For Political Survival, Halima Mdee na wenzake wahamie ACT Wazalendo

Kwani hapo kabla walikuwa wanachukua ruzuku?
 
Ila hawataweza kuaminika tena
 
Chadema haina shida na Ubunge wao, Cha msingi ni kwamba imewakataa na kwa Sasa chadema Ina mwakilishi mmoja bungeni pekee yake.
Ni kweli na nawasifu Sana Chadema kutomgusa AIDA KENANI Kwa kuheshimu maamuzi ya wananchi wa Nkasi waliopiga Kura zào na kuzilinda mbali ya mabomu ya machozi waliyopigwa siku nzima lakini hawakuondoka uwanja wa Sabasaba walikojikisanya kusubiri matokeo karibu na ofisi za Halmashauri ya Nkasi. Wananchi walioamua kuwapa Udiwani Madiwani zaidi ya 5 mbali ya dhuluma zilizofanyika kwenye Kata nyingine.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Jamani Zito alienda Mahakamani kutetea Ubunge wake enzi zile hata Magu hakuwa Rais bado, sijui kwanini binadamu tunasahau haraka, au mna shida gani na hayati Magufuli, muacheni mzee wa watu apumzike kwa amanii
Anazungumziwa Mwendazake kwa vile yeye ndio chanzo cha matokeo ya akina Halima Mdee, Bulaya na wenzao 17 wa CHADEMA, Mwendazake ametuharibia sana Bunge bora na siasa safi kwa maslahi yake binafsi na sio ya Taifa.
 
Halafu waliotajwa kuwa wahuni wataenda kutoa ushahidi mahakamani?
Mimi nitafurahi waende mahakamani ili ikadhihirike waliowasaidia kufoji nyaraka
 
Naunga mkono hoja wahamie ACT. Hawa ni wanawake smart sana na CHADEMA inaenda kufa mara moja.
 
Rufaa imeshasikilizwa na baraza kuu ndio chombo Cha mwisho. Halafu wale kwa Sasa hawana chama na pia kuhusu kuondoka bungeni hilo ni juu ya spika. Ila chadema kwa Sasa Ina mbunge mmoja tu kenan wa nkasi.
Kama chama kinamtambua kenan Basi wanehalalisha uchaguzi 2020 hivyo wapeleke majina hakuna namna.

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Watakuwa wapumbavu kujiunga na chama cha zitto , kwa kuwa hicho chama ni mfu zaidi ya mfu
 
Je na wao wakifunguliwa kesi ya kugushi?
 
Huu ndiyo ukweli. Na kwenye kikao walienda tu ili wawe vizuri kwenye rufaa yao. Nashangaa watu wanavyojenga matuamaini eti wametimuliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…