utapeli upo popote hata hapo unapofanya kazi/unapoishi wewe ulipoanza kimyakimya huko ulitapeliwa? kama wewe umeweza na sisi tutaweza kwa msaada wa Ontario ndiye mwenye nia ya dhati kwa vijana wa tanzania nyie mliamua kunyamaza endeleeni kukaa kimyaaaa!
I second you Mkuu....kusema ukweli hii kitu mm nilikuwa siijui Kabisa mm nilikuwa najua mambo ya kuuza na kununu pesa kwenye maduka ya kubadilisha hela tu..ingawaje sijaanza kujisomea vtabu vilivoelekezwa kutokana na kubanwa na muda ila hii kitu naona ni legit bizz Kabisa.
Hakuna Biashara isiyokuwa na changamoto duniani...kinachonisikitisha ni watu wanakuja na mbwembwe kibao za kutoa tahadhari na wengine kudiscourage watu kwa kweli nashindwa kuelewa Kabisa. Mleta Uzi tayari alishatoa maangalizo kibao Kuhusu hii Biashara kwa hyo huku kutishiana Sijui hii Biashara ni ngumu...Sijui unaweza poteza hela hayo hayatutishi..Biashara yoyote unaweza kupoteza hela sio hii tu.
Kama walikuwa wanajua hii ishu wakaamua kukaa kimya eti ili wapige hela kimya kimya halafu leo Mkuu @ Ontario kaamua kuishirikisha familia ya Jf Kuhusu hii Biashara halafu watu wanakuja na bla bla zao eti Sijui mm ni mzoefu wa hii biashara...kama ni mzoefu kwa nn hukutushirikisha???unakuja kudandia nyuzi za watu hapa na taadhari zako kibao.
Kama unaijua hii Biashara hatujakaa kutoa maoni...muongozo au Ushauri ila yasiwe maoni/Ushauri wa kukatisha watu jamaa..narudia.hakuna Biashara isiyo na lose duniani na kama ni kupoteza hela ktk Biashara mm nilishapoteza sana ila sikukata tamaa niliendelea kukomaa na kujifunza kutokana na makosa niliyofanya.
Hii Biashara lazima nitafanya...nitasoma nitasoma nitasoma mpaka niielewe na kama ni kutafuta mtu wa kunitrain nitamtafuta. Jamani eh hii sio Biashara ya nyanya kuwa watu wengi wakijihusisha nayo basi nyanya zitajaa sokoni na kukosa bei hapana..hii ni Biashara ambayo jinsi watu wengi wanavyoijua ndo inavyozidi kuwa tamu.
Kwa wale mliokuwa mnaijua hii.kitu na mmekuja kwenye juu Uzi ili kuturlimisha tunawashukuru sana ila kwa wale waliokuwa wanaijua na wanakuja kwa kutuvunja moyo mshindwe kwa jina la Yesu. Kwa sasa sisi tupo na Kijana @ Ontario amejifunza hii kitu kwa gharama Kubwa sana ila.ameamua kukitoa kwa watanzania bure Kabisa kwa kuanza na hata kama kutakuwa na kuchangia ili.kupata mafunzo hapo baadae sio kitu cha ajabu....ukitaka kula kubali kuliwa (JK).
Tunamuombea Ontario kwa Mungu ili kila alichokipanga Kuhusu hili jambo kifanikiwe na tunawaombea wale watakaopata zile nafasi za bure za kijifunza wakishamaliza warudishe ujuzi watakaoupata kwa watanzania wengine.
Kwa wale mliokuwa mnaijua hii Biashara mkaamua kukaa kimya endeleeni kukaa kimya na sio kuja hapa kututisha na mambo ya Sijui kupoteza na bla bla kibao...kama ni kupoteza tulishapoteza sana na hatukukata tamaa bado tunaendelea kupambana mpaka kieleweke hata kama kitaeleweka jioni.
Kwa walenaokuja kwa minajili kutuelimisha..tunawashukutu.sana.sana sana na mwenyenzi Mungu awabariki kwa kweli Mkuu @ Bavaria nitakutafuta Mkuu naona mchanga wako.kwenye Uzi huu ni adimu Kabisa.
Kwa kumalizia naomba kusema I salute you Mdogo wangu @ Ontario ....mwenyenzi Mungu akubariki kwa kila Jema unalotenda.