For CHADEMA Followers: What comes around goes around

For CHADEMA Followers: What comes around goes around

Watabiri wa kifo cha CDM kutokea Lumumba mmeongezeka sana!Tabiri kama hizi zipo miaka nenda rudi!
Biashara ya kununua wapinzani inawatia upofu,mtaweza kutununua na wananchi?
 
Jo ungekuwa mnyama ningekulinganisha na kinyonga kwa jinsi unavyoweza kujibadili rangi... Tofauti na huyo ningeweza pia kukufananisha na popo [emoji23][emoji848][emoji144][emoji86]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaaaaa....... Msema kweli ni mpenzi wa Mungu bwashee!

Kwa sasa CCM inatembelea nyota ya Dr Magufuli...... Na huo ndio ukweli!
 
Ruzuku ale nani?
Kwa kweli Chadema imeshapitea kama NCCR mageuzi. Kosa kubwa alilofanya Mbowe ni kugombea tena Uenyekiti. Angekaa pembeni Leo hii angejizolea umaarufu mkubwa sana wa kukijenga chama mpaka kikawa chama kikuu cha Upinzani.

Mbowe ameua chama kwa akili na mikono yake mwenyewe. Kwa sasa kuna kaharufu ka kutambika tambika ndani ya Chadema na serikali ya CCM. Sasa watu wanaangalia wapi penye kondoo wa kutambika aliyenona. Wanaona bora CCM mana kuna ulaji wa nyama ya mabeberu ya tambiko.
Bora mtu ajiunge na Serikali apate posho kuliko kutambika ndani ya Chadema.

Amini ,amini ,amini nawaambia kiroho safi kabisa kuwa Wale wote wasio wa Ukanda na kabila la Mbowe watahama na kukimbilia kule kwenye serikali mana wataona ni bora tambiko la kule litawapa angalau hata Udiwani wa kuteuliwa. Karne ya 21 bado watu wanapeana madaraka kwa makabila ndani ya vyama.

Naona tunataka kutambika.

Kwa Heri Mwalimu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sioni mbunge hata mmoja wa Upinzani bungeni
.
FB_IMG_1582080397242.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama hakiwezi kufa kwa kununua madiwani wenye njaa.
 
CHADEMA haifi kwa maneno ya Lumumba,na kuhama kwa wabunge na madiwani wa CHADEMA wanaouza utu wao siyo kipimo cha kifo cha CHADEMA, hiyo ni mbinu ya CCM ya kujipatia watu wakwenda kuwapa uongozi kwenye chama chao na serekali yao,baada ya kugundua kuwa CCM wote ni choka mbaya hawana uwezo wa kupewa uongozi hata wa serekali ya mtaa.
 
Tatizo la Chadema unaweza usijue katibu ni Nani na m, kiti ni nani?
Kila mtu kambale, kila mtu anatoa matamko
Ukihitilafiana kisiasa na m, kiti wapambe wake ndani ya chama watakupiga vijembe na matusi bila woga
Ni kama vile chama kimekuwa kama shule ya watoto watukutu,
Misingi ya siasa ni kuheshimiana na kusimamia KATIBA
Chama kisichofuhata katiba yake kinasambaratika kama makaratasi kwenye upepo
Unaweza usiamini kinachotokea Chadema si ccm wala polisi ccm
Chadema wanajimaliza wenyewe na sababu kubwa ni kuaminisha vijana kule ccm hakuna demokrasia, hakuna kushika madaraka kama si mtoto wa mkubwa
Ccm kuna mafisadi

Mwisho wa siku vijana wakatamani siasa hasa za Chadema
Wakajua huku Chadema kuna demokrasia, siasa bora na hakuna makundi
Mwisho wa siku vijana wakaja kugundua demokrasia ndani ya CDM hakuna,
Kuna ukabila, umimi na makundi walivyoingia kwa wingi 2005,2010, 2015 ndio hivyo hivyo wanavyo ondoka
Tatizo sasa nani anataka kufulia
Vijana wakitazama kwa jicho la mbali wanaona fulsa ipo ccm ya kupata umaarufu, vyeo, na kutengeneza maisha
Wanaikimbia CDM wanaona hakuna chama mbadala cha wao kupata umaarufu katika upinzani
Wanakwenda Ccm
Na Watakwenda makundi kwa makundi labda m, kiti mbowe ajiudhuru ili kuvunja makundi yake ya vijana maslahi
Wanaomlinda m, kiti
Chama kita kufa kama kilivyokufa NCCR mageuzi kwa kulewa SIFA
chama kikuu cha upinzani mwishowe(. Chaliiii kinabaki story...


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa akili hizi ngoja Magufuli aendelee kujenga viwanja vya ndege kijijini kwake, majengo mazuri ya mahakama kwake, majengo mazuri ya TRA kwake, majengo mazuri ya benki kwake, hifadhi za wanyama kwake, viwanja bora vya mpira kwake, uteuzi wa viongozi wengi kutoka kanda ya ziwa,mpaka mnyooke ndo mtafikriwa kutupiwa mifupa kama mbwa koko.
 
Kama wamepoteza aliyekuwa Katibu wa Chama ambaye aliletwa na mwenyekiti kuokoa jahazi basi ni wazi Chama hiki kamwe hakiwezi kuaminiwa na watanzania.

RiP Chadema.

VIVA WASSIRA kwa kutabiri haya.

Ni uwendawazimu kuamini kuwa Chadema itaweza kupata japo jimbo moja tu la Ubunge.

Muaminishe hayo maneno mwenyekiti wenu halafu akubali kuwepo tume huru ya uchaguzi. Utajua ukweli halisi.
 
Kama kuna vifo hatutakiwi kuvishangilia basi ni vya Taasisi aina ya Chadema kwasababu ya Utetezi wa Maswala ya Kijamii na Kiuchumi
Kama wamepoteza aliyekuwa Katibu wa Chama ambaye aliletwa na mwenyekiti kuokoa jahazi basi ni wazi Chama hiki kamwe hakiwezi kuaminiwa na watanzania.

RiP Chadema.

VIVA WASSIRA kwa kutabiri haya.

Ni uwendawazimu kuamini kuwa Chadema itaweza kupata japo jimbo moja tu la Ubunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom