Fei Toto kukata rufaa rasmi CAS aomba mchango wa pesa kwa Watanzania

Fei Toto kukata rufaa rasmi CAS aomba mchango wa pesa kwa Watanzania

Yanga ni Taasisi ila wangeachana na hii ishu ya Faisal wamwambie aendelee na maisha yake amekosea ila sio kipindi cha kukomoana dogo alikosea na hajui kuwa kakosea waachane nae kuliko hizo mambo zinakokwenda...
Je ni wangapi wataitaji huruma kama iyo ikiwa utaratibu haufuatwi?
 
Baada ya Club ya Yanga kumuandikia barua ya wito Feisal Salum iliyoambatana na mashtaka dhidi yake mchezaji huyo amejitokeza, na kueleza wazi kuwa atapeleka kesi yake CAS kwani amenyimwa haki yake ya kuvunja mkataba na TFF!
Ameomba achangiwe na wote wenye mapenzi mema ili aweze kupata fedha kwa ajili ya kufungua kesi, mawakili wake watafanya kazi bure!
Kwa yeyote mwenye chochote anaweza kumsaidia kupitia Lipa namba 5406394 Feisal Salum.

Haya sasa huu mtanange nani mshindi huko CAS…!? Yetu macho cha msingi tumpe dogo mpunga!
Tatizo la kusajili mashoga Yanga linatugharimu
 
Kiungo wa klabu ya Yanga SC Feisal Salum kupitia ukurasa wake Instagram, ameuomba umma wa Watanzania na wapenzi wa soka kumchangia pesa za kulipia gharama za kufungua jalada la kesi yake kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

“Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heros.

Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki i yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS.

Nahitaji Mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, Heshima na Haki zao. Naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili niweze kupata pesa ya Kulipia gharama za kufungua Jalada la kesi yangu CAS ili kupata Haki yangu ya Kuondoka Yanga kwa kuvunja mkataba.

Tafadhali naomba unichangie ili nipate haki yangu itakayoniwezesha kutumikia kipaji changu na Timu za Taifa (Tanzania na Zanzibar) katika namna tofauti kwa manufaa yangu na Taifa. Shangazi Fatma Karume na wanasheria wengine watafanya kazi Bure.

Unaweza kulipia kwa lipa namba (5406394 FEISAL SALUM) hapo pichani au kwa namba hii ya simu kwa kwa Tigo Pesa 067 912 8899 FEISAL SALUM ABDALLAH.

NAOMBA UNICHANGIE” ameandika Feitoto.
 
Alipokuwa analipwa mshahara wa milioni nne kwa mwezi alikuwa anakula ugali na sukari. Saivi mshahara anatumiwa anaukataa, je maisha yake anaishi vipi kama hakuna watu nyuma yake?

Na kwenda CAS ni haki yake hakuna mtu anaweza kumuhoji kapataje ela za kwendea huko kwasababu hata sasa hakuna mtu aliyefatilia kujua anayekula ugali na sukari anapataje milioni 300 ku deposit kwenye account ya Yanga.
Mtu anayeishi kwa ugali na sukari kipindi analipwa mshahara wa milioni nne je leo hii anaikataa milioni nne atakuwa na hali gani au anaishije. Ila yeye mwenyewe tu kajistukia
Milion 300 ipi ambayo ilikuwa deposited kwenye account ya Yanga?
 
Yanga ni Taasisi ila wangeachana na hii ishu ya Faisal wamwambie aendelee na maisha yake amekosea ila sio kipindi cha kukomoana dogo alikosea na hajui kuwa kakosea waachane nae kuliko hizo mambo zinakokwenda...
Ww mbona naye kama Feisal, haujielewi ...we unadhani kwann Yanga wanakata kumuachia?
 
Ameandikiwa huyu dogo!!hana uwezo wa kujieleza kiasi hiki kuna mkuda tuu ndio kaifanya hii kazi,alafu alivyo mpuuzi anatafuta huruma ya wananchi kwa kumuweka na Mama yake kwenye ujinga wake,,sasa mara mama anatukwana,,mara tff wameshindwa kumsaidia na hawamsikillizi,,,mara anahitaji michango,,,,mara haki kwa wachezaji wa ndani,,Sasa haeleweki anahitaji nini,,,anazidi kujidhalilisha huyu dogo wa visiwa vya Urojo!!!
 
Milioni 112 mkuu
Hapo CAS wanataka 50+m tu,inayobaki anaendelea kula ugali na sukari.

Dogo igizo lake alichemka kutengeneza scripts mwanzoni,sasa hivi anajikaanga mwenyewe kwa mafuta yake.

Dj walete Kolo FC wamchangie.
 
Sasa yanga inamng'ang'nia nini kama hataki kucheza? Wavunje tu mkataba kijana wa watu akacheze kwingine
 
Ww mbona naye kama Feisal, haujielewi ...we unadhani kwann Yanga wanakata kumuachia?
Mkuu mambo ya kujielewa yanatoka wapi ni kama Morrison tuu leo mahakamani kesho tunae tena...ukiwa mtu wa futbal dharau acha maana ukiulizwa kipi kinachokupa kiburi huna hata sehemu ya kushika...
 
Bantu Lady
Antonnia
Screenshot_20230525-195427.png
 
Back
Top Bottom