Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Hivi si unasaini nakala original mbili moja yako mwenyewe na nyingine ya upande wa pili,au kwenye mpira ni tofauti?
 
Hakuna kipengele kilichopo kwenye mkataba kilichovunjwa,CAS wataangalia mkataba unasemaje na unatekelezwaje
Inawezekana upo sawa ila Dogo ameshasema tangu anasaini mkataba alisaini kwa kumuamini Hersi, hata mkataba hakuchukua Kumbe Hersi walichozungumza sicho alichokiandika kwenye mkataba.

Hili ni tatizo ambalo kisheria atashindwa ila ni wazi kuwa kuna kiongozi anafanya maisha ya Fei hapo Yanga kuwa magumu. Kama ni sahihi, Katika mazingira haya mchezaji anaweza kuamua potelea mbali,IMETOSHA ngoja nijaribu nikishindwa nitakaa mtaani.
 
Umeacha mengi na umeandika machache, moja wapo ni hili.

"Nilipata kidogo kuliko nilichokiacha. Simba walinipa milioni 25, lakini moyo ulinisukuma kwenda Yanga ambapo nilipata milioni 10".

Hii ilikuwa ni mkataba wake wa mwanzo, ambao yeye Feisal hakuona kuna shida na mapenzi yake kwa Yanga ndio yaliyomsukuma kufuata klabu anayoipenda na si pesa...

Mkataba wa pili, maisha baada ya mkataba huo na uongozi mpya wa Hersi inaonesha ndio sababu haswa ya fukuto hili...
 
Dah! Inasikitisha sana kumbe ndio ilivyokua 🥲
Yaani kisheria Fei kashika makali ila ameona potelea mbali kuliko kurudi Yanga. Na amekiri, hana tatizo na Yanga, ana tatizo na kiongozi sababu licha ya kumtapeli aliendelea kumnyanyasa.
 
Hivi si unasaini nakala original mbili moja yako mwenyewe na nyingine ya upande wa pili,au kwenye mpira ni tofauti?
Huko juu wamesema amekiri hajui Kiingereza. Yeye wamezungumza na Injinia akajua anachosaini ni kile walichokubaliana kwa mdomo.

Kwahiyo hata akiwa na original haisaidii kitu kwa sababu original inambeba Injinia.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Bibi. Hadi kwenye mpira humo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uto siipendi Ila dogo Fei anapuyanga Sana. Hivi hata habari za huko nje za wachezaji wenzao hawafuatilii? Sadio Mane alikuwa hana furaha pale Liverpool kutokana na kulipwa kidogo Kuliko akina Milner lakini alikuwa anapiga kazi kama kawaida na akasubiri mkataba wake ukaisha akasepa.

Sio kwamba hakujua kama kaongezewa mwaka bali kwa wakati huo aliona inafaida kwake, hakuangalia wakati na alileta ushabiki badala ya kazi.
 
Kuna interview moja Feisal alifanya na Azam, akasema Simba walienda na dau dogo akakataa leo anasema Simba walitoa 25 Yanga akatoa 10, ni vile tuu hawa watangazaji wetu hua hawana taarifa za kutosha,
Ile interview ya leo Clouds walipaswa wawe na mtu wa michezo pia
 
Huyu dogo boga kabisa, kunakuwaje na connection kati ya Mama yako na Yanga? Ina maana huwezi jisimamia au
Mkuu hata Messi anasimamiwa na Baba yake anayeitwa Jorge ndio agent wake,hilo sio tatizo,kuna interview moja,Baba yake Messi alisema; "Messi mpaka leo ananisikiliza mimi,hafanyi movement yeyote bila mimi Baba yake"
 
Sitatoa coment ya maana mpaka mahojiano na ya Feisal na Clouds yatakapo isha ila mpaka hapo mahojiano yalipo fik...
Sawa kuna ujanjaa mwingwi sana kwenye Mambo ya Mikataba, lakini wengi wetu huzingatia sana kwenye swala la muda, hata Kodi ya jengo utazauri visheria vyote vidogo vidogo lakini utazingatia sana kwenye swala la muda wa ulipaji Kodi yako, ukisema hujui umechukua pesa ya muda wa miaka miwili alafu unafanyishwa kazi kwa miaka mitatu hilo haliingii akilini kabisa!!
 
Huko juu wamesema amekiri hajui Kiingereza. Yeye wamezungumza na Injinia akajua anachosaini ni kile walichokubaliana kwa mdomo...
Hayo ameyagundua lini?kwanini hakuanza na hili la muda wa mkataba kuongezwa kinyemela tofauti na walivyoongea maana kusoma hajui
 
Kwa hiyo Feitoto hajui kingereza kabisa kabisa KWA HIVYO TWO YEARS NA THREE YEARS HAWEZI AKATOFAUTISHA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…