Fred Lowassa akihojiwa na Millard baada msiba wa Lowassa ameongea mambo kadhaa kuhusu baba yake. Moja ya swali aliloulizwa ni kipi hawezi kusahau kutoka kwa baba yake.
Fred amesema kitu kikubwa alichokuwa nacho mzee wake ni 'Loyalty' akiita kama 'kufa na mtu wako' kwani katika historia yake ya uongozi yote hajawahi kumsaliti rafiki hata mmoja na ndio kilichomjengea heshima mzee Lowassa na amewafia rafiki zake wote kwenye siasa.
======
Swali(Mwandishi Paschal): Kipi ambacho hutasahau kutoka kwa Baba?
Fred Lowassa: Niseme Loyalty, yaani ni mtu ambaye mimi amenifundisha kiswahili wanaita 'kufa na mtu wako'. Yaani akisema Paschal ni rafiki yangu hata aje nani kumwambia nini, anasema hapana, mimi Paschal namuamini ni rafiki yangu na angekaa nae mpaka mwisho na ndio jambo limemjengea heshma na upendo kwa watu wengi sana kwasababu yeye hakuwahi kumsaliti rafiki yake hata mmoja katika historia yake ya uongozi yote, ni mtu ambae amewafia rafiki wote mwanzo mpaka mwisho.
Hilo ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo kwakweli kwa wanasiasa ni wachache sana wenye kipawa hicho. Amewafia watu wake wote vizuri sana, nadhani hilo jambo mimi nimejifunza, namshukuru Mungu sana.
Kuna maswali ya msingi ya kujiuliza,
Je report ya uchunguzi wa Richmond, ilikuwa real?
Maamuzi ya bunge baada ya kupokea report ikionesha kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi; je, bunge lilikosea kufanya maamuzi kwa niaba ya Watanzania?
Spika Samwel Sitta anabaki mmoja wa viongozi mahiri na waungwana, walitaka yeye kama kiongozi wa bunge apuuze ukikwaji wa sheria na taratibu ili "kulindana".
JK anaweza kuwa rafiki na swahiba wa mtu yeyote, JK alipokuwa Rais na Mkiti, kwa background yake kama Lt. Col; alichofanya ni kuonesha uongozi pasi kupepesa macho.
By the way, sifa ambazo mhusika alitindikiwa 1995 kama alivyotindikiwa mzee John Malecela (aliekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais), je, 2015 zingeweza kutoka wapi?
Maana sidhani kama ni JKN aliewaondoa hao wawili 1995; bali ni upungufu wa sifa wa kukamatia nafasi ya U-CEO wa nchi.
In leadership, people make decision base on facts for the national interest and not to please a friend or a group of individuals. JK, atalaumiwa, ila alionesha uongozi ambao JKN alionesha 1995 kuondoa majina ya wengi wakiwa John na mwenzio, likewise 2005 BWM aliondoa jina la John Malecela mara ya pili bila ajizi.
2015 kuna Samwel Sitta (spika), Dr Billal (VP), Mizengo Pinda (PM), Sumaye (PM); wote hawa waliondolewa round ya kwanza hiyo 2015 sawia na EL; haitakiwi mtu mmoja aonekana alisatahili sana; by the way, Urais sio nafasi ya urithi kwa msingi watu wawili walikubaliana.