Fred Lowassa: Baba hakuwahi kumsaliti rafiki yake

Fred Lowassa: Baba hakuwahi kumsaliti rafiki yake

Fred Lowassa akihojiwa na Millard baada msiba wa Lowassa ameongea mambo kadhaa kuhusu baba yake. Moja ya swali aliloulizwa ni kipi hawezi kusahau kutoka kwa baba yake.

Fred amesema kitu kikubwa alichokuwa nacho mzee wake ni 'Loyalty' akiita kama 'kufa na mtu wako' kwani katika historia yake ya uongozi yote hajawahi kumsaliti rafiki hata mmoja na ndio kilichomjengea heshima mzee Lowassa na amewafia rafiki zake wote kwenye siasa.

======

Swali(Mwandishi Paschal): Kipi ambacho hutasahau kutoka kwa Baba?

Fred Lowassa: Niseme Loyalty, yaani ni mtu ambaye mimi amenifundisha kiswahili wanaita 'kufa na mtu wako'. Yaani akisema Paschal ni rafiki yangu hata aje nani kumwambia nini, anasema hapana, mimi Paschal namuamini ni rafiki yangu na angekaa nae mpaka mwisho na ndio jambo limemjengea heshma na upendo kwa watu wengi sana kwasababu yeye hakuwahi kumsaliti rafiki yake hata mmoja katika historia yake ya uongozi yote, ni mtu ambae amewafia rafiki wote mwanzo mpaka mwisho.

Hilo ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo kwakweli kwa wanasiasa ni wachache sana wenye kipawa hicho. Amewafia watu wake wote vizuri sana, nadhani hilo jambo mimi nimejifunza, namshukuru Mungu sana.
Kuna maswali ya msingi ya kujiuliza,
Je report ya uchunguzi wa Richmond, ilikuwa real?
Maamuzi ya bunge baada ya kupokea report ikionesha kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi; je, bunge lilikosea kufanya maamuzi kwa niaba ya Watanzania?
Spika Samwel Sitta anabaki mmoja wa viongozi mahiri na waungwana, walitaka yeye kama kiongozi wa bunge apuuze ukikwaji wa sheria na taratibu ili "kulindana".

JK anaweza kuwa rafiki na swahiba wa mtu yeyote, JK alipokuwa Rais na Mkiti, kwa background yake kama Lt. Col; alichofanya ni kuonesha uongozi pasi kupepesa macho.

By the way, sifa ambazo mhusika alitindikiwa 1995 kama alivyotindikiwa mzee John Malecela (aliekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais), je, 2015 zingeweza kutoka wapi?

Maana sidhani kama ni JKN aliewaondoa hao wawili 1995; bali ni upungufu wa sifa wa kukamatia nafasi ya U-CEO wa nchi.

In leadership, people make decision base on facts for the national interest and not to please a friend or a group of individuals. JK, atalaumiwa, ila alionesha uongozi ambao JKN alionesha 1995 kuondoa majina ya wengi wakiwa John na mwenzio, likewise 2005 BWM aliondoa jina la John Malecela mara ya pili bila ajizi.
2015 kuna Samwel Sitta (spika), Dr Billal (VP), Mizengo Pinda (PM), Sumaye (PM); wote hawa waliondolewa round ya kwanza hiyo 2015 sawia na EL; haitakiwi mtu mmoja aonekana alisatahili sana; by the way, Urais sio nafasi ya urithi kwa msingi watu wawili walikubaliana.
 
Hiv
Fred Lowassa akihojiwa na Millard baada msiba wa Lowassa ameongea mambo kadhaa kuhusu baba yake. Moja ya swali aliloulizwa ni kipi hawezi kusahau kutoka kwa baba yake.

Fred amesema kitu kikubwa alichokuwa nacho mzee wake ni 'Loyalty' akiita kama 'kufa na mtu wako' kwani katika historia yake ya uongozi yote hajawahi kumsaliti rafiki hata mmoja na ndio kilichomjengea heshima mzee Lowassa na amewafia rafiki zake wote kwenye siasa.

======

Swali(Mwandishi Paschal): Kipi ambacho hutasahau kutoka kwa Baba?

Fred Lowassa: Niseme Loyalty, yaani ni mtu ambaye mimi amenifundisha kiswahili wanaita 'kufa na mtu wako'. Yaani akisema Paschal ni rafiki yangu hata aje nani kumwambia nini, anasema hapana, mimi Paschal namuamini ni rafiki yangu na angekaa nae mpaka mwisho na ndio jambo limemjengea heshma na upendo kwa watu wengi sana kwasababu yeye hakuwahi kumsaliti rafiki yake hata mmoja katika historia yake ya uongozi yote, ni mtu ambae amewafia rafiki wote mwanzo mpaka mwisho.

Hilo ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo kwakweli kwa wanasiasa ni wachache sana wenye kipawa hicho. Amewafia watu wake wote vizuri sana, nadhani hilo jambo mimi nimejifunza, namshukuru Mungu sana.
Hivi umri wa Fred Lowasa ni miaka mingapi? Mbona kama amezeeka haraka? Na nimeona Alihitomu O level na kwenda Chuo UK sijaona A level alisoma wapi? Na umri wake hajaweka hadharani, Kwenye speech yake siku ya mazishi kama niliona anakula Tambuu hivi, wanaemfahamu yuko vizuri kuwakilisha jimbo lake kichwani kweli? Au Chadema waingie na miguu yote jimboni lile?
 
Strange. Siku zote naelewa kuwa wanasiasa hawana kitu kama urafiki wa kufiana. Wao wanachokuwa tayari kufia ni maslahi tu.

Kuna hata tuhuma kwamba Fidel Castro alimsaliti “rafiki” yake Che Guevara. Kwamba alikuwa akimuona Che kuwa “idealistic” sana na fikra zake za kuwasha vita za ukombozi dhidi ya mabeberu dunia nzima. Wakati Castro anataka kutawala Cuba yake kwa utulivu hata kwa kuelewana kiasi na US.

Nashangaa sana kuwa Lowasa pamoja na akili kubwa aliyokuwa nayo ya kutengeneza mitandao ya uhakika ya kisiasa na kifisadi aliishia kukabidhi nafsi yake kwa JK? Eti rafiki yake wa “kufa na kuzikana”? He couldn’t see through the man? Huo ni ushuhuda wa kipekee. Wafaransa wanasema mtu wa aina hiyo bila shaka alikuwa NAIVE kweli kweli.

RIP Statesman.
 
Inashangaza sana kusema kweli.

Moja ya sababu ya Che Guevara kuondoka Cuba ilikuwa kupishana baadhi ya misimamo na Fidel, kwani jamaa (Che...) alikuwa ' too extremist' kwa anachokiamini na kuondoka kwake Cuba ulikuwa uamuzi mzuri sana wakati huo.

Kwa Lowassa namna alivyotoswa na wale aliosimama nao bega kwa bega kuwapa mamlaka ni hadithi ya kipekee ila kwa hapa Tz hili sio jipya.

Hata Mwl Nyerere aliwatosa baadhi ya waliokuwa washirika wake muhimu kwenye harakati za Uhuru baada ya kutwaa madaraka, ukiwa na rafiki asiye na mali wale cheo ila akija kuvipata utaona tabia yake halisi bila kujali ulimsaidia au la.

Rutto alikuwa mjanja sema na angezubaa kidogo tu, Uhuru Kenyatta angemwacha njia panda.
 
Hili jibu la Fred limekuja kupigilia msumari wa mwisho kwa nini jina la JK halikutajwa kwenye mazishi ya Lowassa.

Kumbe JK anaonekana msaliti kwenye familia ya Lowassa. Palikuwepo na muda mrefu wa kurekebisha haya mambo, sijajua kwanini yakaachwa mpaka yafike hapa.

Funzo nimelipata hapa, kumbe duniani kuna wakati mnaweza kuishi kama marafiki, lakini mwishowe mkaja kuzikana maadui.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ni kweli kabisa,muda ulikuepo mwingi tu karibia miaka 10 kuyamaliza. Pride,pride,pride.
 
Back
Top Bottom