Fatma Karume: Tatizo Watanganyika hawajitambui utaifa wao, sisi Zanzibar hatuwezi kufuta utaifa wetu

Fatma Karume: Tatizo Watanganyika hawajitambui utaifa wao, sisi Zanzibar hatuwezi kufuta utaifa wetu

Fatuma Karume kaonge maneno mazito, yatawauma Watanganyika lakini ni ukwel.

1. Tanganyika imevaa koti la Muungano, ni ukweli kwasababu kila kitu cha Tanganyika ni cha Muungano.
Ndiyo maana Balozi Amina anasema iwepo Formula ya kugawana rasilimali za Muungano yaani za Tanganyika ( hajasema kuchangia bali kugawana mapato).

Gharama za Muungano zinabebwa na Tanganyika kwa jina la koti la Tanzania; Bajeti ya Zanzibar, madeni ya mikopo ya Zanzibar hata bili za majumbani kwao

Rais SSH alipokabdihiwa madaraka akachukua deni la Bilioni 60 za Umeme akalifanya la Muungano(Tanzania).
Ni haki alichofanya Rais SSH kwasababu tumebeba koti, kama kuna chawa na kunguni hiyo ni juu yetu.

2. Fatma kasema kinachotakiwa ni uwepo wa Serikali ya Tanganyika.
Hili nalo ni la kweli kwasababui Rais wa Koti la Muungano anapatikana tu bila kujadili anatoka wapi.

Fatma anasema Uzalendo kwa maneno ya Uzanzibar yanawafanya wajivunie Uzanzibar, sasa huyu anayejivunia Uzanzibar anauchungu gani na Tanganyika?

Lakini muhimu alichosema ni kwamba Serikali ya Tanganyika itasimamia na kulinda masilahi yake.
Fatma anona wazi Masilahi ya Tanganyika hayana mwangalizi, ni ukweli mchungu lakini ni ukweli.

3. Fatma anasema Wazanzibar wanajivunia Uzanzibar kwanza kabla ya Utanzania.
Ni kweli, na Watanganyika wanapaswa kujivunia Utanganyika kwanza ili wanaohitaji Muungano wauheshimu.

Nakubaliana na Fatma kwasababu sasa hivi Wazanzibar hawana uchungu na Muungano kwasababu ya ''free ride'

Mtamsema Fatma lakini ukweli unabaki pale pale, tunahitaji Tanganyika tusimamie masilahi yetu na watu wetu.

CCM wanaotetea huu Muungano wengine ni wanaufaika wa mfumo, mwananchi wa kawaida wa Kadewele, Kidogo Basi, Magoroto au Isevya zaidi ya kuumia kwa gharama sidhani kama anafaidika na Muungano!

Wasichoeleza Wazanzibar , Tanganyika inanufaika na nini na huu Muungano?

Hili ndilo akina Fatma hawasemi wanajificha kwamba Wananchi wa pande zote wanataka Muungano! No! Mwananchi wa Tanganyika haihitaji Muungano , kama anahitaji ni kwa faida gani?

PakiJinja Pascal Mayalla Mag3
Tanganyika wana ujinga mwingi na wameukumbatia hawataki uwatoke. They are happy being cornered in a comfort zone.

Harakati ni kama zinaenda kuchukua mkondo mpya. Baada ya kelele za muda mrefu zilizoelekezwa serikalini kuhusu aina hii ya muungano kutoweza kuleta unafuu wala ku promise unafuu wowote, sasa mbinu imerudi kwa wananchi na wanaharaki kuanza kujazana upepo.

Wale wa Zanzibar wanawa mock Mainlanders na wa Mainlanders wanawa mock Islanders.
Wananchi wameamua kutafuta suluhu kwa kuanza kushambuliana kwa maneno, hii itazaa chuki na uhasama basdaye tutaanza kushihudia mashambulizi ya kudhuriana. Mainlanders waliopo visiwani wataanza kushambuliwa na mali zao kuharibiwa huku biashara zao zikisusiwa na Wa zanzibar waliopo huko Mainland na wao watakutana na the same.

Huu ndiyo wakati wa serikali na mamlaka zote husika kukubali reform juu ya aina ya Muungano.
Wananchi hawapaswi kuishi kwa kuenzi bali wanapaswa kuishi katika ile namna wanayostahili, ukichukulia hata hili swala la Muungano hawakuwahi kuulizwa.

Watu hawapingi Muungani bali wanataka aina ya Muungano ambao watajivunia, pia utawapa heshima mbele za watu, lakini siyo Muungano huo mlio nao ambao unawafanya muonekane Majuha. Aina hii ya Muungano ni Tusi kubwa sana kwa Watanzania. Muungano wa kuenzi siyo Muungano ambao watamzania wanauhitaji.

Kama wana nia nzuri ya kuuenzi Muungano huu, basi waruhusu uingie katika phase ya kuwashirikisha wananchi ili na wao washauri namna nzuri ya kuuboresha Muungano huo kwa Maslahi ya pande zote zinaziungana.
 
Wakili msomi Fatma Karume anasema kuwa viongozi waTanganyika ndiyo tatizo.

View: https://m.youtube.com/watch?v=upbVqLpdVmk

Viongozi wa Zanzibar na wananchi wa Zanzibar wanajitambulisha kama wazanzibari katika muungano wa nchi mbili kisha inafuata uTanzania.

Lakini viongozi wa kutoka upande wa bara hasa hawa wa CCM na serikali yake wanaona haya na kulazimisha kuufuta utanganyika wa asili raia taifa lao Tanganyika.

Upande wa Zanzibar utambulisho ni Mzanzibari kwanza, halafu mbili kutoka Tanzania.

Hapo ndipo kunapotokea zogo lakini kiuhalisia huwezi kufuta uasili wa kitaifa wa mtu katika Muungano anasisitiza wakili Fatma Karume kwa viongozi wa CCM bara na walio katika serikali yake.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni wa nchi mbili Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Jina la kwanza lilitambulika kama nchi ya Jamhuri za Tanganyika na ya Watu wa Zanzibar April 26, 1964.

Ilichukua miezi kadhaa baada ya muungano jina hilo la kwanza refu hadi kubadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba 1964

Historia ya nchi ya Tanganyika iliyopata uhuru mwezi December 1961 na nchi ya Zanzibar iliyopata uhuru wake mwaka 1963 mwezi December pamoja na vizazi vya nchi hizo vilivyofuatia haviwezi kufutwa na viongozi wachache wa CCM kwa kuwa utaifa ni asili.

Tumsome/tumsikilize vizuri Fatma Karime. Anasema ndani ya Muungano imo Zanzibar na wanajivunia Uzanzibari wao. Anahoji Utanganyika uko wapi. Anadai viongozi ndio tatizo katika suala hili, hawakubali.

Kabla ya kuongeza chochote - chanya au hasi - hebu tujikumbushe yafuatayo: Tume ya Jaji Nyalali, G55, Tume ya Jaji Kisanga na Tume ya Jaji Warioba wote walishauri nini na kwa nini ushauri wao uliwekwa pembeni na nani huyo aliyechukua maamuzi hayo. Tukijikita katika kutafuta majibu yake tutaweza kumtendea wema Wakili Karume.
 
Tanganyika wana ujinga mwingi na wameukumbatia hawataki uwatoke. They are happy being cornered in a comfort zone.
Ni kweli lakini waliaminishwa Muungano una faida za Usalama kwa wakati huo. si zama hizi.
Zanzibar wakachukua 'advantage' kuaminisha Dunia wanaonewa, wanapunjwa n.k.
Watanganyika wamebaini hakuna uonevu, wamebeba mizigo
Harakati ni kama zinaenda kuchukua mkondo mpya. Baada ya kelele za muda mrefu zilizoelekezwa serikalini kuhusu aina hii ya muungano kutoweza kuleta unafuu wala ku promise unafuu wowote, mbinu imerudi kwa wananchi na wanaharaki kuanza kujazana upepo.
Ni kweli! si kwamba wanajazana upepo ni suala la muda. Wanaoaminisha muungano ni adimu na adhimu wanatoweka, sasa ni kizazi cha kuhoji 1/2 wamezaliwa Karume na Nyerere wameshazikwa, kuwaaminisha bla bla inachagiza ''curiosity' unayoiita kujaza upepo
Wale wa Zanzibar wanawa mock Mainlanders na wa Mainlanders wanawa mock Islanders.
Ukweli, Watanganyika wanajibu mapigo, Wazanzibar walipewa ''pass' ya kusema chochote , kudai chochote na kutishia Muungano, walioishi miaka ya 70 na 80 wanakumbuka. Watanganyika wanajibu kama hawaridhi wavunje Muungano! In fact waliokuwa ''cornered' ni Wazanzibar! Watanganyika hawana cha kupoteza
Wananchi wameamua kutafuta suluhu kwa kuanza kushambuliana kwa maneno, hii itazaa chuki na uhasama basdaye tutaanza kushihudia mashambulizi ya kudhuriana. Mainlanders waliopo visiwani wataanza kushambuliwa na mali zao kuharibiwa huku biashara zao zikisusiwa na Wa zanzibar waliopo huko Mainland na wao watakutana na the same.
Zanzibar wameshaanza! huna habari za Wamasai ! Hukumsikia Mbunge wa Zanzibar akiiwadia Watanganyika passport wasijazane Zanzibar! Tayari hali ni tete, Viongozi wanaficha ficha ukweli upo wazi, hakuna mapenzi
Huu ndiyo wakati wa serikali na mamlaka zote husika kukubali reform juu ya aina ya Muungano.
Wanadhani wataishi kwa kulaghai na kudanganya kwasababu wamezoea! zama zimebadilika
Wananchi hawapaswi kuishi kwa kuenzi bali wanapaswa kuishi katika ile namna wanayostahili, ukichukulia hata hili swala la Muungano hawakuwahi kuulizwa.
Haya maneno ya kuenzi, adhimu na adimu ni 'kutokuwa na majibu' ya maswali magumu ya Muundo wa sasa.
Watu hawapingi Muungani bali wanataka aina ya Muungano ambao watajivunia, pia utawapa heshima mbele za watu, lakini siyo Muungano huo mlio nao ambao unawafanya muonekane Majuha.
Kikundi cha CCM na siyo CCM wote kinahusika na hili
Aina hii ya Muungano ni Tusi kubwa sana kwa Watanzania. Muungano wa kuenzi siyo Muungano ambao watamzania wanauhitaji.
Kama wana nia nzuri ya kuuenzi Muungano huu, basi waruhusu uingie katika phase ya kuwashirikisha wananchi ili na wao washauri namna nzuri ya kuuboresha Muungano huo kwa Maslahi ya pande zote zinaziungana.
Hakuna ! narudia hakuna Tume iliyowahi kuundwa ikaja na majibu tofauti na Tume ya Warioba.

Wananchi wameshasema lakini kikundi cha watu wachache ndani ya CCMhakitaki.

Ni kikundi hicho kilihujumu mchakato wa Tume ya Warioba, kikaunda Tume feki ya Mkandara kufutilia mbali maoni ya Tume ya Warioba. Hili lmuundo wa Muungano ni kama upembe wa ng'ombe, halifichiki.

Kuna siku tuaamka hakuna Muungano maana wenye nchi wakiamua itakuwa basi!
Nyerere aliokubali vyama vingi aliiona hatari ya 20% akasema kabla haijawa majority tufanye mabadiliko
 
Wazanzibari always wako proud kuitwa Wazanzibari, sijui kwanini sisi Watanganyika tukiitwa Watanganyika huwa tunakasirika na kuona kama tunabaguliwa?
Kuna watu walishatangulia kuwaita watu kwa ubaguzi kupitia hilo jina ndio maana leo mtu akiitwa anaona kama kabezwa.
 
Wazanzibari always wako proud kuitwa Wazanzibari, sijui kwanini sisi Watanganyika tukiitwa Watanganyika huwa tunakasirika na kuona kama tunabaguliwa?
Waondoke kwanza warudi kwao tubaki wenyewe waone kama tutajiita watanzania, tukijiita watanganyika wao watakuwa kama wanyarwanda hapa nchini
 
Tanganyika ndio Tanzania wala sihitaji kujielezea sana.

Ila watawaliwa lazima wawe na maelezo mengi kujielezea.
 
Wazanzibari always wako proud kuitwa Wazanzibari, sijui kwanini sisi Watanganyika tukiitwa Watanganyika huwa tunakasirika na kuona kama tunabaguliwa?
Ila hata jina lenyewe la Tanganyika lipo local sana, yaani la kishambashamba hivi tofauti na jina la Zanzibar linavyo sound vizuri.
 
Tanganyika always ni sleeping giant hata kwa majirani zake, mtapiga kelele weee ila akiamka ni vilio na kuomba maridhiano.

Hapa Tanganyika ikisema "Sawa, Mzanzibari aende kwao na aingie Tanganyika kama mgeni, utaona vilio vya wazanzibari na hao hao kina Fatma usishangae wakapiga U turn wakalaani na kuingiza mambo ya haki na usawa, sisi ni wamoja.
 
Mwenye bendera ya Tanganyika please naiona nianze ipeperusha kwenye gari yangu
 
Ila hata jina lenyewe la Tanganyika lipo local sana, yaani la kishambashamba hivi tofauti na jina la Zanzibar linavyo sound vizuri.
Lina ushamba gani? Yale yale ya ukila viazi na mchuzi ni chakula local tofauti na ukila "potato mix stew." Tanganyika ni jina zuri sana.
 
So technically Tanzania ni Tanganyika mpaka uongelee mada ya Muungano ndio unakumbuka kuna kitu kinaitwa Tanganyika.

Huwa nawambia kila siku, Tanzania ni Tanganyika, hii kitu wazenji inawaua sana ndo maana wanajitahid kujitambulisha kila kukicha ili uwepo wao uonekane.
Mimi huichukulia Zanzibar kama moja ya Majiji makubwa nchini Tanganyika🤣
 
M
Zanzibar ndo hawajitambui ndo maana tumewafanya ni koloni letu
Maneno hayavunji mfupa.na mwenye macho haambiwi tizama,usichokijua ni usiku wa Giza,watanganyika wanapenda sana kusifiwa,kama hiiivi,hivi!;kama sio sisi,wale si kitu wengi wao wamejaa huku wanamiliki mashamba,migodi,biashara,makazi,Kwao tunaenda na passport.
 
Aahaa, kumbe! Kama ni hivyo ngoja na watanganyika waamke waanze kuuthamini utaifa wao.
 
Wazanzibari always wako proud kuitwa Wazanzibari, sijui kwanini sisi Watanganyika tukiitwa Watanganyika huwa tunakasirika na kuona kama tunabaguliwa?
Sio wote, Mbona Watu wa Arusha wanajibrand kuwa Watanganyika?
 
Tanganyika haikufa, ipo hai tena ina nguvu zake imara. Zanzibar kuachiwa madaraka yake ni zuga tu isijione inatawaliwa na dude kubwa lenye nguvu za ajabu tanganyika
 
Wazanzibari always wako proud kuitwa Wazanzibari, sijui kwanini sisi Watanganyika tukiitwa Watanganyika huwa tunakasirika na kuona kama tunabaguliwa?
Tatizo jina. Tanzania imekaa poa. Na Zanzubar imekaa poa. Tanganyikaa... 🤔
 
Back
Top Bottom