Uchaguzi 2020 Fomu namba 8A ndiyo itakayombana Tundu Antipas Lissu, ni ya Maadili ya Uchaguzi

Huko kwa Jaji kwenyewe ataenda?
 
Hivi kuna mtu mwenye jazba, hasira, kisirani na mropokaji hapa Tanzania kumzidi Meko?
 



Mabeyo nimeona naye katajwa, mweh jamaa wana mikwara hawa....
 
Eti munkari, jazba na mizuka! Kama fomu hii iliyobatizwa namba 8A ingetumika kwa wagombea wote wa Urais, leo hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hangekuwa huyu wa sasa. Kama hata Katiba yenyewe inayotoa ruhusa ya uwepo wa fomu kama hiyo ameshindwa kuilinda, kuiheshimu na kuitetea sembuse hii ya mjukuu wa Katiba!

Mada ya kipuuzi kama hii ingeweza kuletwa humu na mtu moja tu anayejiita johnthebaptist, hakuna mwingine.
 
Utanikumbuka bwashee!
 
Mnatunga kanuni kuwabana Wagombea au kuratibu uchaguzi huru na haki??
 
Akili finyu inafikiria kubanana tu.
 
wewe zuzu kweli kweli karne hii bado unataka watu waondoane kwenye uchaguzi kwa mapingamizi. mmezoea mizengwe kama ile ya serikali za mitaa 2019
 
Mkimuondoa Lissu wetu nchi itasimama.
 
kwa ujasiri na akili alizonazo nafkiri njia sahihi ya kushindana naye ni hiyo maaana alitakiwa awe marehemu ila Mungu kakataaa
 
ila mimi sioni tofauti ya Mh.JPM na Lissu kwa maaana ya Munkari, au jazba sema tofauti yao huyu mmoja ana machungu ya kutaka kuuwawa na pengine akiamini wahusika serikali imeshindwa kuwakamata.

Kwa hiyo kama ni kupigwa spana hata kama ni katikati ya kampeni wote yanaweza kuwapata. Ila kwa tume yote nazani itakuwa inaangalia goli upande mmoja tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…