Baada ya kusikia kelel nyingi juu ya suala la ESCROW, Nimepitia taarifa mbalimbali zinazohusu suala la fedha za account hii ya EScrow kwa upole, utulivu, unyenyekevu na bila ushabiki. Katika taarifa hizo nimepata kuelewa kuwa fedha za Escow si za umma, wala hazijaibiwa ka namna yoyote. Bali fedha hizi ni mali ya kampuniya IPTL kupitia kampuni tanzu mbili yaani Menchmar na VIP.
Kwa muda wa zaidi ya miaka miwili kumekuwapo na mgogoro wa waziwazi wa kimaslahi kati ya wamiliki wa IPTL ambao ni kampuni ya VIP na kampuni ya Mechmar kutoka Malaysia. Tuliokuwa tunafuatilia habari, hili si jambo geni
Cha ajabi kwangu, watu wengi wanashabikia bila kujua wala kujali kufuatilia kuwa account ya escrow ilianzishwaje. Taarifa zilizowazi zinaonyesha kwamba Mahakama Kuu, kufuatia mgogoro uliokuwepo, iliamua pande zote mbili yaani VIP na Mechmar zisaini hati ya makubaliano juu ya kutunza fedha za malipo ya kila mwezi ya umemeyatokanayo na umeme unaozalishwa na IPTL na kuiuzia TANESCO. Mpaka hapo nadhani wenzangu mmeanza kupata picha ya hili suala sumbufu.
Taarifa zinaonyesha kuwa, mahakama ilielekeza malipo hayo yahifadhiwe katika akaunti hiyo mpya ya ESCROW iliyofunguliwa Benki kuu hadi mgogoro kati ya wabia hawa wawili utakapoamriwa. Mpaka hapo ndugu zangu, ikiwa taarifa hizi ni za kweli, mtakubaliana nami kuwa fedha za ESCROW ni mali ya IPTL. Yaani MENCHMAR na VIP. Zaidi ni majungu na wivu.
Sasa tujiulize mgogoro upo wapi? walalamikaji ni akina nani? fedha ambazo TANESCO imeridhia kulipia huduma inayotolewa kwa kazi ambayo imeshafanywa zinakuwaje fedha za umma?Ijulikane kuwa malipo yoyote ya taasisi nyeti kama TANESO hufanywa kwa kufuata taratibu na kuzingatia kanuni. maana yake malipo yale ni malipo halali kwa kazi halisiiliyofanywa.
Mwenzenu nimeona kuwa yawezekana jambo hili ni zaidi ya haya yanayotaarifiwa kwa uwazi.Pengine kuna nguvu inayoendesha mambo nyuma ya pazia. Suala lenyewe hapa lipo katika swali la kwanini baadhi ya viongozi wa umma wamepata mgao (Kama kweli wamepata, mimi hainihusu wala sina muda wa kuwaonea wivu). Hata hivyo bado hakuna sababu dhahiri ya kuziita fedha za ESCROW kuwa ni za umma. Zinabaki kuwa ni malipo ya umeme ambao TANESCO imeridhia kuwa umezalishwa na IPTL
Najua ni rahisi kuzusha mambo na kuyafanya yawe ni mjadala mkubwa katika jamii ya watu waliokosa mweleke na kukata tamaa. Wengi wetu tuna madeni, mipango yetu na njozi zetu zimevurugika... katika hali hii ni rahisi kupenda habari za uzushi zaidi kuliko za kweli na zenye tija. Lakini katika suala hili la fedha za Escrow...pesa hizo ni za IPTL.
Nahisi kuna mvutano wa makundi ya kisiasa. Lakini, ndugu zangu, kwa wanasiasa, muda huu ni muda wa kujipambanua. wale ambao watashindwa katika medani za ushindani katika mchezo huu rahisi, yamkini hata kuwa viongozi wa umma hawafai. Mimi niweke wazi, kama ningekuwa ni PM au AG nisingekubali kujiudhuru kwajambo lisilonihusu mimi wala kuuhusu umma, hata kama nimepokea fedha za ESCROW kwa maendeleo ya umma.
Mwenye taarifa tofauti atuletee hapa.... uzushi uwekwe pembeni, matatizo binafsi yawekwe pembeni...ebu tupeni raha ya kusoma vigezo na ukweli, si uzushi na kejeli. Suala hili limenipotezea muda kulifuatilia ili nione uhalisia ulipo...kumbe twajadili mipasho na uzushi. jambo hili si jema kwa ustawi wa jamii inayoheshimu utu, sheria na misingi ya utawala bora.