Sioni kosa kwa boss wako kumbuka tayari taarifa zilimfikia yeye kupitia watu wa chini yake inawezekana aliona akilifumbia macho kuna uwezekano wa yeye pia kumgharimu kwani labda lingefikishwa kwa ngazi ya juu yake.
Unapaswa kusonga mbele, chukulia hilo kama funzo, stay positive kama una mwamini Mungu basi ndio wakati wako wa kupimwa imani, ukiichukulia kama funzo na ukaweza stay positive trust me kupitia dhiki utazokumbana nazo kipindi hiki zitakujenga zaidi persistency, stamina na integrity vitakuwa na wewe.
Wakati mwingine wale wanaodhani wanatushusha ndio wanatupanfisha bila kujua, hivyo muda ndo husema, narudia tena stay positive.