Figisu Hatimae kufukuzwa kazi

🙏🙏🙏
 
Pole.... Punguza tabia za kike mkuu, acha tabia za kukaa na wanawake kuwateta wanaume wenzio, kumbuka mwanamke hawezi kuchimba kaburi
 
Minaona unastahili kufukuzwa mkuu, maana mwenye ofisi yake alitumia muda mwingi na gharama kubwa kuifikisha kampuni yake hapo ilipo then wewe unakuja kuleta michongo ya hovyo ya kuihujumu kamuni.... hili ni kosa na wewe ni kama msaliti.
Lakini kwa upande mwingine uongozi wa kampuni umekufukuza kihuni maana ilitakiwa upewe notice kwamba nafasi yako inafutwa kwahivyo ulipaswa upewe mwezi mmoja (28days) za ufahamu na kisha baada ya hapo walipaswa wakulipe malipo stahiki kama mkataba wenu ulivyo elekeza.
Lakini pia sheria ya kazi ilimtaka mwenye kampuni yenu asilete mtu wa kuireplace nafasi yako nadhani walau ingekaa wazi kwa muda wa miezi sita. Kama hivyo ndivyo basi unaweza ukawapeleka kwenye mahakama ya kazi ili mkapate suluhisho ama mkishindwana kabisa mnaingia kwenye mgogoro.
 
sawa mkuu nimekueelewa
 
Sioni kosa kwa boss wako kumbuka tayari taarifa zilimfikia yeye kupitia watu wa chini yake inawezekana aliona akilifumbia macho kuna uwezekano wa yeye pia kumgharimu kwani labda lingefikishwa kwa ngazi ya juu yake.

Unapaswa kusonga mbele, chukulia hilo kama funzo, stay positive kama una mwamini Mungu basi ndio wakati wako wa kupimwa imani, ukiichukulia kama funzo na ukaweza stay positive trust me kupitia dhiki utazokumbana nazo kipindi hiki zitakujenga zaidi persistency, stamina na integrity vitakuwa na wewe.

Wakati mwingine wale wanaodhani wanatushusha ndio wanatupandisha bila kujua, hivyo muda ndo husema, narudia tena stay positive.
 
shukrani sana ntajitahid kuwa positive mdaa wote
 
Kuna msemo unasema Ampigae chura teke amemwongezea hatua. Usilaumu kwa kufukuzwa kazi hiyo ni one step ahead na wewe fungua kampuni yako tu Mkuu.
 
Wakati mwingine kwenye maisha una weza dhani unapoteza kumbe una gain

Huenda kuondoka kwako hapo kukawa ndiyo mwanzo wa kufanya makubwa Zaid ambayo usinge weza kufanya hapo

So be strong
 
Kwenye barua ya kufukuzwa kazi, sababu iliyoandikwa ya/za wewe kufukuzwa kazi ni ipi/zipi?
 
Ukiwa mwajiriwa tambua kuwa
1. Boss sio ndugu wala rafiki yako
2. Wafanyakazi wenzako ndyo washindani wako
3. Cheo ulichonacho ni cha mpito
4. Kazi uliyonayo inaweza kwisha wakati wowote hta kama una mkataba wa kudumu
5. Hakuna urafiki wa kweli kazini.

Yanatosha kwa leo karibu kitaa ulikokuwa unatupita bila kutusalimia ukiwahi kazini na kutuita sisi jobless
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…