Fatuma Karume kaonge maneno mazito, yatawauma Watanganyika lakini ni ukwel.
1. Tanganyika imevaa koti la Muungano, ni ukweli! kila kitu cha Tanganyika ni cha Muungano. Balozi Amina anataka '' Formula '' ya kugawana rasilimali za Muungano yaani za Tanganyika ( hajasema kuchangia ni kugawana tu).
Gharama za Muungano zinabebwa na Tanganyika kwa jina la koti la Tanzania; Bajeti ya Zanzibar, madeni ya mikopo ya Zanzibar hata bili za majumbani kwao
Rais SSH alipokabdihiwa madaraka akachukua deni la Bilioni 60 za Umeme akalifanya la Muungano(Tanzania).
Ni haki alichofanya Rais SSH kwasababu tumebeba koti, kama kuna chawa na kunguni hiyo ni juu yetu.
2. Fatma kasema kinachotakiwa ni uwepo wa Serikali ya Tanganyika.
Hili nalo ni la kweli kwasababui Rais wa Koti la Muungano anapatikana tu bila kujadili anatoka wapi.
Fatma anasema Uzalendo kwa maneno ya Uzanzibar yanawafanya wajivunie Uzanzibar, sasa huyu anayejivunia Uzanzibar anauchungu gani na Tanganyika?
Lakini muhimu alichosema ni kwamba Serikali ya Tanganyika itasimamia na kulinda masilahi yake.
Fatma anona wazi Masilahi ya Tanganyika hayana mwangalizi, ni ukweli mchungu lakini ni ukweli.
3. Fatma anasema Wazanzibar wanajivunia Uzanzibar kwanza kabla ya Utanzania.
Ni kweli, na Watanganyika wanapaswa kujivunia Utanganyika kwanza ili wanaohitaji Muungano wauheshimu.
Nakubaliana na Fatma , Wazanzibar hawana uchungu na Muungano kwasababu ya ''free ride'
Mtamsema Fatma lakini ukweli unabaki pale pale, tunahitaji Tanganyika tusimamie masilahi yetu na watu wetu.
CCM wanaotetea huu Muungano ni wanaufaika wa mfumo, mwananchi wa kawaida wa Kadewele, Kidogo Basi, Magoroto , zaidi ya kuumia kwa gharama za kubeba Muungano na Zanzibar anafaidikaje na Muungano!
Wasichotakaueleza Wazanzibar , Tanganyika inanufaika na nini na huu Muungano au kuvaa koti la Muungano?
Hili ndilo akina Fatma hawasemi wanajificha kwamba Wananchi wa pande zote wanataka Muungano!
No! Mwananchi wa Tanganyika haihitaji Muungano , kama anahitaji ni kwa faida gani?
PakiJinja Pascal Mayalla Mag3