GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Ushauri wangu pekee kama GENTAMYCINE Kwake ni kwamba awe makini sana na Usalama wa Maisha yake ili yale yaliyomkuta Marehemu Deo Filikunjombe yasije Kumkuta na Yeye. Tafadhali auzingatie sana huu Ushauri wangu kwani Maono yangu 99% hutimia.Mfanyabishara Wa Nguo na Kijana Wa Kikinga Fredy Ngajiro Maarufu Kama Vunjabei ameteuliwa Kuwa M/kiti Wa Kamati Ya Fedha Ya Uvccm... Vijana Tafuteni Njuruku Hakuna Namna
----
Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu kama Fred Vunjabei jana tarehe 23 May 2021 amepitishwa na Baraza kuu la UVCCM kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha kupitia kikao cha Baraza Kuu ambacho kimemalizika jana Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Kamati ya utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Kheri James ilikuja na pendekezo la jina la mwenyekiti huyo wa kamati ambapo baadae alithibitishwa na wajumbe kwa kura nyingi za ndio huku katibu wake akifahamika kwa jina la Rose Manumba, Baraza lilichagua wajumbe wengine wanne wa kamati kutoka bara na visiwani.
Ameanza Kutengeneza Maadui kuliko vile ambavyo Yeye anajua na hakuna sehsmu ambako kuna Wanafiki na Mafia wengi kama huko aliko UVCCM na Mafia Wakubwa wawili ni miongoni mwa waliompitisha. Kapewa Cheo kwa Kumtega ili aharibu na wamchafue vizuri au hata wamuondoe mazima.