Muongozaji mkongwe wa video hapa Tanzania, Adam Juma amedai kuwa watumiaji wengi wa mtandao wa Instagram wanamatatizo kiakili. Kwani wapo kwenye mtandao huo kwa lengo la kufuatilia umbea. Adam Juma ametoa kauli hiyo, baada ya jana kuposti picha ya Boss wa Clouds Media, Ruge Mutahaba kwenye mtandao huo akimpa pole ya kuugua. Baadhi ya Watumiaji wa mtandao huo, walimshambulia wakidai ameposti picha hiyo kinafiki. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Adam Juma ameandika "Kuna sababu kubwa huwa sipendelei kushinda instagram, asilimia 80 ya watu insta ni wehu ambao hawana kazi na kupenda udaku. Mara nyingi mimi hutumia instagram kusema jambo linalonisumbua au kunifurahisha, jana niliandika ujumbe kuhusu ruge. Naomba nitoe ufafanuzi kidogo sababu kuna ujinga unaendelea usio na manufaa yoyote maandiko yangu naomba yasitumike kumshambulia mtu yoyote au chombo chochote kile kwani itakua kunikosea heshima. Kumpa shukrani binadamu mwenzako sio dhambi, kum shukrani haimanishi kila kitu kisimame katika maisha hapana. Sio kila kitu katika maisha yetu ndio iwe bifu tena hizo ndio style za ki clouds clouds, yes labda nirudie ki CLOUDS CLOUDS. Wasanii wengi wanajua uhusiano wangu mimi n ruge sio mzuri kwa vitu vilivyotokea nyuma ambavyo hata wewe mtu uliyeko kwenye ista hujui chochcote ila hii haimanishi simheshimu Ruge. Naomba ieleweke yakua kuna mihili katika tasnia na panapokesekana muhimili 1 tu basi mapungufu ni makubwa mno mno. Kinachofanyika sasa hivi mimi binafsi nakiponge kwani kinawapa wasanii fursa na kipato. Msanii akienda kwenye FIESTA , WASAFIfestival au kingkiba tour atapata kula yake kitu ambacho ni bora katika tasnia, tusitengeneze makundi eti ki huyu kaperform huku basi tumtenge tutakua hatuna tafauti na siasa zile za clouds tunayoijua Mwanaume wa kweli katika vita ni yule ambaye anaweza kusimama na adui wake na kumuangal usoni huku akimpa pole kwa ngumi aliyomtandi kichwani na kumshukuru kwa kumpa fursa ya kupigana naye. Narudia tena naomba maneno yangu yasitumike kurusha vijembe kwenye kam zenu za ugomvi. Get well RUGE.