Mpira wa Australia na France nimechelewa sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza nitaiangalia baadaye kwa vile ilirekodiwa. Mpaka sasa wako half time na bado hawajafungana. Mtangazaji anasema wamepambana nguvu sawa pande zote mbili.
Kipindi cha pili kimeshaanza.
Bado mpira unachezewa katikati tu kama nilivyoukuta kipindi cha kwanza; hashambuliani sana. Nafikiri wanategeana.
Australia imeanza kuwaelemea wafaransa kidogo lakini bado kama 50-50 tu.
Mpira unaelekea kuwa mgumu kwa upande wa Ufaransa sasa. Naona Ufaransa wameanza kuelemewa; ila mchezo huu huwa hautabiriki; meza zinaweza kugeuzwa wakati wowote.
Wanawake hawa wamekabana makoo kweli kweli. Tumebakiza kama dakika nane tu kumaliza zile 90 na sioni wakishambuliana sana; bado mpira unachezewa katika kati ingawa kuna wakati Australiwa walikuwa wakishambulia lakini naona mwamerudishwa tena katikati.
Tuko kwenye dakika za majeruhi; bado dimba ni 0-0.
Official time imekwisha, sasa wanapewa mapumziko kidogo ili waongezewa dakika nyingine 30. Mbape wa kike wa Ufaransa leo alidhibitiwa sana na hao wanawake wa "Austwalia"
Kipindi cha kwanza cha dakika za ziada kimeanza. Naona mchezaji mmoja wa Australia kapewa yellow card.
Naona ufaransa walianza kwa kasi kidogo lakini gesi imeanza kupungua tena
Mpira huu ni mzuri sana kwa wanaoutazama na neutral eye. Ila mimi kapuku ninayetaka Australia ishinde ndiye ninapata pressure ya bure sana. Kwa juma timu zote ni ngomu na wanawake wote wanacheza kwa ufundi sana.
Tumeingia kwenye dakika za majeruhi ya kipindi cha kwanza cha nyongeza.
Kipindi cha kwanza kimekwisha
Kipindi cha pili cha dakika za nyongeza kimeanza; hakuna mabadiliko makubwa kwa timu zote mbili.
Ufaransa ilifanya shambulio kali sana golini mwa Australia lakini halikuwa na madhara.
Ufaransa imeoangeza sana mashambulizi upande wa Australia.
Naona mcehazo huu pia utaamuliwa kwa matuta. Mpaka sasa tuko kwenye dakika za majeruhi ya kipindi cha pili cha ziada, na mpira utakiwasha wakati wowote. Kipindi hiki France ilijitahidi kufanya masmabulizi sana lakini yote hayakuwa na madhara yoyote.
Muda official umekwisha sasa ni penalty kicks. Bado wanafanya modalities za nani atapiga penalty kwa pande zote husika. Imeamriwa kuwa Ufaransa ndiyo itakayokuwa ya kwanza kupiga penalty.
Ufaransa imekosa penalty yao ya kwanza.
Asutralia wanapata penalty yao ya kwanza.
Zamu ya Ufaransa sasa: Ufaransa wamepata penalty yao ya pili (Diani)
Zamu ya Australia: Australia wamekosa penalty yao ya pili
Zamu ya Ufaransa: Ufaransa wamepat penaly yao ya tatu (Wendy)
Zamu ya Australia: Australia nao wamepata penaly yao ya tatu
Zamu ya Ufaransa: Ufaransa wamepata penalty yao ya nne (Eugenie)
Zamu ya Australia: Australia pia wamepata penalty uyao ya nne
Zamu ya Ufaransa: Ufaransa wanakosa penalty yao ya tano
Zamu ya Australia: Australia nao wanakosa penalty yao ya tano.
Kipindi cha penalty tano official kimekwisha na timu bado zimelingana kwa 3-3. Sasa tunaingia kipindi cha the first lead.
Grace anaifungia Ufaransa bao la kuongoza
Katarina anaifungia Australia bao la kusawazisha
Sakina anaifungia ufaransa bao la kuongoza
Tameika anaifungia Australia bao la kusawazisha
Mayelle anaifungia Ufaransa bao la kuongoza
Elia anaifungia Australia bao la kusawazisha
Hapo hajapatikana mshindi.
Kenza wa Ufaransa anapoteza penalty
Australia wanasita katika kumchagua mtu wa kupiga penalty inayofuata
Clara wa Australia naye anakosa penalty yake
Inaelekea timu zote zimeanza kukosa wapigaji wa penalty. Wanajishauri sana nani akapige.
Vicki wa Ufaransa amekosa penalty
Cortney wa Australia amepata penalty yake na mchezo umekwisha kwa ushindi wa Australia dhidi ya Ufaransa 0-0(7-6)
Hongera zenu rafiki zangu wa Australia.
Ngoja tuwasubiri FOX watuletee video. Mchezo ulikuwa na msisimkuoa sana na pressure kubwa sana kwa wapenzi kama mimi. Kinachoonekana hapa ni kuwa timu vigogo wamwkuwa wang'olewa mmoja mmoja: Canada, USA, China, Japan, Netherlands na leo France. Sasa ngoja tusubiri England ambaye pamoja na sweden tu ndio vigogo waliobaki.