakini je, Mwenyekiti wako wa ccm akikosea, unaweza kumkosoa? Ni jambo jema kujenga utamaduni wa kukosoana, badala ya kujenga UNAFIKI, kwamba watu wanaweza kumkosoa tu pale anapofariki, kama tunavyoona kwa Magufuli .
Kwa hiyo wanaccm mko huru kumkosoa Rais Samia anapokosea. Ndiyo Demokrasia hiyo
 
ujasiri wa kutukana hivi hadharani unatoa wapi inaonyesha wazazi wako walikulea kiwendawazimu
Sina ujasiri wowote ndugu, na nimelelewa vizuri kabisa. Mwenyewe Mwendawazimu kwa mdomo wake alisema yeye ni KICHAA .
na Ndugai kwa mdomo wake ametamka kuwa anafaili lake Mirembe.
Mimi nani mpaka nibishe ..
 
Narudia, katika hili, Mbowe kakosea sana na sijui nani kamshauri.

Ni vema arekebishe kauli au aifute.

Hizi chanjo bado zina utata mwingi hivyo si busara kuja na hiyo kauli unless kuna ambazo zineshathibitishwa kuwa hazina madhara kwa walio wengi.
Hajakosea!
Nashawishika kusadiki kuwa huo ni mpango mkakati wa Chama chao, unaolenga kuvutia ruzuku na misaada ya hali na mali kutoka kwa mabeberu wa kimataifa waliobuni hii biashara ya corona duniani.

Bila shaka ni kutokana na ushawishi mtamu wa balozi wao anayeishi na kula maisha nchini
Ubelgiji!
 
Narudia, katika hili, Mbowe kakosea sana na sijui nani kamshauri.

Ni vema arekebishe kauli au aifute.

Hizi chanjo bado zina utata mwingi hivyo si busara kuja na hiyo kauli unless kuna ambazo zineshathibitishwa kuwa hazina madhara kwa walio wengi.
Kwa hiyo kakosea kutoa msimamo wake au Ni msimamo wa chama? Pia tuheshimu mawazo ya wengine..m
 
Hampati maambukizi au mnapata ila haifanyi mkaumwa hadi kulazwa na kusababisha kifo? maana nachojua chanjo hazizuii maambukizi hivyo unaweza ukapata maambukizi na usiumwe ila ukaambukiza wengine wasiochanjwa.

Kuhusu suala la vifo kuwaelimisha nadhani hilo hadi sasa lingekuwa limeshawaelimisha, kwa sababu corona imeanza toka mwaka jana mpaka leo kama bado hakuna la kujifunza basi hakuna tena somo litakalopatikana hapo au kwamba hakuna vifo vya kufanya watu wajifunze na kutaka chanjo.
Chanjo yenyewe ni maambukizi yaliyo control, so baada ya hapo hata ukipata maambukizi ambayo hayatojionesha, ambayo ndiyo majority, that is irrelevant.

Kwenye vifo kuwaelimisha, ukiwa na tabia ya kuvuka barabara huku umefumba macho, ukasema umevuka mara tatu na hivyo kuvuka hivyo ni salama, huku hujui kwamba umeweza kuvuka kwa bahati tu, hilo halimaanishi kwamba kuvuka barabara huku umefumba macho ni jambo salama.

Tanzania Covid bado haijachanganya, usichukulie kwamba ndiyo imeshafika peak sasa.
 
Narudia, katika hili, Mbowe kakosea sana na sijui nani kamshauri.

Ni vema arekebishe kauli au aifute.

Hizi chanjo bado zina utata mwingi hivyo si busara kuja na hiyo kauli unless kuna ambazo zineshathibitishwa kuwa hazina madhara kwa walio wengi.

Umeongea kizalendo
 
Mbowe hana uwezo wa kulazimisha chochote nchini; hawezi kuwa dikteta; sio kiongozi wa nchi. Katoa tu maoni yake kuhusu chanjo ya Covid-19. No need to overrate him.

Mimi binafsi siungi mkono wazo la chanjo kuwa lazima ingawa naelewa nia Mbowe. Haki zangu za binadamu haziwezi kuathiriwa na maoni ya mtu binafsi.

Inategemea.... Umezingatia huyo mtu na maoni yake vina influence gani katika jamii?
 
Chanjo yenyewe ni maambukizi yaliyo control, so baada ya hapo hata ukipata maambukizi ambayo hayatojionesha, ambayo ndiyo majority, that is irrelevant.

Kwenye vifo kuwaelimisha, ukiwa na tabia ya kuvuka barabara huku umefumba macho, ukasema umevuka mara tatu na hivyo kuvuka hivyo ni salama, huku hujui kwamba umeweza kuvuka kwa bahati tu, hilo halimaanishi kwamba kuvuka barabara huku umefumba macho ni jambo salama.

Tanzania Covid bado haijachanganya, usichukulie kwamba ndiyo imeshafika peak sasa.
Madereva wengi wa kitanzania wanaamini kuwa pombe haiathiri uendeshaji wake. Wengine wanadai kuwa wakinywa ndio wanakuwa makini zaidi. Lakini sheria inazuia madereva wote kuendesha magari wakiwa wamekunywa kiasi fulani cha pombe hata wale wanaosema kuwa pombe inawafanya madereva bora zaidi. Kinachozuiwa hapa ni uwezekano wa dereva aliye kunywa kusababisha ajali ambayo itaathiri uhai wa watu wengine hata kama yeye atatoka mzima. Ingekuwa ukinywa pombe na kuendesha gari utaathirika peke yako, pengine serikali zingeona hamna haja ya kuingilia uhuru wako wa kunywa pombe.

Chanjo ni hivyo hivyo. Unaweza ukawa hauamini kuwa kuna corona au/na hauogopi kufa kwa corona kitu ambacho ni haki yako. Shida ni uwezekano wa wewe kuwaambukiza wengine na kuwasababisha ama wapoteze maisha yao au waathirike kwa namna nyingine( kiuchumi, kiafya n.k.) baada ya wewe kuwaambukiza. Na mbaya zaidi ni kuwa wengi wao hautawajua. Ndio maana ili kuwaokoa hao utakaowaambukiza, chanjo ni muhimu kuwa ya lazima. Tusipofanya hivyo hatutafikia herd immunity ambapo wote tutakuwa salama.

Amandla...
 
Back
Top Bottom