Fei Toto kukata rufaa rasmi CAS aomba mchango wa pesa kwa Watanzania

Fei Toto kukata rufaa rasmi CAS aomba mchango wa pesa kwa Watanzania

Je ni wangapi wataitaji huruma kama iyo ikiwa utaratibu haufuatwi?
Naona ni kama mambo ya Morrison tuu haya baada ya muda unaona yupo Yanga tena...nishafatilia hizo mambo toka Hamis Gaga mpaka leo huyu najua watakakoishia...
 
Afate taratibu, alisaini mkataba, kuvunja Kuna masharti, mi mwenyewe Kuna kazi nilivunja mkataba naogopa hata kudai sent nccf lazima utaambiwa uende kazini kwako kwa zamani upewe barua na hawawezi kunipa , malizia mkataba wako kwanza, Najua nimeharibu mwenyewe, najua nikienda timbwili lake na hivi hawakutaka niondoke, [emoji17]
 
Ningemchangia ila ametuzalau kama analipwa million 4 anakula ugali nasukari sie machinga ndio tutamuda kwel kumchangia
 
Yaani unamchangia mtu ambaye alikubali kufanya kazi mwenyewe kwa malipo ya milioni 4 lakini leo anajiona hayupo sahihi kusaini huo mkataba wa ela ndogo kwake.
Leo namchangia mtu anayeona milioni 4 ni ndogo kwake je mimi nafikisha mshahara wa kiwango hiko? Je ndugu zangu wameshatosheka na michango yangu? Huyo aliyemwambia avunje mkataba ndiye atakayemsaidia kumpeleka CAS
 
Mchangieni nyie mashabiki wa ujinga
Mpoteze hizo pese
 
Wanathiiimbaaaaa mnaitwa huku mumpe maua yake baada ya kumpambania asicheze tena Yanga
 
Hapo CAS wanataka 50+m tu,inayobaki anaendelea kula ugali na sukari.

Dogo igizo lake alichemka kutengeneza scripts mwanzoni,sasa hivi anajikaanga mwenyewe kwa mafuta yake.

Dj walete Kolo FC wamchangie.
Nani kakudanganya?

Kwa hiyo pesa labda kama umeongelea endapo Yanga watakubali kutoa.

Lakini since Yanga hana maslahi kwenye hii case hivyo hawezi kutoa hiyo hela. Badala yake Feisali inatakiwa awalipie Yanga ambapo ni jumla ya dola 40,000 kwa ajili ya kufungia kesi.

Bado kuna gharama nyingine za ziada kwa ajili ya kuendeshea kesi
 
Management yake imevurugwa kabisa, milioni 55 wanakosaje? Wakati alitaka kuvunja mkataba 110milioni? Anachukua hapo na chenji inabaki......zile training za Dubai nazo alichangiwa? Mpira wa Tz unasiasa zake ila wewe Siasa zako nikama za Lipumba kabisa......
 
Yanga ni Taasisi ila wangeachana na hii ishu ya Faisal wamwambie aendelee na maisha yake amekosea ila sio kipindi cha kukomoana dogo alikosea na hajui kuwa kakosea waachane nae kuliko hizo mambo zinakokwenda...

Childish comment, by doing so Yanga will be setting precedence that will bite them in future.
Dogo sio lazima u- comment.
 
Kwa mshahara upi aliokuwa anaupata Yanga?
Kwamba mshahara wa milioni 4 kwa mwezi ni ndogo? Halafu unakuta mtu anayeongea hayo mshahara wake amezidiwa na Feisal zaidi ya mara mbili.
 
Nani kakudanganya?

Kwa hiyo pesa labda kama umeongelea endapo Yanga watakubali kutoa.

Lakini since Yanga hana maslahi kwenye hii case hivyo hawezi kutoa hiyo hela. Badala yake Feisali inatakiwa awalipie Yanga ambapo ni jumla ya dola 40,000 kwa ajili ya kufungia kesi.

Bado kuna gharama nyingine za ziada kwa ajili ya kuendeshea kesi
Kuna gharama zipi wakati zinafanyika online gharama Bundle.

Ila upo vizuri yaani mpaka maamuzi ya CAS ushayajua yatakuwaje ,daaah umetisha kaka.

Ila yakiwa kinyume chake hamchelewi kusema Yanga kaiweka CAS mfukoni.
 
Hivi zile milion 160 sijui alizowapa Yanga kuvunja mkataba nao wakamrudishia zilienda wapi? Si atukie hizo hizo tena zinazidi sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Upuuzi mwingine huu, yaani usimpe yatima, mjane uje umpe mchango mpuuzi anayeshinda beach?.
 
Baada ya Club ya Yanga kumuandikia barua ya wito Feisal Salum iliyoambatana na mashtaka dhidi yake mchezaji huyo amejitokeza, na kueleza wazi kuwa atapeleka kesi yake CAS kwani amenyimwa haki yake ya kuvunja mkataba na TFF!
Ameomba achangiwe na wote wenye mapenzi mema ili aweze kupata fedha kwa ajili ya kufungua kesi, mawakili wake watafanya kazi bure!
Kwa yeyote mwenye chochote anaweza kumsaidia kupitia Lipa namba 5406394 Feisal Salum.

Haya sasa huu mtanange nani mshindi huko CAS…!? Yetu macho cha msingi tumpe dogo mpunga!
Kuna wengi wenye uhitaji wa kusaidiwa Ila sio kwa upuuzi huu...ni Bora kusaidia wagonjwa kuliko hiki kiburi, yani kimeshindwa kusema samahani wakamaliza Mambo kinataka kuchangiwa? Upuuzi mtupu na sijui anajiona nani
 
Baada ya Club ya Yanga kumuandikia barua ya wito Feisal Salum iliyoambatana na mashtaka dhidi yake mchezaji huyo amejitokeza, na kueleza wazi kuwa atapeleka kesi yake CAS kwani amenyimwa haki yake ya kuvunja mkataba na TFF!
Ameomba achangiwe na wote wenye mapenzi mema ili aweze kupata fedha kwa ajili ya kufungua kesi, mawakili wake watafanya kazi bure!
Kwa yeyote mwenye chochote anaweza kumsaidia kupitia Lipa namba 5406394 Feisal Salum.

Haya sasa huu mtanange nani mshindi huko CAS…!? Yetu macho cha msingi tumpe dogo mpunga!
Bange ni mbaya sana.
Nilimuona kijana mwelewa na mwerevu sana kumbe kichwani majivu tu.
Kwa wito huo wa kamati anakwenda kuadhibiwa vibaya mno....faini na kifungo ndani na nje ya nchi HATOCHEZA.
Time Will tell.
 
Back
Top Bottom