Fei Toto ni mchezaji wa kigeni, Yanga ilifuata kanuni?

Wewe umesoma kiupandupande. Najua hayo mambo na najua kuwa ZFA iliomba tena kwa bidii kuwa mwanachama wa FIFA na ikakataliwa kwa kigezo kwamba si nchi inayotambulika kimataifa kwa kuwa na mipaka yake.

Zanzibar inatambuliwa CAF kama mwanachama mshirika na ingawa haina sifa kama Tanzania (kwa Timu za Taifa) lakini ligi yake ya vilabu ina sifa kama Ligi ya vilabu ya Tanganyika. Kwa ivo linapokuja suala la Ligi ya vilabu, Zanzibar inajitegemea.

Kujitegemea kwake ndiyo maana zile nafasi mbili za Klabu Bingwa (Simba na Yanga ) na zile mbili za Shirikisho (Azam na Geita Gold FC), haziwahusu Zanzibar bali zinazihusu timu za Tanganyika Pekee. Leo KMKM ikiongeza nafasi zitakuwa ni za Zanzibar peke yake, Tanganyika haitahusika.

Yanga ilifuata Kanuni?
 
Tuanze na TFF, kwanini kwenye zile kanuni za wachezaji 12 wa kigeni haziwahesabu wachezaji wa zanzibar kama ni wa kigeni?
 
Tuanze kuuliza, je hiyo timu ya Taifa ya Zanzibar ipo? Kama haipo ni kwanini?
 
Ifuate kanuni ipi mbona unajichanganya? Feitoto ni raia wa nchi gani?
 
Ifuate kanuni ipi mbona unajichanganya? Feitoto ni raia wa nchi gani?
Najichanganyaje? Wewe hujui kwamba kwenye mashindano haya inayoshiriki Simba na Yanga Zanzibar Mwakilishi wake ni KMKM. KMKM inashiriki ligi ya Tanganyika?

Klabu hazihamishi uraia zinahamisha uchezaji wa mtu. Chama alipotoka Simba kwenda Al ahly ya Misri, kibali chake cha uhamisho kilitolewa na chama cha soka Zambia au Tanzania?

Mambo ya Uraia hayapo kwenye uhamisho wa wachezaji. Yaani CR7 anatoka Juve kwenda Man U anaulizwa Uraia ama alikuwa anacheza ligi ipi? Yaani kwa kuwa ni Mreno basi uhamisho utoke Ureno!!

Leo hii itokee Mwamnyeto asajiliwe na Mamelod Sundown na kama hajamaliza mkataba wake akitaka kurudi Tanzania hata kama yeye ni mtanzania, ni lazima apate kibali cha Uhamisho toka chama cha soka cha Afrika ya Kusini.

Naandika ninachokijua siyo ninachokihisi,

Yanga ilifuata utaratibu wa kumhamisha Fei Toto??
 
Kwanini fei Toto kwanini ujauliza kuhusu Ninja, Kanavaro, Banka na wengine kibao ambao walishapita yanga miaka na miaka!!
 
Kwanini fei Toto kwanini ujauliza kuhusu Ninja, Kanavaro, Banka na wengine kibao ambao walishapita yanga miaka na miaka!!
Ndugu yangu kila jambo na wakati wake. Halafu hata mahakamani huwezi kusema kwa nini ushitakiwe wewe mwenye msokoto mmoja wakati unawajua walimaji wa bangi hawajashitakiwa. Hao kina Ninja na wenzake nilikuwa bado sijatanabahi kwamba kumbe Zanzibar wana Ligi yao inayojitegemea.
 
Tuanze na TFF, kwanini kwenye zile kanuni za wachezaji 12 wa kigeni haziwahesabu wachezaji wa zanzibar kama ni wa kigeni?
Hoja hapa siyo uraia, bali ni kucheza kwenye Ligi ya nchi nyingine. Kichuya ni Mtanzania lakini Simba ilipotaka kumrejesha toka Pharco ya Misri haikufanya hivyo kienyeji tu eti kwa kuwa yeye ni mtanzania.

Feisali alikuwa anacheza Kwenye Ligi ya Zanzibar isiyosimamiwa na TFF, sasa anapotaka kuja kwenye Ligi inayosimamiwa na TFF haitaji uhamisho wa Kimataifa?
 
Itakuwa vyema kama pia utapewa majibu kama Simba S.C nao wamekamilisha uhamisho wa kimataifa kwa goalkeeper Ally Salim maana nae pia ni raia wa nchi ya Zanzibar
 
Ligi ya Zanzibar inaitwaje mdau?
 
Kwahiyo Zanzibar ni nchi?
 
Zanzibar ni nchi?
 
Nyerere alituachia haya mazingaombwe yanayoitwa Muungano. Hata ukijaribu kuwaelekeza CAF wataona unawachanganya tu. Hakuna anayeelewa haya makitu.
 
Nimeupenda huu mjadala ila pia naomba nielekezwe kwa ajili ya afya ya uelewe wangu, kwan TFF ni mamlaka ya nchi gani?
 
Hili nalo CAF walitazame ngoja tuanze kukoleza [emoji91]

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…