Fiston Mayele tumepigwa mchana kweupe

Fiston Mayele tumepigwa mchana kweupe

Umesahau msimu uliopita raundi ya kwanza hamkufungwa mkajinasibu nyie na Baca ndio hamjafungwa duniani [emoji3]jitulize ligi bado mbichi
Hatufurahii matokeo ya kushinda bali performance ya timu. Sisi tunafurahishwa na timu inavyozidi kuimarika kwa kucheza soka zuri wala hata hatuna haja na matokeo maana tupo kwenye utengenezaji wa timu. Vipi nyie mlioenda Morocco mwezi mzima na kambi ya Arusha, na nyie mnatengeneza timu?
 
Yule Djuma Shabani ni mtu na nusu sana, ana mwendo mno yaani anapandisha vizuri mashambulikama inavyotakiwa kwa full back wa kisasa!

Halafu kuna Yanick Bangala, jamaa ni kiraka mzuri! Anacheza kwa usawia akicheza kama beki wa kati na hana tofauti akicheza kama kiungo mkabaji. Ana sambaza sana pasi za upendo, ana utulivu wa hali ya juu sana! Huyu akiwa As Vita ndio alikuwa akimuweka benchi Mukoko kwenye nafasi ya kiungo mkabaji.

Mchezaji mwingine mwenye kitu cha ziada ni Heritier Ebenezer Makambo atafunga magoli ya kutosha hasa ukizingatia udhaifu wa mabeki wetu katika ligi ya bongo.

Waliobaki hao akina Fiston Mayele hamna kitu, yaani tumepigwa mchana kweupe, Ukibisha wewe bisha ila mwezi wa 11 mje hapa kufukua huu uzi, Mayele Tu-Me-Pi-Gwa
Je kwa sasa una la kusema tena kuhusu mayele?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom