Fixed Deposits Account, UTT-Amis ni njia nzuri za kutunza pesa LAKINI SIYO uwekezaji abadani

Una ubishi wa Kizamani sana kwenye dunia ambayo kila taarifa ni rahisi kuipata. Jaribu kufanya utafiti mkuu utachekwa na watoto wadogo.
Kwanini kila mtazamo unautazama kama wa kubishana, unahisi wewe peke tako umewekeza katika hizo taasisi, nina uzoefu na huo uwekezaji ndiyo maana nimeinua hoja, but anyway isiwe tabu ni kubadilusha elimu tu, unaogopa kuchekwa na watoto wewe utaweza kuwa mfanyabiasha sasa si utaogopa hata kuzikabili risk, labda ndiyo maana unafurahia easy money isio na risk
 
Approach yako nimeona kama umelenga ubishi unapotoa conclusion kwamba hicho kitu “hakipo”. Hili ni kosa kwa mtu anayetaka kujifunza. Mimi kila mwezi napata interest ndugu, ni vema ufanye utafiti kabla hujatoa hitimisho la hivyo.
NB. Nakuheshimu sana mkuu, naomba tusitofautiane sote daima tunajifunza.
 
Mkuu huo ni mfano tu wa jinsi matumizi ya fedha kwenye biashara yanavyolipa kuliko kuweka fixed deposit.

Pili, hizo route alizosema haimaniishi kuwa anatumia gari kama taxi bali anabeba abiria anapoenda na kurudi kazini tu.

Kama wewe utaona kuwa gari ni risk, kwamba inaweza kupiga mzinga wakati wowote, basi fanya kitu kingine lakini sio kuweka fixed deposit. Are we together?
 
Inawezekana kumbe kupokea kwa mwezi imenibidi niulizie moja wapo ya bank ulizotaja maana kila bank zina utaratibu wake wa kiuendeshaji,kumbe unaweza kupokea kila mwezi hata kama account yako ita mature baada ya miaka mitatu,
 
Wala mimi point yangu kuu sio Pesa as resource bali muda as a resource (Yaani kitu ambacho unasahau na kufumba macho) Mtaji sio Pesa pekee mkuu mbona mtu unaweza hata ukatengeneza matrilioni bila hata senti moja - Ila huenda hapo utahitaji skills fulani kwahio advantage ya kitu kama hiki sio ngapi unapata bali ni low risk as well as hands free
 
Kama ni hivyo sawa mkuu
 
Mkuu anachosema Jebel ni sahihi, kwa mfano TCB unapofungua ac ya fxd deposit unachagua kama upate interest monthly, quarterly semi annually au annually.
Lakini wadau mnachokosea ni kufananisha kati ya business na investment, hizo ni avenues mbili tofauti. Unapaswa kulinganisha business na business au investment na investment.
 
Hapo uko sawa sana mkuu! Nami hapa nilitaka kuonyesha tofauti hiyo hiyo, fixed ni investment na siyo business kabisa.
 
Hiyo sio fixed account ni FLEXI ACCOUNT.

#YNWA
 
Anafananisha fixed na flexi account.

#YNWA
 
Kuna watu wanafanya hiyo kitu??
Yaani anaweka zaidi ya 50M UTT au benki akitegemea awe anapata gawio na huo anauita uwekezaji akitegemea kukua zaidi au??

Mi nadhani ni wanahifadhi huku wakiwa na ishu zao nyingine wanafanya hiyo ni extra tu. Yaani huna mbishe ndo umepata 100M unaisokomeza yote huko.. alooo.
 
Binafsi ni mtu niliyen’gatwa na nyoka wa ujasiriamali, nilienda kufungia baishara za maduka kwa nondo za JF nikaishia kuchoma 18M within 6 months tu SITOSAHAU.

Sitaki tena upuuzi wa uwekezaji, baada ya kufikisha 12M through saving nimeipeleka zangu UTT Amis kwny mfuko wa liquid.. kila mwezi hela inaingia.

Nina mpango October nikaweke 10M nyingine katika mfuko Bond fixed hapo hapo UtT (2 years fixed acc).

Lakini pia napambana kwny bishara nyingine lakini sio hii miradi ya JF ambayo ukienda kwny utekelezaji unaambulia kuchoma mtaji.

NB: DUNIANI KOTE MATAJIRI WANALINDA MITANI YAO, HIVYO NI MUHIMU KUPATA FAIDA KIDOGO ILA USIPOTEZE MTAJI .
 
Ameidadavua tu upne ni kiasi gani kwa mwezi,sio kwamba wanalipa kwa mwezi.
 
MDF sio pvc,maoni yako nayaafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…