Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
Ontario mi nafikiri usipoteze mda mwingi Wa kupambana Na wenye wivu ya maendeleo yako hizi Ni sababu za kukuonea wivu
1.umefakiwa ukiwa mdogo
2.umeweza kuleta jibu la vijana wengi swala la ajira (kujiajiri)
3.wengi wanataka waigeuze wapige dili Kama kawaida ya watanzania but una misimamo mizuri
4.Hawana kazi za kufanya! Badala ya kuleta ubunifu ututoe hapa tulipo tumekalia majungu
5. Africa ukiwa Na kipaji wanatafuta kukiuwa nchi za wenzetu ulaya , America hata uraia watakupa

*Mi nafikiri wewe kaa kimya acha kujibizana nao. Ukweli utaongea. Hata biblia imeandika zaburi 35-4

Waibishwe, wafedheheshwe wanaoitafutia nafsi yangu mabaya, warudishwe nyuma wafadhaishwe wanaonizulia mabaya.

Don't worry wote wanaoitafuta nafsi yako. Na wote wanaokukuzulia mabaya ndicho kitakachowatokea.
 
HAO KAMA WANAJIAMINI WATUPIE POST ZAO HUMU,WAONE MCHAKAMCHAKA WAKE,KWANGU MIMI WAMECHELEWA,HIVI HATA MTU ASIYE NA UELEWA MPANA ATASHANGAA- KILA MTANDAO UNAOFUNGUA IMEANDIKWA KUWA HII BIASHARA NDIO INAYOONGOZA DUNIANI NA WATU WANAPIGA PESA NDEFU,NAJIULIZA - HIVI HAO WAPINZANI WETU WANATAKA SISI TUFANYE NINI ? HATUSUBIRI PESA ZA MAKINIKIA WALA ZA ACCACIA ,TUNATAFUTA ZETU FOR ANY MEANS MRADI TUSIUE MTU,KAMA WANADHANI WATAWATISHA WATU WATASUBIRI SANA
 
Hayo ya kuchafuana yamepita - tupeane ushirikiano in case of anything!!

Weekend motivation

Hua sipendi kabisa kupost screen shots za trades, hasa kama trades si zangu... but hua nakua humbled sasa na incidents zinazomgusa maisha ya mtu directly.

Kuna huyu dogo, nimemzidi kama mwaka au miwili, niseme tulikua nae kitaa kimoja enzi bado niko mtoto. Bahati mbaya huyu bwana hakufanikiwa kuendelea na masomo yake baada ya kufail form 4. Sasa akawa anaunga unga kitaa, akapataga leseni ya kuendesha magari, mwishoe akaja akaajiriwa kuendesha yale magari ya kunyanyua mizigo kampuni 1 ya publishing. But still mambo hayakuchange - coz mshahara alikua anapewa buk 10, akikata nauli na maji anabaki na matatizo.

Sasa huyu dogo hua anajua home ninapoishi nikiwa Dar, akanicheki, akaomba nimsaidie. Mimi nikaona nimpe siri ya forex, lkn bado nilikua nina hofu sana kutokana na uelewa wake na level yake ya elimu, but nikasema nijitahidi nitakavyoweza.

Nikawa nampiga pindi kila siku masaa mawili kwa wiki 2 mfululizo, namuonesha ninavyotrade nk nk, nikamfungulia demo ya 1000 nikawa namtest skills zake.

Sasa J5 nikamwambia aweke pesa aliyonayo ajifunze kutrade, nilikua nahofia sana kwamba ataweza kuunguza account siku ya kwanza, but I just gave him confidence. Akatafuta pesa akapata km dola 150, nikamwambia aongeze zingine 150 ili iwe 300 ili aweze kutrade bila hofu na kupunguza probability ya kuunguza account (kadri account inavyokua ndogo ndio rahisi kwa mtu kuipiga kiberiti). Lkn dogo akasema hapo ndio mwisho wake.

Nikamwambia afanye afanyavyo lkn asitumie lot size kubwa zaidi ya 0.01. Jana ijumaa ndio ametrade kwa mara ya kwanza, na leo ndio akanitumia screen shot hii (nimeiedit ili kuficha baadhi ya info zake)

Hii imenipa motivation sana, hapa ni kama kagonga 5% ya balance yake... hii ni kama 14,000 kaipata kwa muda mfupi sana, hajatumia nguvu nyingi zaidi ya knowledge - ndio pesa ni ndogo, lkn ni wangapi wamenunua bajaji kwa mil 7 na kwa siku hawapati elfu 15??.

Mtu kama huyu mdg mdg ataanza kupiga 20,000 per day, atakuja 30,000 per day atafika kipindi anapiga mshahara wa Professional lawyer au auditor per day. Ni matter of time of learning more about the market na kua mvumilivu.

this boy is a pure definition of a hustler - hana masters, hajasoma international finance, hajui hata definition ya micro economy but he's hungry for knowledge. That's all he has!!

Cheers!! Happy weekend bosses!!
 
 
Doh aiseee safi sana kwake ,kiukwel ni hustler na mie nafuata huko mdogo mdogo nameza vitabu
Keep it up ontario,umetufungua macho wengi sana kwenye hii issue
 
Watu wasiopenda kujitumaa Siku zote ni watu wa majungu maneno na lugha chafu pole kwa yote mkuu Elimu haina umrii wala rika.Wengine chuoni na mashuleni wamefundishwa na watu wanao wazidi umri lakini hawakuwazarau hata kidogo acha azidi kukuchafua anavyo weza but hata kama angeenda kwenye magazetiii yotee ya Tanzania this issue is non stoppable by any reason inyeshe mvua au jua amechelewaaa sanaa watu tumeziacha nchi zetuuu tunaishi kwa watu ili swala liende sawaa mwambie alete sheet zoteee lakini Alisha chelewaaa sanaaaa sanaaaaa ila Ushaurii WANGU kwako Mkuu.ONTARIO please over please jitahidi kupokea na kupunguzaa jazibaaa palee unapokutana na watu kamaa hawaa Saivii your a coming young billionaire with a great name na kwenye heshima yake no matter upo katika age ya katiii au laaa maintain your status avoid them please kabisaaaa hao ndiyo kila Siku wanakujaa kutaka kutupangia sisi cha kufanya achana nae uyooo relax tupige kazii ila akushukuruu kwa hata hicho kidogo ulichomsaidia akifanyie kazi kimsaidie kwenye maishaa ya baadaae.Relax Kaka tuko pamojaa forever and always.


By Foreigner the one.Niushaurii wanguu tuuu.
 
nimejifunza kitu hapo!
 

Thats very good!! Tutafika tu mkuu!! Dogo amechukua hatua!

Shukrani kwa kutujuza!! Nimeamua na mimi niwashirikishe ndugu zangu!! Atleast nao waanze kusoma! Ngoja niweke mambo sawa!!
 
mda mwingine ukitafakali sana tabia zetu waafrika unakosa jibu eeh..ngoja niishie hapohapo..ontario mkuu MUNGU akutangulie kaza uzi ndugu kazi uliyonayo ni kubwa sana ya kutuokoa vijana wenzako wa kitanzania dhidi ya dhiki/umasikini uliotawala kuanzia kwenye mafamilia zetu hadi serikalini..kwapamoja tutafika hata kama tusipokimbia tunatembea na tukishidwa kutembea tutatambaaa tu LENGO NI KUONDOKANA NA DHIKI YA KIPATO. dhiki inadhalilisha dhiki inauwa dhiki inaumiza.....
 
Wakuu naomba mnisaidie image zilizoko katika kitabu cha astrofx page no 33. Natanguliza shukrani
 
Thats a real motivation.
 
Mkuu nipo na demo account ila bado sielewi jinsi ya kuset viwango vidogo...nipe maujanja ni kweli hayo madola mengi hayana uhalisia kabisa!!
 

Ontario! You've gone extra miles! Kwenye post yako ambayo sikumbuki Ni namba ngapi ulielezea jinsi ulivyo msikia jamaa akijiuza kupitia jina lako kwenye mgahawa wa KFC Kama sikosei. Ukasema ulikuwa unapata chochote ili uende kanisani, Na south pia ulienda kwenye kanisa la mchungaji bushiri Kama sikosei.
Nakuomba tumia busara hizo unazo pewa Na Mungu Mwenyezi kwa kutumia lugha laini kwa wanaokuchafua kwa kuwaambia 'Asante Mungu awabariki' mwenyewe atawatenda Na utakapo KUWA ume kamilisha dhamira yako, wabaya wako wote watapata aibu.

Muombe Mungu akusamehe kwa hasira hizo Na akupe ujasiri wa kupambana Na waovu. Barikiwa sana.
 
Unachokisema nakijua vzr sana, umasikini naujua inside out, nimeuishi almost 80% ya maisha yangu. Nauchukia sana umasikini, ndio maana sitaki hata watu walionizunguka waingia ktk mtego wa kua masikini. Poverty damn sucks deep down!!

Sijaanza leo kuwashirikisha watu kile kidogo nnachokifahamu... I do this for love - hakuna anaenilipa, niseme hakuna anayeweza kunilipa. Kwa hii forex ningeweza kukaa zangu ndani nimezungukwa na screen nashusha zangu pips, kwa siku kulala na $3000 inanitosha sana - tena hata Bongo ningehama niende SA.

Lkn siku zotenajiuliza sana, kuna furaha gani kuaccumulate pesa zoooooote afu siku ukifa unaziacha watu wanazigombania. Kuna haja gani ya kuwa na pesa kwa nia ya kutafuta sifa watu wakulambe miguu na kukuona mfalme. Kuna faida gani kuzungukwa na majirani wasio na uhakika wa milo miwili kwa siku huku wewe mbwa wako anakula balanced diet - ni kama UCHAWI aisee. Hivi kuna haja gani mtu uondoke duniani kama ukivyokuja, yani hata ukifa hakuna anayesikitika... it's cr*p

Unajua bana mtu kua na pesa si kwamba yeye ni genius sana, ama talented or anything, it's just by the love of God (no disrespect for atheist/agnostic). Kama hiyo Love umepewa bila kulipia kwanini nawewe usisambaze just ROBO ya huo upendo?? Hapa nilikua nina miaka 21 (National museum theatre)
Hapa nilikua nina miaka 22 (ESRF).
 

Inauma Lkn mkitumia busara Za kutomkimbiza kichaa aliye kwapua nguo zako ukiwa unaoga mtoni itakuwa vyema zaidi. Kwani ukimkimbiza ukiwa mtupu, watu watahisi nani kichaa? Cool down,
 
mkuu hongera , nimefanikiwa kuangalia video zako za interview youtube , no wonder you did what you did , wewe ni mtu wa kipekee sana, God bless you brother
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…