Fatma Karume: Tatizo Watanganyika hawajitambui utaifa wao, sisi Zanzibar hatuwezi kufuta utaifa wetu

 

Attachments

30 April 2024
AMOS MAKALA AJITOSA MZIMA MZIMA, AMVAA TUNDU LISSU - "ANAENDESHA SIASA UCHWARA" NI JUU YA KAULI ZAKE KUHUSU RAIS WA MUUNGANO ...


View: https://m.youtube.com/watch?v=YkE6D7YnygE
Katibu uenezi, itikadi na mafunzo wa chama kongwe dola CCM ndugu Amos Makala .... azungumzia juu ya nchi moja tu tulionayo... huku kuna nchi mbili yaani Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zilizonda taifa moja ...

Amos Makala anasikitishwa na kauli kuwa rais Samia Suluhu Hassan ni mzanzibari na kuwa uzanzibari wake .....

Kuhusu chawa wengi ....
 
✅NANI ANAFAIDIKA NA MUUNGANO?
✅NINI FAIDA ZA MUUNGANO?
✅KWA NINI TUWE NA MUUNGANO TULIONAO?
✅NINI KIFANYIKE KUUFANYA MUUNGANO KUWA BORA ZAIDI?
✅MAPUNGUFU YA MUUNGANO TUNAYATATUAJE?

Wananchi wanapaswa kuelimishwa zaidi kuhusu Muungano wetu kuliko kutishwa ama kufumbwa macho,midomo,masikio..
 
Wamshukuru Nyerere kwa kuwaachia Nchi yao kuitwa Zanzibar.
Hata hivyo yeye ni mtu wa Malawi atulize mshono.
 
Asante
 
Katika nchi zote zilizoungana utaifa wa kwanza ni ule wa Muungano. Ndio maana m Quebecois akiwa nje ya Canada atajitambulisha kama mCanada halafu kama mQuebecois. Aidha, mtu wa Texas akiwa nje ya Marekani atajitambulisha kama Mmarekani, na sana sana Mmarekani anaetoka Texas. Au muingereza akiwa nje atajiita British lakini akiwa ndani English, Scot, Welsh au Northern Irish. Akiwa Marekani atasema yeye kwao ni Texas. Wakina Fatma kwa kujitambulisha kwanza kuwa wao ni uzanzibari ni kuonyesha identity yao ni uzanzibari kuliko utanzania. Sisi tunaoishi bara hatuwezi kujiita wa Tanganyika au Tanzania Bara kwa sababu hizo hazipo. Sisi tutajitambulisha kama watanzania tu. Wao kama wana prioritise uzanzibari wao basi wasishangae kama loyalty yao kwa watanzania wasio wazanzibari ikatiliwa shaka. Hakuna mtu anawakataza kujivunia uzanzibari lakini isiwe at the cost ya utanzania.

Amandla...
 
naunga mkono hoja ya shangazi. ccm ndio mchawi mkuu hapa.
 
Katibu uenezi, itikadi na mafunzo wa chama kongwe dola CCM ndugu Amos Makala ..

Huyu katibu uenezi wa chama kongwe dola CCM ameshindwa na kufeli vibaya sana katika kujibu hoja za Tundu Lissu na za Fatma Karume zilizozungumzia utaifa na uraia wa Tanganyika na ule wa Zanzibar
 
Mijadala mizuri sana sielewi kwanini CCM hawataki kusikia?
 
Hakuna muugano Bali ni kichaa cha maccm kuficha katika wizi wa Mali Za watanganyika.
 
Zanzibar ndo hawajitambui ndo maana tumewafanya ni koloni letu
Akili nyingi mbele kiza, koloni letu baadae limetutawala tunabaki kulialia Wazanzibari wanauza ardhi yetu kwa wajomba zao.
 
Siyo lazima upande juu ya bati na kupayuka kuwaambia majirani wewe ni baba mwenye nyumba.Tutamuona mkeo tumbo lake linavyoumuka tu.
NB;Fatma anatulisha sumu tuchukie na kuweweseka.
Fatma anawaamsha mjitambue nyinyi ni Watanganyika. Msione aibu kujiita Watanganyika.
 
Wazanzibari always wako proud kuitwa Wazanzibari, sijui kwanini sisi Watanganyika tukiitwa Watanganyika huwa tunakasirika na kuona kama tunabaguliwa?
Wazanzibari wamekuwa Wazanzibari kwa zaidi ya miaka 200 na ndio maana wanaojivunia Uzanzibari wao. Wana utamaduni wao, lugha yao, chakula chao, michezo yao, dini yao na kadhalika. Wewe Mtanganyika nchi yako ilidumu miaka mitatu tu. Una cha kujivunia zaidi ya Utanzania?
 
Fatma Karume yupo sahihi
 
Huwa nashangaa sana watanganyika kuitwa watanzania na wazanzibar kuitwa wazanzibar ikiwa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar.

Waasisi wa Tanzania walidhamiria nini hasa kuacha nchi Moja na utambulisho wake na nyingine kuipokonya utambulisho wake!?

Ina maana viongozi wa Tanganyika walishindwa kuliona hili awali wakalirekebisha au ilikuwa ni sehemu ya mpango wao kutuachia utaifa usio na uhalisia!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…