Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
Huyo alijitoa muhanga sana naye [emoji23]. Ila wewe, nina uhakika mkianza real trade hamto choma account ni vile tu unaogopa risk na unasubiri upewe confidence na Ontario. Mwisho wa siku you will have to overcome that fear. Kama vp anza hata na $50 sababu the only way to get going is to start, hizi demo zisitufariji sana
kaka mi nakukubali sana, unamisimamo ya kiume, ulicho ongea ni kweli, hata yeye maelezo yake alikomaa sana, kabadilisha broker 3, kaacha kutumie indicator baada ya kuona zinampoteza hayo yote maana yake alitumia real account baada ya kuona analoose ndo akajifunza, mimi naona kama mtu hayuko radhi kupoteza hata $200 hawezi kuijua hii biashara na kufanikiwa baadae, yeye kasema alichoma account
 
My story so far!

Nilikua offline kama siku mbili tatu nikiwa naugulia maumivu[emoji23]!

Awali ya yote, kwangu hili ni somo naimani kwako pia litakuboresha in a positive way (sio tu katika forex bali na maisha kwa ujumla)!

Juzi kama part ya mafunzo nikaamua kufungua real account!

Yaliyonikuta!

Kwanza nilifungua acc. Kwa xm brokers. Hawa jamaa wana customer care nzuri sana!! Baada ya kufungua account nikapewa bonus ya euro 25 hivi!! Nikaona nisiweke pesa kwanza ili nizitumie hizi euro 25 kama majaribio!

Kazi ikaanza! Nikaisogeza ndani ya masaa mawili au manne niliweza make kama euro 10 au 12 hivi!!

Nikawa na open positions kama nne au tano zina run, kwa kujisahau nika click sell...ikajiuza ikiwa na loss...hapa faida ilishuka!

Huku positions nyingine zikiendelea...nika close ya kwanza (maana ilikua kwenye profit position) nikashangaa zina close zenyewe bila mimi ku comand sell au buy! Mpaka sasa sijui nilikosea wapi duuuh!!

Mpaka hapo acc. Ikawa na minus!! Yaani loss! (hapa nilihisi kichwa kinauma)

Kwa kifupi account imeungua!

Hizi ndio sababu za kupata loss...

1. Kupoteza focus. Natrade huku nafanya mambo mengine!

2. Kuopen positions nyingi

3. Kuto tumia vyema top profit HASA stop loss!

4. Kuto focus hasa baada ya kupata first loss (ambayo ilikua ni kosa langu mwenyewe) !

5. Niliruhusu hisia/emotions zinitawale (hapa sijilaumu maana sisi ni binadamu, japo nitajihidi next time isiwe kama last time)!

Somo nililojifunza...

Kweli faida ipo tena uwezekano wa kupata ni mkubwa kuliko kupata hasara kama ukiweza kuji-control na kufocuss na kuwa na maarifa hasa ya kusoma na ku-analyse candle sticks na soko siku husika!

Unaweza poteza 1mil within a second pia unaweza pata 10mil within a second!

Theory na practical ni vitu viwili vyenye sura inayofanana lakini maana tofauti! You should be good on both though!

Nimeamua ku-retreat na kurudi mezani kujifunza zaidi kulingana na makosa yangu!! Japo imeniuma ila Nitarudi tena kutrade soon as I can!

Nilianguka sasa nimeamka. Ntajitahidi nisianguke tena!

Tuendelee kujifunza...

Tuko pamoja!
 
Ukiyeweka uzi huu,tell us where we can see you and join please let us know your contacts seriously
 
Daaah nazidi kupata morali aisee hebu ngoja nikomae na hiki kitabu kwanza

Ila nilichogundua hiki kitabu kimeweka wazi mambo ya msingi sana yani hakujifichi na katika yote kimetumi lugha nyepesi sana kutoa ufafanuzi

Ukisoma naked forex na hiki basi unapata knowledge ya kutosha unatamani hata uanze Ku trade live ila kwanza tumalize theory

Ushauri mwingine kwa wote ni vizuri kuzipunguza zile namba za pesa kwenye demo angalau hata kufikia $200 ili Uwe unacheza na uhalisia kidogo man katika hali halisi hakuna anaeweza Ku trade na $10000000

Cha mwisho kwa sisi ambao tuna haraka ya mafanikio naomba tumalizr kwanza hiki kitabu cha mwisho alafu demo ifanye kazi ya ziada and then nitaku free to goo
Hilo ni la muhimu sana huwezi kutrade account yenye hela ndefu haikupi uhalisia mm yangu nimeset $50 mpaka nimefikisha $70 na lot size ndogo[emoji5] [emoji5]
 
Hii biashara Si ya kukurupuka. Invest in books kwanza kabla ya kukimbilia kutrade.mimi najipa miezi 3 kwanza! Then miezi 3 kwenye demo. Kisha hapa nitaangalia Kama nifungue real account au VIP! Boss Ontario naomba kujua unatumia broker gani? South Africa? Lot size umeset ngap? Kinacho burn account Ni pipps kubwa au Lot size kubwa? Broker demo account ipi nzuri kwa bigginer? Kama broker ndio anayetoa rates bid/offer je Ana asilimia ngap ya wewe kupoteza biashara au kupata? Je Kama Si mwaminifu je Si rahisi kukutia hasara akicheza Na hizo figure? Je ulipotoa ela kwenye account ulituma moja Kwa moja au lazima zipitie sehemu ingine like pay pal, au Spt, to bank account. Ulisema ulivyotaka Toa mzigo mkubwa walikusumbua je kuanzia dola ngap hawasumbui kuanzia dola ngap wanasumbua?
Mkuu maswali mengi umeuliza yameshajibiwa,pitia Uzi wote,mfano brokers alisema ametumia XM,Etoro,Hot forex na now kawakubali zaidi JPmarkets.lot size hata Leo kasema alitumia0.01
 
KAKA we unamawazo kama mimi, ONTARIO kaleta ideal watu badala ya kujiongeza wanafikiria wote kupata darasa, real fighter kwa idea hii ameshafanikiwa nusu ya safari yake, mimi kama sitopata nafasi kwa kwenye hiyo training sitorud nyuma, nitacomaa mpaka nitatoka, msimamo wangu ndo huo. if they can do you can do.
Mkuu kuna darasa na mentor,je wewe una mentor tayari?
 
Duh hizi nondo zilizopo kwenye ASTROFX ni hatari yaani kinaeleweka vizuri kwani image zilizoko zinakufanya hata uweze kufanya practice barikiwa sana wadau hapa ni mwendo mdundo,yaani kuliko ucheze mchezo wa kubet wa mpira bora upate dollar mbili kwa siku hakika ina thamani sana
 
Duh hizi nondo zilizopo kwenye ASTROFX ni hatari yaani kinaeleweka vizuri kwani image zilizoko zinakufanya hata uweze kufanya practice barikiwa sana wadau hapa ni mwendo mdundo,yaani kuliko ucheze mchezo wa kubet wa mpira bora upate dollar mbili kwa siku hakika ina thamani sana
Hicho kitabu ni noma mkuu!!
 
Nimeona kitu kama hiko.
Ila ni vizuri kuona kitabu kinasemaje.
"Kiu ya Mafanikio haichagui cha kusoma"
kwney ile webinar moja niliatend juzi nikalike paje ya jamaa sasa naona signal provider wananiwinda kama swala kila mtu anaifuate private akitaka aniuzie signal nikiwaambia mimi ni newbie wananiambia watanicoach, Nimewakatalia nimewaambia nahitaji kujua kwanza ninachokifanya kabla ya kuuziwa signal ila WANAFORCE mpaka mwisho.

sina intention ya kuanza kununua signals

ILA HAPA ninaomba ushauri kuhusu hawa Signal provider, kuelewa YUPI NI MKWELI NA YUPI NI MUONGO?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom