Fatma Karume: Tatizo Watanganyika hawajitambui utaifa wao, sisi Zanzibar hatuwezi kufuta utaifa wetu

Fatma Karume: Tatizo Watanganyika hawajitambui utaifa wao, sisi Zanzibar hatuwezi kufuta utaifa wetu

Lina ushamba gani? Yale yale ya ukila viazi na mchuzi ni chakula local tofauti na ukila "potato mix stew." Tanganyika ni jina zuri sana.
Nadhani hata tafsiri yenyewe ya jina Tanganyika HAINA MASHIKO.
 
Wakili msomi Fatma Karume anasema kuwa viongozi waTanganyika ndiyo tatizo.


View: https://m.youtube.com/watch?v=upbVqLpdVmk

Viongozi wa Zanzibar na wananchi wa Zanzibar wanajitambulisha kama wazanzibari katika muungano wa nchi mbili kisha inafuata uTanzania.

Lakini viongozi wa kutoka upande wa bara hasa hawa wa CCM na serikali yake wanaona haya na kulazimisha kuufuta utanganyika wa asili raia taifa lao Tanganyika.

Upande wa Zanzibar utambulisho ni Mzanzibari kwanza, halafu mbili kutoka Tanzania.

Hapo ndipo kunapotokea zogo lakini kiuhalisia huwezi kufuta uasili wa kitaifa wa mtu katika Muungano anasisitiza wakili Fatma Karume kwa viongozi wa CCM bara na walio katika serikali yake.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni wa nchi mbili Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Jina la kwanza lilitambulika kama nchi ya Jamhuri za Tanganyika na ya Watu wa Zanzibar April 26, 1964.

Ilichukua miezi kadhaa baada ya muungano jina hilo la kwanza refu hadi kubadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba 1964

Historia ya nchi ya Tanganyika iliyopata uhuru mwezi December 1961 na nchi ya Zanzibar iliyopata uhuru wake mwaka 1963 mwezi December pamoja na vizazi vya nchi hizo vilivyofuatia haviwezi kufutwa na viongozi wachache wa CCM kwa kuwa utaifa ni asili.

Zanzibar forever
#waingie Kwa passport
 
Wewe unajua jina la Tanganyika lometokana na nini. Na je hiyo maana yake inathaminisha nini kama Taifa
Boss, historia ya Tanganyika ilianza 1919 ipo wazi. Wewe umesema jina halina mashiko ndo ungetuambia sababu zako.
 
Tukisema tuanze kuulizana mambo kama hayo.

Itabidi tuulizane pia kama babu yake ni mzanzibari kweli au mnyasa wa Malawi.
 
Hao mix mix ndiyo wanaleta chkchk,hivi we jiulize huko zenji kabla mwarab hajaingia
Walikuwepo watu gani,mbona hadi wandengereko walikuwepo huko

Ova
Mbona wengine wanasema walipelekwa huko na waarabu kama watumwa?
 
Mbona wengine wanasema walipelekwa huko na waarabu kama watumwa?
Siyo kweli,kabla mwarabu hajafika
Hapo walikuwepo watu
Kwani machotora/wapemba hapo wamepatikana vp...
Si mwarabu alizaa na wafrika

Ova
 
Siyo kweli,kabla mwarabu hajafika
Hapo walikuwepo watu
Kwani machotora/wapemba hapo wamepatikana vp...
Si mwarabu alizaa na wafrika

Ova
Nauliza tu kwani nadharia ni nyingi. Kuna wasemao visiwa vilikuwa havina wakaazi.
 
Zanzibar ndo hawajitambui ndo maana tumewafanya ni koloni letu
Sisi tunafaidikaje na koloni hili?

Kwenye ulingo wa Ajira, Mtanganyika hawezi kuajiriwa kwenye Serikali ya Zanzibar lakini Mzanzibar anaajiriwa kwenye Serikali ya Muungano. Ikumbukwe wote wapo ndani ya Muungano. Sasa hapa nani ni Koloni wa mwenzake?
 
Back
Top Bottom