Fei Toto kukata rufaa rasmi CAS aomba mchango wa pesa kwa Watanzania

Fei Toto kukata rufaa rasmi CAS aomba mchango wa pesa kwa Watanzania

Baada ya Club ya Yanga kumuandikia barua ya wito Feisal Salum iliyoambatana na mashtaka dhidi yake mchezaji huyo amejitokeza, na kueleza wazi kuwa atapeleka kesi yake CAS kwani amenyimwa haki yake ya kuvunja mkataba na TFF!
Ameomba achangiwe na wote wenye mapenzi mema ili aweze kupata fedha kwa ajili ya kufungua kesi, mawakili wake watafanya kazi bure!
Kwa yeyote mwenye chochote anaweza kumsaidia kupitia Lipa namba 5406394 Feisal Salum.

Haya sasa huu mtanange nani mshindi huko CAS…!? Yetu macho cha msingi tumpe dogo mpunga!
Nitamchangia[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga mtupu.

Hao CAS nao mnawaona wajinga hivi eti?

Huyu hata aende jehanamu hawezi sikilizwa. Hakuna mtu atakuruhusu uamke asubuhi eti sababu kajitokeza tajiri akupe hela basi uvunje mkataba katikati ya msimu.

Feisal unadanganywa na unadanganyika kindezi sana dogo.

Kitu kimoja ukumbuke, mwisho wa siku ni wewe ndio unaathirika na si mawakili wako, si Fatma Karume wala sio mashabiki wa kolowizad wanaokujaza ujinga. Hao niliowataja kila mtu yuko na ajira yake mind you!
Mtoto mpumbavu Sana huyu akili Hamna hata kidogo
 
Mshahara anarudisha kila mwezi
Mshahara upi? Mnawajua Yanga nyie? Mchezaji haondoki Yanga hadi kwa kesi na malumbano viongozi wa hii timu ni wa hovyo Sana halafu wanarithishana hii tabia ya hovyo ya kung'ang'ania wachezaji, mchezaji kachoka/kavunja mkataba awalipe kwa kukiuka mkataba aende zake sio kujidhalilisha namna hii, Mimi nilijua wamepata Engineer labda ataleta mabadiliko kumbe walewale Tena anasema anapeleka mshahara unarudi [emoji44][emoji44] wamwache aondoke
 
Apite dukani kwangu nitamchangia sukari nusu kilo.
Kutoa ni moyo.
 
Akitokea FIFA wamemlima faini tutaendeleza mchango. Zile milioni 100 alizoweka kwenye akaunt ya Yanga baadae YANGA walimrudishia kashazimaliza?
 
Kwa mlioanza kufatilia mpira na madudu yake siku za karibuni mnaona ajabu kumbe hayo madudu yapo toka enzi za kina Method Mogela,Iddfonce Amlima sema vijana wa leo mnaona ajabu hiyo ya huyo dogo na Yanga watalimaliza hilo...
 
Kwamba mshahara wa milioni 4 kwa mwezi ni ndogo? Halafu unakuta mtu anayeongea hayo mshahara wake amezidiwa na Feisal zaidi ya mara mbili.
Naongea kimichezo mkuu siongelei ushabiki nilichoandika kina maana kubwa kuliko ulivyokibeba niishie hapo.
 
Hivi zile milion 160 sijui alizowapa Yanga kuvunja mkataba nao wakamrudishia zilienda wapi? Si atukie hizo hizo tena zinazidi sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mshahara upi? Mnawajua Yanga nyie? Mchezaji haondoki Yanga hadi kwa kesi na malumbano viongozi wa hii timu ni wa hovyo Sana halafu wanarithishana hii tabia ya hovyo ya kung'ang'ania wachezaji, mchezaji kachoka/kavunja mkataba awalipe kwa kukiuka mkataba aende zake sio kujidhalilisha namna hii, Mimi nilijua wamepata Engineer labda ataleta mabadiliko kumbe walewale Tena anasema anapeleka mshahara unarudi [emoji44][emoji44] wamwache aondoke

Umeandika nini? Wacha hili lifike mwisho ili tuone kati ya viongozi wa Yanga na Feisal ni upande upi upo sahihi.
Viongozi wa timu ni wa hovyo sana lakini hao hao wa ovyo imeifanya timu icheze fainali ya michuano ya CAF confederation cup msimu huu, na ubingwa wa ligi tayari mkononi misimu miwili mfululizo na Azam Federation wanaitetea, je viongozi wenu wa maana wamewafanyia nini? Kuahidi kuifunga Yanga? Au kumleta Manzoki kuwa ajenda ya kupsta kura?

Yanga wanachokitaka utaratibu ufuatwe ikiwa ni mchezaji kufika klabuni ili waongee kuhusu kuvunja mkataba je huyo Feisal wenu alifanya? Mkataba ulisainiwa na pande mbili, hivyo hata kuvunja lazima pande mbili zikae mezani zifikiane kuuvunja mkataba. Mbona ishu ni nyepesi tu ila kwasababu ya ujeuri wa huyo dogo na maneno mnayomjaza ndio inaifanya ishu iwe kubwa.

Endeleeni kujipoza na mikataba ila mkumbuke Yanga inscheza fainali ya michuano ya CAF
 
Yanga ni Taasisi ila wangeachana na hii ishu ya Faisal wamwambie aendelee na maisha yake amekosea ila sio kipindi cha kukomoana dogo alikosea na hajui kuwa kakosea waachane nae kuliko hizo mambo zinakokwenda...
Haya mambo ya kuoneana huruma ndo yameharibu sekta karibu zote hapa nchini.....watu wanaiba, wanahujumu, wanakiuka kila aina ya taratibu kwa manufaa yao! Acha kwenye hili iwe fundisho kwa mengine na wengine pia!
 
Nadhani Feisal hajawajua vizuri watanzania, Watz watakushangilia wakiwa wanufaika nawewe ila saizi anatafuta public sympathy kumbe watu hawana habari naye.......Yanga ni kubwa sana......akamuulize Singano a.k.a Messi baada ya mgogoro na Madunduka saizi anauza kahawa mtaani 😀😀
 
Mshahara upi? Mnawajua Yanga nyie? Mchezaji haondoki Yanga hadi kwa kesi na malumbano viongozi wa hii timu ni wa hovyo Sana halafu wanarithishana hii tabia ya hovyo ya kung'ang'ania wachezaji, mchezaji kachoka/kavunja mkataba awalipe kwa kukiuka mkataba aende zake sio kujidhalilisha namna hii, Mimi nilijua wamepata Engineer labda ataleta mabadiliko kumbe walewale Tena anasema anapeleka mshahara unarudi [emoji44][emoji44] wamwache aondoke
Singano,Yondani waliondokaje Simba au ndiyo nyie vitoto vya 2005?
 
Back
Top Bottom