Freeman Mbowe anatutukana watanzania kuwa sisi ni wajinga?

Mbowe amesema watanzania ni wajinga. Sawa ni uhuru wake . Angeweza kusema yeye ni mjinga. Sawa pia ingekua ni uhuru wake .
Wewe Mlamba asali umesema Watanzania sio wajinga. Sawa ni uhuru wako.
Ungeweza ukasema wewe sio mjinga.Sawa pia ni uhuru wako.
Tuheshimu katiba. Kila mtu ana uhuru wa kujieleza.


Hata hivyo ni wazi kabisa kuwa Wapigaji wapo Kazini Kwa Sasa.
Wanatengengenza mtandao wao Kwa Kasi kubwa sana.

Magufuli alikua na mapungufu yake lakini hakuwa anamchekea kima pale anapomuona anasogelea Shamba.

Kukusanya Tozo nyingi hatukatai lakini kuwaacha wezi wazitumie wanavyotaka wakati Wana mishahara ni udhaifu mkubwa sana. Nchi inajengwa na wenye moyo lakini inaliwa na wenye meno.

Kwa Sasa mabosi na masekretari wao wanashindana kusafiri. Hivi anayefanya kazi ni bosi au ni yule mtu wa chini na ana Msimamizi Sasa safari za kiguu na njia za mabosi Zina tija Gani zaidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma.?

Kwa Nini mama alikubali kudanganywa. Yani unaongeza tozo,unaongeza mishahara halafu unaongeza matumizi na safari wakati ndio TU nchi na Dunia Iko kwenye tatizo kubwa la kiuchumi.


Kwa Nini Mama asingeongeza tozo akazuia safari, akazuia kupanda Kwa posho za safari ,akazuia mishahara kuongezeka Kwa mishahara ,akazuia pesa za wizi unaofanywa na Tasaf ,akazuia ununuaji wa magari ya kifahari Kwa mabosi wachache wakati watumishi wa chini ambao ndio watendaji hawana hata baskeli za serikali. Wajumbe wa nyumba kumi na wenyeviti wa Serikali za mitaa hawana hata mshahara wa shilingi 50,000/ Kwa Mwezi lakini Kuna watu wanatumia magari ya mil. 500/- na mafuta ya Mili 3 Kwa Mwezi.

Mbowe hajawatukana Watanzania .

Hapo aliyewatukana watanzania ni yule anayewaibia na kuwaambia walipie starehe zake .

Mbowe anazidi kupata umaaru mana hajakurupuka na ameonyesha shida ilipo.
 

Kaka mkubwa ameongea. Hii ndio raha ya kuwa na wakubwa Kwenye jf. Asipoukubali ushauri wako atapotea kabisa.
 
Ni kweli kàbisa huyu ni Mndali
 
Wewe ni mjinga sana....
 
Enzi zile za Chama kimoja Vijana wa CCM walikua wanawapongeza Makada na Mawaziri waliokua wanapiga dhulma na ubadhirifu wa Mali za umma.


Siku hizi Vijana wanasifia wezi na kuwapongeza Kwa sababu ya kulambishwa asali.

Vijana mnaangamiza Taifa lenu wenyewe.

Hawa walioko madarakani wengi ni zao la Wahalifu .

Msiingie kwenye mtego wa kuwasifu.Ni zao la uovu uliofanywa Kwa muda mrefu.
Miaka ya nyuma palikua na wizi mkubwa sana wa mitihani.
Watoto wa wakubwa na matajiri walikua wanapata paper wiki mojakabla ya mitihani. Walikua hawasomi mana uhakika wa kupata mitihani ulikuwepo.

Walipofika vyuo vikuu wengi walikua wanatumia madesa na wale wa Ke walikua wanapata digrii Kwa miili yao. Hali kadhalika ajira zilikua ni ama kuhonga au kujuana.
Kura zilikua na mpaka Sasa zinapatikana Kwa Rushwa na kupindua matokeo.

Hao ndio wengi wao wapo kwenye position. Wanapeana Connection kwenye mabaa na magest.Yaani watu kila siku wanakutana kwenye starehe Kwa kutumia pesa za urefu wa kamba zao halafu unamwona Mbowe kuwa ana chuki binafsi. Mbowe ni mfanya biashara na tajiri Kwa kuzaliwa hajatajirika Kwa kuiibia nchi, anawajua wanaopiga na wanaojificha nyuma ya siasa huku wakiwa mabilionea walioiibia nchi na kutengeneza mitandao ya kusifu na kuabudu.

Ndugai alisema tubanane humu humu tuijenge nchi . Mbona Mlimfukuza? Ndugai Alimaanisha kwamba tubane matumizi ya pesa za Tozo na nyinginezo.

Kuna makampuni Mengi sana hayalipi Kodi ipasavyo na wanaojificha nyuma ya walioko madarakani.

Kama kampuni Moja ya TBL inakusanya zaidi ya Bil. 400.
Basi tunahitaji kampuni 100 TU kupata zaidi ya Trail. 40.
Ni wazi kampuni nyingi hazilipi Kodi. Pesa nyingi kwenye makampuni ya mafuta na utalii zinaishia mikononi mwa wasio hata na kamba.

Badala ya kumshambulia Mbowe tuelekeze nguvu zetu kuwasimamia watawala wanaotumia vibaya fedha zetu na kushindwa kubana matumizi huku wakitoa kauli za kejeli.

Kama Mwenyezi Mungu alimtumia Mwalimu Nyerere kuleta uhuru na uhuru ikapatikana Kwa wepesi basi Mwalimu alipewa nafasi Ile ili kuweka misingi ya Taifa hili na hiyo ndiyo aliyoitaka Mwenyezi Mungu iwe hivyo . Ni Hakika kama walamba asali wasipoacha kuitafuna nchi bado atakuja kutokea mtu mwenye roho Ile Ile ya Mwalimu na Ile ya JPM na wanaoiba Sasa watapata aibu kubwa.
 
Uelewa wako umekupeleka gizani
 
Kwani lini mmekuwa na akili tena kuwa wajinga Bado katumia lugha laini mno nyie ni wapumbavu tu.

Wazee wa kupiga kelele mitandaoni bila kuchukua hatua.

Hii ni nchi ya mbumbumbu me naweza waita hivyo.

Huo ndio ukweli mchungu
Hili aliliona mkapa kitambo sana
 
Tunajenga nchi wenyewe wakati tunakopa kwa staili ya mwendo kasi? Tupunguze matumizi ya uendesjaji Serikali na wananchi waongeze uzalishaji
 
Huu tunamuita ni ufisadi wa mawazo Kwa Mtanzania mvivu hata kufikiria Kwa kuwa anao mwanya wa kulamba asali au wa kulambishwa asali hata anajigeuza kipofu Ili hata asione🤔
 
Yes anafanya vitu vingi, kwenye kasoro lazima akosolewe kwa Sasa jambo lililopo kipaumbele kwenye midomo na akili za watanzania wengi ni Tozo ila sijawahi ona Uzi wako hata mmoja ukizungumzia hili zaidi ya kusifia utendaji wa rais.
Kwani tozo imeanza leo? Tulianza kuwekewa kwenye mafua ya disel, petrol na kerosene na magufuli tukakaa kimya leo wamenogewa na tozo tunatokwa povu, tuache unafiki watz
 
Ndugu zangu yaani Mbowe anatutukana watanzania kisa tu tumeamua kuijenga nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe? Kwamba Mh. Mbowe haoni namna moyo na uamuzi huo wa kuamua kujenga nchi yetu ulivyo saidia kusogeza huduma muhimu kwa mwananch
Nyie ni wapumbavu NDIO, alikua kimya mmeanza kumchokoza Kila siku Mbowe kalamba Asali Yuko kimya
 
Jionee mwenyewe hii ID ya nani.
 
Unataka Nani akujengee nchi yako, unataka huduma Bora ziboreshwe na Nani kwa chanzo kipi Cha mapato, unazani hao ulaya waliyapokea maendeleo Kama zawadi toka uwanja wa ndege
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…