Finland tayari wamekatiwa gesi na umeme na Russia

Kwa i
 
Nyie msokoment kishabiki mtwambie walijiandaaje nawakat NISHATI tayar zishapanda bei kwenye hayo mataifa husika
Nisuala la muda tu kabla hawajaelekea MOSCOW kwenda kulialia!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Swala la kupanda nishati lipo Duniani kote,hapa Bongo mbona nishati imepanda mara dufu au na sisi ni kwa sababu 'tumekatiwa na Urusi'? Hakuna Taifa lolote Duniani linaloweza kusurvive kwa muda mrefu kwa vitisho vya Taifa jingine.

Finland na Sweden watakuwa na muarobaini wa hilo na hata Putin na Kremlin watakuwa wanashangaa iweje pamoja na vitisho vyote hivyo bado hawatishiki? Yeye Russia anaekata hiyo gesi ataigeuza kuwa chakula ili ale au na yeye anaitegemea hiyo gesi awauzie ili apate pesa za kuendeshea Nchi?

Aendelee kukata tena kwa muda mrefu tuone yeye atasurvive vipi na gesi yake. Russia anacheza mchezo wa kitoto tuliokuwa tunaufanya utotoni,unamuona mdogo wako kavunja kikombe kwa siri unaahidi kumfichia siri ili asipate bakora za Mama,lakini unatumia hiyo siri kumnyanyasa,kazi zako zote awe anakufanyia akijaribu kujitetea unamkumbusha ile siri uliyomtunzia ya kuvunja kikombe,siku akichoka anakugomea anaamua liwalo na liwe kaseme tu kwa Mama,unabaki umepigwa butwaa na kusema huwezi na ndiyo unakuwa mwisho wa kumnyanyasa.Narudia tena ukiona Kobe yupo juu ya mti .........[emoji846]
 
[emoji2957][emoji2957][emoji2957] mikwara mbuzi hii bado wanayo tu,tunaelekea mwezi wa nne sasa
 
Finland walishasema week iliyopita kwamba Russia wakate gesi na mafuta maana wanajitosheleza,gesi na mafuta wanayochukua toka Russia ni 10% tu
Na hii factor ya utegemezi wa hiyo 10% tu hawa Pro Russia wanajifanya hawaioni,hawathubutu kuiweka hapa wazi,wanatuletea propaganda zao za Kikomunist za kuondoa ukweli unabakiza yale unayotaka watu wayasikie na kujifurahisha moyo.
 
Hawa jamaa na wao wapuuzi sana,yaani wanamzingua mtu aliyeshika mpini? Sifa zitawaponza pamoja na kidanganywa na hizo nchi za magharibi.........
Ni sawa na Uganda waikatie umeme Tanzania. Sehemu ndogo tu za mpakani kagera huko. Finland wameendelea kuliko Russia wana Umeme wa kila aina. Gas watachukua Norway.
 
Hiyo aile mwenyewe tuone atafika wapi, mwisho wa siku hata kama watapata shida kwa muda watakuja kupata mbadala
Kwani European countries hawana mbadala wa gas ya Russia? Mbadala upo tatzo ni gharama kubwa hzo gas nyingine zinatoka mbali mpk zikifika kwenye nchi zao pamoja na cost za usafirishaji bei ina kuwa juu zaidi inasababisha mfumuko wa bei
 
Unabishana Na Hawa watu?? Matumizi mabaya ya akili
 
Ni kweli kabla ya uvamizi walikuwa hawapendi kujiunga NATO lakini baada ya kuona uwendawazimu wa Putin kule Ukraine wameona bora kujihami kabisa,Viongozi wao hawajakurupuka kuamua kupeleka maombi ya kujiunga,hizo siyo Serikali za mtu mmoja anajiamulia mambo,tutarudi hapa kucoment tena baada ya mchakato kukamilika.
 
Kwanini Ukraine na yeye alijiandaa kupigwa wewe ndo wale mnaoamini wazungu wote wanaakili Kuna wengine ni wajinga
 
Wewe mwenye akili sana hebu kwanza fanya ugunduzi wa machine ya toothpick tu ndiyo tutakuelewa hii comment yako.
 
NAWEKA MSISITIZO, MTAONGEA YOTE KWA MIHEMKO TU LAKINI MKAE MKIJUA GASI NA OIL NI BIDHAA ADIMU MNO NA HAZIWEZI KUKOSA WATEJA. WEWE UKISUSA WWNGINE WALA
Na kuandika kwa herufi kubwa mwanzo mwisho ni dalili kubwa ya mihemko na kupiga makelele
 
Russia ataendelea kufanya biashara na dunia, anaowakatia koki ni baadhi ya nchi za EU tu. Bidhaa ya oil na gesi haiwezi kukosa wateja
Kama kina nani unafikiri wanaweza replace soko la watu wa Ulaya la gesi na oil?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…