Feisal penalty/fidia ya kutokutumikia mkataba inamsubiria

Kinachokuja kuleta utofauti ni consequences, kwa mtu aliyevunja kiholela kunakuwa na adhabu ya faini pamoja na kifungo. Lakini mkataba lazima uvunjike
Sasa tatzo la yanga hapa lipo wapi!? Fei si aende akakutane na yanga kama watampiga hizo faini si fresh tu? Kwann hataki kwenda?! ..

Huo mkataba unaosema ww ni lazim uvunjike yanga ipo tayari kwa hilo na TFF kama wenye dhamana ya kusimamia mpira wameshatoa muongozo kwamba Fei akamalizane na mwajiri wake(ambaye nao wana nia ya kuvunja huo mkataba kama wenyewe wanavyosema) Fei hataki kwenda kuuvunja analazimisha kuuvunjia kwenye kamati ambayo maamuzi yao yameshafungwa na sheria "functus offico" means option ni mbili tu zilizobaki aende CAS au Akamalizane na yanga

Yanga wanamuita kila siku hataki unataka asaidiweje huyu?
 
Yaan upewe mamlaka na mkataba wako kuuvunja hakuna kitu kama hicho
 
Kwanza rekebisha kumbukumbu zako.

Yanga ndio waliokuwa wakwanza kwenda TFF kumshtaki Feisali.

Notice ndio nini?

Na nani kati ya Feisali na Yanga ambaye unamtegemea awe na huo wajibu wa kuandika notice ya kushindwana kuwapelekea TFF?

Feisali kurudisha pesa ilikuwa ni matakwa ya kisheria ya uvunjaji wa mkataba na ndio maana ali quote na kifungu cha ndani ya mkataba. Ambapo kwa mujibu wa Yanga walidai kifungu hicho hakijitoshelezi peke yake.

Yanga ilimuita mezani sio kwa lengo la kuvunja mkataba.

Uwe unaandika vitu ambavyo unavijua sio kubahatisha.

Kwenye press release ya Yanga walisema walimuita Feisali kwa lengo la kuongeza maslahi yake.

Na hiyo ni baada ya kutangaza kutofurahia maisha akiwa Yanga.
 
Nikasomaje nawakati TFF hao hao wanasema feisal ana mkatana na Yanga
Tumia akili mambo mengine
Kwani mara ya kwanza TFF walipotoa uamuzi wao kuwa taratibu hazikufuata ikiwa wao hawajahusishwa.

Fei na mawakili wao wakarudi tena wakasema mkataba ukivunjika umevunjika hata kama utaratibu haukufutwa. Faini au adhabu ihusike, TFF walikataa kwa kuwa wao lazima wahusishwe kama chombo .

Haya wakaona ngoja tuombe idhini Kwa TFF majibu yaliyotoka ndiyo hayo
 
Tatizo la Yanga ni kuzidi kum consider kama mchezaji wao wakati ishabainika kavunja mkataba kinyume na sheria

Bodi ya TFF imefanya usanii na hili nililiona mapema kabisa
 
Tanzania pekee ndio chama cha mpira kina haki ya kuvunja mkataba, ila huko duniani ni mchezaji ndio anavunja mkataba
 
Ili uvunje makataba lazima Yanga wawe hawajamlipa mshahara na hawajamchezesha mechi kumi ndo angeweka hio milion 100 kama fidia ya kuvunja mkataba

Kama ameshavunja mkataba kwanin hana timu mpaka sahivi
Sikujua una upeo mdogo hivi
Dogo hataki tena kucheza mpira kwanini unalazimisha awe na timu? Anataka kwenda njombe kulima maparachichi
 
Mbona mnalazimisha kubaki na mtu ambaye amewakataa?

Nani analazimisha? Yanga since day One walimwambia wakae mezani wajadiliane jinsi ya kuvunja mkataba na siyo kukurupuka unauvunja mkataba facebook/instagram na kuingiza pesa bila kukaa mezani na mwajiri wako,inaonekana haujawahi kufanya kazi zenye mikataba wewe....Ukitaka kuacha kazi lazima utoe notice kwa mwajiri either 1 month or 24 hrs ila huyu Amijei yeye hajatoa notice wala nini yeye kadumbukiza fedha kisha akavunja mkataba Instagram/facebook.

Mikataba ya mipira ipo wazi haivunjwi kienyeji enyeji ,ingekuwa inavunjwa kienyeji enyeji ipo siku utakuta simba mmebakia na MO tu,wachezaji wate wamevunja mkataba facebook nyinyi mkakuta fedha kwenye account halafu hapo hapo mna mechi ndani ya siku 3,utafanyaje?

Amijei amekurupuka ,wamemdanganya ,asichokijua mshahara ni bargaining kati ya mwajiri na mwajiriwa ,ndiyo maana wote mnaweza kuwa same position lakini mkazidiana mishahara ,kama yeye aliona analipwa kidogo kuliko azizi ki ,mkataba ulipoisha hapo mwanzo asingeongeza.
 

Elimu Elimu Elimu ,Nyerere alizungumzia Umuhimu wa katiba ,Katiba ndiyo sheria Mama ,Hauwezi kukurupuka asubuhi umepata ushauri kutoka kwa mkeo halafu unakuja kuiplement nchini ,hii nyerere alimaanisha lazima ufuate katiba/sheria na si kukurupuka.

Ni kweli mkataba una pande mbili na kati ya hiyo yoyote anaweza kuvunja na kila pande kuna taratibu hata mwajiri akikurupuka tu kuvunja mkataba inabidi akulipe pesa ndefu sana kama hajafuata taratibu ,the same kwa fei(mwajiriwa) hawezi kukurupuka kuvunja mkataba bila kufuata sheria ,mwajiri akitaka kuvunja mkataba kwanza inatakiwa aongee na mwajiriwa kisha atoe notice ya mwezi mmoja kwamba mwezi ujao sitoendelea na mkataba kisha ampe stahiki zake kimkataba na hivyo hivyo mwajiriwa akitaka kuvunja mkataba inabidi atoe notice kwa mwajiri wake either 1 month notice or 24 hrs ,Sasa Amijei yeye alilipa tu fedha kisha akavunja Mkataba instagram/facebook hajakaa mezani wala kuwapa taarifa waajiri kama ana nia ya kuvunja mkataba.
 
Ulikuwa hujamfahamu tu. Ni Aina ya watu àmbao ukiwaheshimu Sana wanakudhalilisha.
 
Huyo dogo ni wa kumnyoosha tu ili wajinga wanaopotosha wajinga wa aina yake waje na mbinu mpya pia iwe fundisho.
 
Yule mchezaji wa Brighton Moises Ceicedo aliyekuwa akitakiwa na Arsenal.

Arsenal walipeleka ofa mbili na kukataliwa na Brighton uku mchezaji akiutangazia uma anataka kuondoka Brighton na kujiunga na Arsenal na mpaka Sasa anakipiga pale Brighton.

Kwanini Moises Ceicedo asitumie mbinu ya Feitoto Kuvunja mkataba kwakutumia icho kipengele Cha FIFA Cha kua na Sababu au kutokua na Sababu za Kuvunja mkataba Ili aweze kwenda Arsenal ki ulaini?
 
Hata umuelewshe vipi hawezi kukuelewa anaongozwa na ubishi kila siku anaeleshwa humu amekaza shingo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…