Fred Vunja Bei ateuliwa kuwa Mwenyekiti kamati ya Uchumi na fedha UVCCM Taifa

Fred Vunja Bei ateuliwa kuwa Mwenyekiti kamati ya Uchumi na fedha UVCCM Taifa

Nice and smart. Mipango ya kuingia bungeni 2025. Km hamuamini tusubiri 2025
Anaiwinda nafasi Kati Ile ya Jah people ama zinginezo huko makete na njombe au ilembuka! Wenye majimbo yao wajiandae na figisu na nguvu ya njuluku!
Nimpe angalizo la kuchunga kibubu chake asije kulia! Amtafute Rosti tamu amuulize yaliyomsibu akiwa mwekahazina wa ccm ampe mbinu za kulinda kibubu chake kabla wajanja wa uvccm hawajazimisha mikono yao humo na kukikomba chote!
 
Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu kama Fred Vunjabei amepitishwa na Baraza Kuu la UVCCM kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha kupitia kikao cha Baraza Kuu ambacho kimemalizika jana Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Kamati ya utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Kheri James ilikuja na pendekezo la jina la mwenyekiti huyo wa kamati ambapo baadae alithibitishwa na wajumbe kwa kura nyingi za ndio, Katibu wake ni Rose Manumba na pia Baraza lilichagua Wajumbe wengine wanne wa kamati kutoka Bara na Visiwani.

Katibu Mpya wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa ni Victoria Charles Mwanziva ambaye jina lake limeridhiwa na Baraza Kuu Taifa kuelekea Mabadiliko ya Secretariat ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa.
FB_IMG_1621873045632.jpg
FB_IMG_1621873045632.jpg
FB_IMG_1621873045632.jpg
 
Hapo Ndio Uvccm mnakwama, ya I Vunjabei ni UVccm mtu ana miaka 40 kasoro?
Halafu hao ..............tunawajua lazima wawe ccm. Wakiwa upinzani kesho tu biashara zinakufa
 
Umasikini wa watanzania umasababishwa na CCM, utajiri pia.

Masikini wanatafuta pakutokea,
Matajiri wanatafuta pa kujificha wakiendelea kuvuna utajiri kupitia CCM.

Hakuna tajiri aliye nje ya CCM ambaye hakupata misukosuko hasa enzi za mwendazake.
 
Mfanyabishara Wa Nguo na Kijana Wa Kikinga Fredy Ngajiro Maarufu Kama Vunjabei ameteuliwa Kuwa M/kiti Wa Kamati Ya Fedha Ya Uvccm... Vijana Tafuteni Njuruku Hakuna Namna

----
Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu kama Fred Vunjabei jana tarehe 23 May 2021 amepitishwa na Baraza kuu la UVCCM kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha kupitia kikao cha Baraza Kuu ambacho kimemalizika jana Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Kamati ya utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Kheri James ilikuja na pendekezo la jina la mwenyekiti huyo wa kamati ambapo baadae alithibitishwa na wajumbe kwa kura nyingi za ndio huku katibu wake akifahamika kwa jina la Rose Manumba, Baraza lilichagua wajumbe wengine wanne wa kamati kutoka bara na visiwani.
Huyu jamaa,alikuja kwenye game la biashara ya nguo baada ya Husein pamba kali,na lobby one fashion,lakini ameweza kukuza biashara yake ya nguo zaidi ya hawa miamba wawili,hii kitu imenifundisha jambo,unaweza kuwa unafanya biashara fulani akaja mtu mwingine anafanya kama hiyo ila kwa kuongeza technic fulani akakupita kama umesimama.
 
Kwa Kweli Umaarufu Huja kwa Njia tofauti...Huyu Kijana angeiga Mfano wa Bakhresa ambae pamoja na ubilionea wake anajificha sana.
 
Na yeye atawapiga vilevile tena atawapiga vizuri sana maana si ana biashara ya nguo so yale madela, kofia, leso, tshirt, chupi, sidiria, tight, pedi za ccm za wakati wa uchaguzi na nyakati nyingine tayari zishapata mdhabuni/supplier
Sema CCM biashara zao nyingi ni mikopo kulipa matanga, muulize Shigongo hajawahi kulipwa hela zake tisheti na khanga....walichofanya walimlipa ubunge kwa kumpooza.

CCM ni taasisi moja dhulumati Sana.
 
Back
Top Bottom