DOKEZO Fidia ya Kipunguni A mbona danadana nyingi, TAA tuambieni ukweli

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Screenshot_2024-01-09-16-43-00-1.png

Uharamia wa Malipo ya watu hawa ambao wamefanyiwa kwa zaidi ya miaka 20 , si wa kawaida , unaambiwa wameanza kufanyiwa Tathmini ya eneo lao miaka 28 iliyopita , kwa madai ya eneo hilo kutumika kwa upanuzi wa Uwanja wa Ndege .

July 2022 wakafanyiwa tena Tathmini nyingine na kwamba walipaswa kulipwa kabla ya octoba 2023 , lakini hadi leo kimya ! kumbukeni kwamba kwa kipindi chote hicho hawaruhusiwi kuendeleza maeneo yao , Maana yake hutakiwi kupaka rangi wala kujenga Choo kipya hata kama kilichopo kimefurika .
 
Mkuu ukitoka Kyela na kujenga kwa kuuziwa eneo na mzaramo mjanja matokeo yake ndiyo hayo.
Wengi wameingia huo mkenge, unauziwa sehemu kumbe mipangomiji walisha li zone hilo eneo kwa matumizi mengine.
Sina nyumba Kipunguni
 
Watalipwa fidia tu, bilioni 147 ndogo sana, uwanja wa ndege kwa mwaka utaingiza mapato mara kumi ya hizo.

Halafu kama inapita muda fulani, kwa mujibu wa sheria ya uthamini, uthamini wa awali unafutwa
 
Walipeni basi
 
Kuna wale waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki.

Nao wana madai miaka na miaka.
 
Sio hao tu ,kuna kijiji kinaitwa Nyatwali Bunda wao sasa ni mwaka wemefanyiwa Tathimini kulipwa ni hadithi Serekali inanyanyasa sana watu.
 
Uharamia wa Malipo ya watu hawa ambao wamefanyiwa kwa zaidi ya miaka 20 , si wa kawaida , unaambiwa wameanza kufanyiwa Tathmini ya eneo lao miaka 28 iliyopita , kwa madai ya eneo hilo kutumika kwa upanuzi wa Uwanja wa Ndege .

July 2022 wakafanyiwa tena Tathmini nyingine na kwamba walipaswa kulipwa kabla ya octoba 2023 , lakini hadi leo kimya ! kumbukeni kwamba kwa kipindi chote hicho hawaruhusiwi kuendeleza maeneo yao , Maana yake hutakiwi kupaka rangi wala kujenga Choo kipya hata kama kilichopo kimefurika .
Hata kama wanachelewa miaka 100 kulipwa siyo mbaya kama yule DIKTETA Mwendazake alivyowafanyoa wakazi wa Kimara- Kibaha ambapo aliputisha barabara ya njia 6 bila kuwafidia wakazi waliokuwapo.

Naamini hawa watu WATAFIDIWA kabla ya Juni 2024, na hicho ndicho kielelezo cha utawala bora chini ya Rais Samia
 
Headline inasema "unyama"..nikajua labda watu wanauwawa au kuvunjiwa nyumba na kutupwa nje..kumbe wamefanyiwa tathmini na malipo yamechelewa
Bila kuona damu hamuhisi kama ni unyama !
 
Hata kama wanachelewa miaka 100 kulipwa siyo mbaya kama yule DIKTETA Mwendazake alivyowafanyoa wakazi wa Kimara- Kibaha ambapo aliputisha barabara ya njia 6 bila kuwafidia wakazi waliokuwapo.

Naamini hawa watu WATAFIDIWA kabla ya Juni 2024, na hicho ndicho kielelezo cha utawala bora chini ya Rais Samia
Hizo porojo umetoa wapi ?
 
Back
Top Bottom