Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL (Tegeta Escrow account), ni mali ya umma


Hivi hiyo 1.6 bn unayozungumzia imetoka kwa Akaunt ya nani??,Nnavoona wengi hawajui hata wanachojadili ukija kwenye sakata la Escrow..Mtu hujui Historia ya IPTL,Hujui Escrow akaunt kwa nini ilifunguliwa na lini,hujui ilifungwa lini,hujui kipindi inafungwa kulikuwa na makubaliano yapi baina ya wabia,hujui mahakama ilitoa agizo gani kwenye hilo, hujui riport ya CAG itakuwaje.Kila kitu hujui alafu unaandika mashudu tu hapa....
 

hili linaeleweka ingawa baadhi ya watu wanajitoa ufahamu na kudhani IPTL ni mali ya umma na hivyo hawakustahili kulipwa na umeme tuliotuma miaka kumi na moja tutumie bure
 

kweli mkuu hawa jamaa ni vilaza na wanalenga kupotosha umma kwa makusudi
 
kujandili escrow unatakiwa uwe mtu kama mwendawazimu kuna watu wanaielezea vizuri sana kuwa hela hizo si za uma lakini wanaosema hela umma hawafafanui utasikia watoke wajiuzuru

wanafahamu ila wanajitoa ufahamu hawa wadudu, ila jumatatu upuuzi huu utaisha na ukweli utawekwa wazi
 
[h=2]Saturday, 22 November 2014[/h] [h=3]SAKATA LA ESCROW BUNGE KULIPUKA[/h]
SAKATA la akaunti ya Escrow limezidi kuchukua sura mpya, baada ya kuibuka mambo mazito ikiwemo taarifa za baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) kudaiwa kuchukua rushwa kwa kampuni ya Independet Power Limited (IPTL).

Taarifa hiyo imekuja wakati ripoti ya uchunguzi wa akaunti hiyo ikitarajia kusomwa ndani ya bunge, ambapo imeelezwa kuwepo kwa makelele mengi ndani ya bunge kunatokana na baadhi ya wabunge kukosa mgawo wa fedha na wengine na wao kuchukua rushwa.

Nyaraka za malipo, ambazo gazeti hili ilizipata ambazo zinamuhusisha mtumishi wa bunge ambaye ni mmoja wa makatibu wa kamati ya PAC, Beatus Malima na wakili wa Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe aitwaye Alberto Msando, ambao walichukua milioni 10 kila mmoja kwa nyakati tofauti na kuzipeleka kwa wajumbe PAC ili waandae Ripoti itakayoonyesha kwamba kwenye IPTL haina Tatizo.

Katika vocha ya malipo iliyotoka PAP inamuonyesha April 8, 2014 Wakili Msando alipokea sh. milioni 10 kwa ajili PAC na Zitto kuandaa majibu ya malalamiko ya kampuni ya MECHMAR dhidi ya IPTL/PAP kazi ambayo inasemekana zitto aliifanya Machi 28, mwaka huu.

Taarifa zaidi zinaonyesha kwamba tarehe hiyo, mtumishi wa bunge anayefanya kazi na Kamati ya PAC, Beatus Malima naye alichukua kiasi kama hicho cha fedha kwa kazi hiyo hiyo

Msando alitambulishwa na Zitto kwa uongozi wa IPTL/PAP kama mshauri wake wa kisheria na mwanasheria hivyo chochote atakachowaambia ni maagizo kutoka kwake, ambapo Zitto alimtambulisha kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sethi baada ya kikao kirefu walichokifanya yeye na zitto kabla ya Mwenyekiti huyo wa PAC hajasafiri kwenda India kwenye matibabu ya marehemu mama yake, siku chache kabla ya malipo haya hayajafanyika.

Mmoja wa wabunge, ambaye hakupenda kutaja jina lake, alisema hili suala lina makandomakando mengi na wala si hayo yanayozungumzwa kwa kuwa PAP waliipata IPTL kwa kufuata taratibu zote kisheria pamoja na malipo waliyopewa katika akaunti ya Escrow yalikuwa halali kwao.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wakili huyo na mtumishi huyo waliendelea na utaratibu wa kuwa wanachukua pesa IPTL kwa sababu mbalimbali na mwishowe kuwapa maagizo kwamba itabidi PAC walipwe kiasi cha billioni 1.5 ili wazuie mjadala uliotarajia kuibuliwa kipindi hicho kuhusu sakata hilo.

"Hawa jamaa wanaonewa kwa kuwa kuna kundi kubwa la wafanyabiashara nyumba ya IPTL, ambao waliitaka kampuni hii lakini wameshindwa. Hawa hawana makosa yeyote na kinachofanyika ni kuwaonea na mvutano uliopo kwa wale waliokosa mshiko wao ndio wanatumiwa,''alisema mbunge huyo.

Mbunge huyo, alisema "hebu fikiria, kama wangepewa hizo pesa walizoomba, je IPTL ingekuwa halali leo machoni mwao?, kwanini wawatese watu wasio na hatia kwa uroho na njaa zao binafsi?, ninakuhakikishia safari hii hatutakubali bunge kutumiwa kama kichaka cha watu kutimiza matakwa yao ya kisiasa baada ya kukosa hongo walizoomba" alisema.

Hivyo, alisema wabunge wengi wamejiandaa kueleza ukweli ndani ya bunge pamoja na kutoa mawasiliano ya simu kati ya wajumbe wa PAC na baadhi ya wabunge kuwaomba wawape nguvu katika suala hilo, pamoja na mawasiliano ya fedha kwa viongozi wa PAP yalivyokuwa yakifanyika.





HABARI MOTO: SAKATA LA ESCROW BUNGE KULIPUKA


SOURCE GAZETI UHURU, JAMII FORUMS
 
Bado naendelea kukusanya idadi ya misukule sugu ya magamba nikishamaliza hii kazi ntakuambia we ni msukule namba ngapi!!.

bora misukule inayoishi kuliko maiti iliyooza......mmmh kweli fumbo la mjinga ni kemi
 

jumatatu tutajua nani mzalendo, nani mwizi huyu zitto hajaanza leo huu wizi aulizwe iko wapi list ya wanaomiliki mabilioni uswis?,kaificha baada ya kupewa visenti vya kutuliza njaa yake,sasa amekwaa kisiki kwa iptl hajapata kitu, na njaa hii imemfukuzisha chadema na itamfukuzisha hata ACT anakopanga kukimbilia
 
Haya sasa kiko wap...??? PAC wameanza uumbuka nao duh!
 


Wewe jamaa ni tahira,kamueleze mkeo haya mambo
 

OK good ni za kwao..kwa nini wawagawie watumishi wa umma tena majaji,Mawaziri,wabunge?.Au hao wana hisa katika ile kampuni?

Jibu kwa fact kwani CAG alipokagua hesabu zao alitoa majibu gani??Si bure unaweza ukawa ni mmoja wa waliogaiwa.

Subiri uone zinavyowatokea puani ndo utatuambia ni kwa nini wana wajibika..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…