For CHADEMA Followers: What comes around goes around

For CHADEMA Followers: What comes around goes around

Mashinji Hana ajira, kakimbia ili apate Cha kuteuliwa kutoka kwa teuwa tengua.

Mashinji ilikuwa lazima akimbie baada ya kupwaya kwenye nafasi yake for 5 yrs.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukosekana kwa uwanja sawa wa kisiasa ndio unaoua upinzani na siyo CHADEMA. Laiti kungalikuwa na uwanja sawa wa kisiasa, kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara kama inayofanywa na CCM nchi nzima, maandamano yangekuwepo kama nyakati za JK, Bunge lirushwe live,

hizi hama hama kamwe haziwezi kuubomoa upinzani. Katika mikutano ya wazi ya kisiasa ndipo vingeibuka vipaji vipya kila siku, wangetokea wakina Slaa wapya, wakina Zitto wapya, hamahama haiwezi kuua chama. Hata CCM walihama, lakini kinachofanya kionekane bado imara ni kwasababu kinafanya siasa kwa uhuru, na hayo ndio matokeo yake.
 
makatibu wakuu wawili wamekihama kwa muda sio zaidi ya miaka mitano, ni jambo la kufikirisha mno.

Kumbuka hawa ndio walikuwa watendaji wakuu. sasa wakihama jiulize nini kinaendelea humo ndani. Ni wazi kuwa kuna matatizo.
Makatibu ndio wapiga kura? Ni wananchi wangapi wamehamia CCM? Sijui huwa unatumia kifaa cha namna gani kufikiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wamepoteza aliyekuwa Katibu wa Chama ambaye aliletwa na mwenyekiti kuokoa jahazi basi ni wazi Chama hiki kamwe hakiwezi kuaminiwa na watanzania.

RiP Chadema.

VIVA WASSIRA kwa kutabiri haya.

Ni uwendawazimu kuamini kuwa Chadema itaweza kupata japo jimbo moja tu la Ubunge.

Wewe Mwenyewe ushakufa kitambo , endelea na ndoto za fisi kusubiri mkono wa binadamu uanguke..

Chama kilichokufa unapata wapi ujasiri wa kununua viongozi wake,
Kwa nini msije na mbinu bora ya ku recruit vijana wenye mawazo mapya, badala ya hawa Wabunge na Madiwani mnaowanunua, hamuoni huo ni udhaifu mkubwa ndani ya chama chenu na muda mfupi ujao itawagharimu sana hii kitu.
 
hata ka chembe ka ushahidi, tuweke hpa mkuu, siyo kukaririshwa muda woote na story ya kununuliwa, mkiambiwa mjitathimini kwenye chama chenu na kutafuta tiba ya hama hama mnakimbilia neno hilo hilo huku ushahidi hamna, nani aliyenunuliwa ukaona hela yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kama kweli hawajanunuliwa,Ila kamwe sitoamini eti mtu aache stahiki zake za ubunge/udiwani kwasababu ya kuunga mkono juhudi bureeee,Kama hawajanunuliwa basi wamelogwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naona kimsingi CCM ndio imekufa kabisa
Kama wamepoteza aliyekuwa Katibu wa Chama ambaye aliletwa na mwenyekiti kuokoa jahazi basi ni wazi Chama hiki kamwe hakiwezi kuaminiwa na watanzania.

RiP Chadema.

VIVA WASSIRA kwa kutabiri haya.

Ni uwendawazimu kuamini kuwa Chadema itaweza kupata japo jimbo moja tu la Ubunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upinzani haufi kamwe, kinachoweza kufa Ni taasisi zinazounganisha upinzani na viongozi wanaowaunganisha watu wenye mawazo tofaut na state. Upinzani upo hai, hai mioyon mwa watu, hata ikitungwa Sheria kua chadema kifutwe, Bado mioyo pinzani ipo, n muda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli hapa tulipofika Chadema ni kama mgonjwa mahututi anayerusharusha mikono na miguu na usipofikiri sawasawa utaamini anaweza kuvuta.

Ukiangalia kwa makini msingi ulioisimamisha Chadema utakubaliana kuwa hakitakufa kirahisi hata kama kitakosa mbunge au diwani hata mmoja uchaguzi huu wa 2020.

CCM kwa sasa inafanya vizuri katika siasa na hii inatokana na juhudi binafsi za Mwenyekiti wake Dr Magufuli.

Bila Dr Magufuli CCM bado ni ile ile na ushahidi ni mapokezi waliyoyapata wale wastaafu walioitwa kuhojiwa pale Lumumba.

Binafsi siwaamini sana hawa wahamiaji hasa wanaotoka kanda yetu pendwa ya kaskazi ila wakati ndio utaamua.

Maendeleo hayana vyama!
 
Pamoja na juhudi kubwa mnazozifanya za kuwanunua viongozi wake lkn bado huna aibu unajitoa akili na kuwa mtangazaji wa kifo cha CHADEMA?

In God we Trust
 
Tatizo la Chadema unaweza usijue katibu ni Nani na m, kiti ni nani?
Kila mtu kambale, kila mtu anatoa matamko
Ukihitilafiana kisiasa na m, kiti wapambe wake ndani ya chama watakupiga vijembe na matusi bila woga
Ni kama vile chama kimekuwa kama shule ya watoto watukutu,
Misingi ya siasa ni kuheshimiana na kusimamia KATIBA
Chama kisichofuhata katiba yake kinasambaratika kama makaratasi kwenye upepo
Unaweza usiamini kinachotokea Chadema si ccm wala polisi ccm
Chadema wanajimaliza wenyewe na sababu kubwa ni kuaminisha vijana kule ccm hakuna demokrasia, hakuna kushika madaraka kama si mtoto wa mkubwa
Ccm kuna mafisadi

Mwisho wa siku vijana wakatamani siasa hasa za Chadema
Wakajua huku Chadema kuna demokrasia, siasa bora na hakuna makundi
Mwisho wa siku vijana wakaja kugundua demokrasia ndani ya CDM hakuna,
Kuna ukabila, umimi na makundi walivyoingia kwa wingi 2005,2010, 2015 ndio hivyo hivyo wanavyo ondoka
Tatizo sasa nani anataka kufulia
Vijana wakitazama kwa jicho la mbali wanaona fulsa ipo ccm ya kupata umaarufu, vyeo, na kutengeneza maisha
Wanaikimbia CDM wanaona hakuna chama mbadala cha wao kupata umaarufu katika upinzani
Wanakwenda Ccm
Na Watakwenda makundi kwa makundi labda m, kiti mbowe ajiudhuru ili kuvunja makundi yake ya vijana maslahi
Wanaomlinda m, kiti
Chama kita kufa kama kilivyokufa NCCR mageuzi kwa kulewa SIFA
chama kikuu cha upinzani mwishowe(. Chaliiii kinabaki story...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom