For CHADEMA Followers: What comes around goes around

For CHADEMA Followers: What comes around goes around

Naomba niwasabahi wanachama wa jf,hamjambo?

Naomba niende kwenye hoja yangu juu ya wafuasi na wanachama wa CHADEMA,Naomba niweke kumbukumbu sawa, hakuna mwaka ambao chadema aliwahi kuvuna wanachama wengi toka CCM kama mwaka wa Mafuliko 2015, ambapo watu mashuhuri toka CCM walijiunga na CHADEMA huku chadema akishangilia na kujitanua juu ya anguko la CCM.

Kwa kuwa vile unavyo mtenda mwenzako ndivyo nawe utakavyo tendwa(what comes around ,goes around) Leo hii chadema amesahau kuwa wakati CCM inasikitika kupoteza wanachama wake wakongwe mwaka 2015, yeye Chadema alikuwa anashangilia, mambo yamekuwa kinyume chake chadema ameanza kulialia na kulalamika eti CCM inanunua wapinzani,hii ni hoja mfu ambayo haina nashiko na inapaswa kupuuzwa, kama ndivyo hao chadema watuambie waliwanunua kiasi gani Lowassa na Sumayi maana inaonekana wana uzoefu mkubwa wa kununua na kuuza wafuasi wa vyama.

NB: Chadema wavumilie ,huu ni ubatizo wa moto,kwani ngoma bado mbichi sana hii,kufikia Oct 2020 tutaheshimiana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sumaye , Lowasa Mashinji wamerudi kwa shinikizo yaani msalaba ni mzito kuubeba,Sumayi na Lowasa wamejisalimisha kulinda maslai yao yaani stahiki za ustaafu na kulinda mali zilizopo zisipukutishwe yaani wafanye wawe masikini ili uwatawale,mashinji kajisalimisha msalabani kukwepa kifungo kwa kesi inayosogezwasogezwa ili ibakie miezi michache hukumu ya maagizo kuwafunga wapinzani wote kuanzia kina zito hadi uchaguzi upite,kule maalimu atawekewa bandio hadi atimize miaka 2 ya kujiunga chama kipya.Wengine waliohama wamefata asali yaani shibe uwasikii tena wakipiga kelele kama walivokuwa upinzani, wengine wana mikopo mikubwa benk watailipa vipi sasa ile fear of unknown yaani kutishwa hakuna mpinzani atakaerudi bungeni ile hofu imewapelekea kujisalimisha kupigwa chapa.Swali kama sio biashara mbona viti maalumu na Zanzibar awaungi juhudi?Uliona wapi timu ya mpira ikafa kwa kuondoka kwa baadhi ya wachezaji tena sio kiungo ni timu B yaani wakaa bench hali makocha na mashabiki wapo?
 
Mnaposema wananunuliwa huwa mnalalamika au ? Mtakoma you just wait,CCM's
ambition is to eradicate chadema's existence as a political party and turn it to a group of street vendors.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ili uwe ccm inatakiwa uwe either ni mnufaika au uwe mnyonge yaan a futureless person jiulize wamefata nn kwann wote uhamia cccm na si kwenda vyama vingine
 
Kama wamepoteza aliyekuwa Katibu wa Chama ambaye aliletwa na mwenyekiti kuokoa jahazi basi ni wazi Chama hiki kamwe hakiwezi kuaminiwa na watanzania.

RiP Chadema.

VIVA WASSIRA kwa kutabiri haya.

Ni uwendawazimu kuamini kuwa Chadema itaweza kupata japo jimbo moja tu la Ubunge.
Mngetuonyesha kaburi la upinzani kwanza au huu sio 2020 si mlisema utakuwa umeshafutika
 
Chama akifi kwa kuondokewa na Viongozi bali wanachama na makocha wake,hao wanaorudi ni wale waliosombwa na kisulisuli cha mafuriko hivo wanarudi home
 
Mnaposema wananunuliwa huwa mnalalamika au ? Mtakoma you just wait,CCM's
ambition is to eradicate chadema's existence as a political party and turn it to a group of street vendors.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wangu hili likitokea taifa litafaidika na nini?
Naona tutarudi kipindi kile cha 2000 - 2015 giza tupu na rushwa, hayo ndio maoni yangu.
Hata ndani ya CCM huko mtakuwa na vita kubwa na mvurugano.
 
Hii hoja ya kununuliwa inashangaza. Wanasiasa wakubwa wakubwa kabisa eti wananunuliwa kama maembe sokoni.

Yawezekana pia kukawa na matatizo ama ya kiutendaji na hata kiulaji huko wanakopakimbia. Na badala ya kukalia kusema kuwa wananunuliwa, si vibaya pia kujifanyia tathmini kama kuna sababu nyingine inayowafanya watu hawa wazima na akili zao kutimka. Kujifanyia uchunguzi wa kina wa afya mara kwa mara kwa kawaida ni jambo jema.
Hakuna tathmini yoyote,kama mpinzani anaweza kupigwa risasi 32 ili afe,na uchunguzi usifanyike,hata kumuombea ilikatazwa,mtu yuko mahututi wenzie na familia ikaona akimbizwe kenya lkn serikali ikasema apite muhimbili kwanza apate kibali,akanyimwa mshahara,akanyimwa matibabu,akavuliwa na ubunge na mengine mengi...hata mimi ningeogopa kuwa upinzani.
 
Hizi stahiki za lowasa na sumayi ziko kwa mujibu wa katiba au ziko kwa utashi wa chama cha siasa?
Sumaye , Lowasa Mashinji wamerudi kwa shinikizo yaani msalaba ni mzito kuubeba,Sumayi na Lowasa wamejisalimisha kulinda maslai yao yaani stahiki za ustaafu na kulinda mali zilizopo zisipukutishwe yaani wafanye wawe masikini ili uwatawale,mashinji kajisalimisha msalabani kukwepa kifungo kwa kesi inayosogezwasogezwa ili ibakie miezi michache hukumu ya maagizo kuwafunga wapinzani wote kuanzia kina zito hadi uchaguzi upite,kule maalimu atawekewa bandio hadi atimize miaka 2 ya kujiunga chama kipya.Wengine waliohama wamefata asali yaani shibe uwasikii tena wakipiga kelele kama walivokuwa upinzani, wengine wana mikopo mikubwa benk watailipa vipi sasa ile fear of unknown yaani kutishwa hakuna mpinzani atakaerudi bungeni ile hofu imewapelekea kujisalimisha kupigwa chapa.Swali kama sio biashara mbona viti maalumu na Zanzibar awaungi juhudi?Uliona wapi timu ya mpira ikafa kwa kuondoka kwa baadhi ya wachezaji tena sio kiungo ni timu B yaani wakaa bench hali makocha na mashabiki wapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naona unakimbia kivuli chako,nadhani huenda tunajadili na MTU asiye na uelewa mpana wa masuala ya kiutumishi vile yanaendeshwa
Hakuna tathmini yoyote,kama mpinzani anaweza kupigwa risasi 32 ili afe,na uchunguzi usifanyike,hata kumuombea ilikatazwa,mtu yuko mahututi wenzie na familia ikaona akimbizwe kenya lkn serikali ikasema apite muhimbili kwanza apate kibali,akanyimwa mshahara,akanyimwa matibabu,akavuliwa na ubunge na mengine mengi...hata mimi ningeogopa kuwa upinzani.
A

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema ukweli CHADEMA miaka kuanzia 2010 kilikuwa ni chama kilichoonyesha matumaini ya kuwa chama mbadala wa CCM kwa kuaminiwa na watanzania walio wengi.

Kilichokiponza chama hiki bila kumung'unya maneno ni huruka na asili ya kabila la mmoja wa waasisi wa chama hicho ambao agenda yao kubwa ni kupiga hela!

Kikajaa kabila hilo hilo na kujinyakulia vyeo na nafasi nyeti za kupiga hela za ruzuku!

Kwa vile ruzuku hugawanywa kulingana na wingi wa wabunge pamoja na ada, michango ya wanachama na wahisani ilipelekea wenye chama kuona wanapiga hela ndefu kuliko biashara za baa, maduka, kitimoto, mahoteri.

Hiyo hela ndefu tena ya bure ikawavuta wengine (hao hao) wa huko huko tena mawaziri wakuu wastaafu kukimbilia CHADEMA kula urojo wa hela ya bure na kuaminishwa wataingia Ikulu.

Sasa angalia matokeo yakawa ndivyo sivyo na kuanza kugombania madaraka na ulaji ambapo yule aliyeaminishwa kuwa Rais alipokosa Urais karudi CCM na yule aliyetaka kuwa mwenyeketi wa CHADEMA ili apige ruzuku alipoambiwa "Sumu ailambwi" kakimbilia tena CCM na mwenyekiti wa siku zote kagandia kwenye kiti cha Uenyekiti wa chama ili aendelee kula ruzuku na kuwatupia makombo wanaomshobokea huku wakiacha ofisi za CHADEMA nchi nzima wakifugia kuku na mbuzi na nyingine kunyang'anywa kwa kutolipa kodi ya pango.

Jamani upinzani Tanzania baado sana hasa hasa vyama vya hawa mabwashee ni kupiga hela na ukiwapa nchi wataiuza mchana kweupe!

Tuwaache wabobee kwenye biashara lakini kuwapa nchi hapana kwa kweli!!
 
Back
Top Bottom