Freeman Mbowe anatutukana watanzania kuwa sisi ni wajinga?

Utakuwa UNASHAMBWA wewe..!!
 
Nimeupenda mchango wako, umeendika kiweledi zaidi
 
Nikukosoe kwa mengi:

1. Lugha: anazani => anadhani. Kumbuka umerudia hivyo mara nyingi mno! Dalili za kujawa kiwewe.

2. Hoja za Mbowe ulizozifumbia macho: Yako wapi yale magari yenu pendwa yenye kutugharimu wajinga sisi mamilioni 400/- plus (kwa moja) aliyoyaongelea Mbowe ili mtanue nyie, ewe mlamba asali au kibaraka wao?

3. Ujenzi wa shule, matundu ya vyoo: wewe hukumsikia rais akishukuru pesa za Covid-19? Ghafla zimegeuka kuwa manufaa ya tozo ili kutuhadaa wajinga sisi?

4. Mikopo na misaada: wewe hukumsikia rais akielezea umuhimu wa hiyo? Kumbe hata hukumwelewa kulikoni kumtimua Ayubu? Mawazo yenu wajinga sisi hatuoni wala kusikia?

Kwa hakika wewe unafuzu kuwamo kwenye hili kundi lenu pendwa:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

5. Ungependa sana tuendelee kuwakalia kimya ili muendelee kulamba asali kwa raha zenu?

Kwa taarifa yako tunaomuunga mkono mh. Mbowe tuko wengi kuliko ninyi wote walamba asali, vibaraka na chawa kwa pamoja.

Mwisho wenu uko karibu. Tukutane Tahrir:

Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir.
 
Lucas mwashambwa mambo vipi? Nimeona nikufuate huku private. Eee bwana jitahidi kumtetea mama usiache. Kama ambavyo tuliambiwa kwenye ile meeting ya mwisho kuwa piga ua tutetee tu ili hawa wapinzani wasipate pa kusemea.hili la tozo linaumiza watanzania ila tusiache. Hapa sasa tutumie IDs zetu zote. Pia usisahau kutupia hii link kwenye group ili wadau wengi waje kutetea. Na uwakumbushe admin kuwa ni wewe wawe wanahesabu maana huwezi jua zikitoka teuzi...
 
Mchonganishi huyu CCM jr.
Post zake za kiwaki kinoma. Anataka kusema Mbowe kaongea kitu hatunacho.
Mjomba Rudi Mbeya
 
Nimeupenda mchango wako, umeendika kiweledi zaidi
Kama kazi ya upinzaaniii ni kukosoa kila kitu na kwa kila Jambo lazima ijulikane na ifahamike kuwa Ni Haki yangu nami pia kueleza Yale aliyo yafanya mh Rais wetu, Haki haiwezi ikawa kwa mkosoaji pekee halafu kwangu ikawa Ni ushambuliaji, Anayo haki hiyo mh Mbowe ya kukosoa, lakini nami pia ninayo haki ya kumtetea mh Rais kwa kuwa aliyoyafanya na kuyatekeleza ninayaona na yanaonekana , Hivyo siwezi kujipa ukipofu wa kuamua kukaa kimya tu

Lakini pia lazima ujuwe upinzani wa Tanzania Ni tofauti Sana na wanchi zilizoendelea maana upinzani wa wenzetu Ni kuwa wanakosoa mahali panapohitajika kuboreshwa na wanasifia na kupongeza mahali palipofanyika kazi nzuri

Wenzetu walioendelea wanaweza wakapongeza Sera lakini wakakosoa utekelezaji wake, na wakashauri njia iliyo Bora, wenzetu Taifa mbele vyama baadaye wakati huku kwetu ni kupingaa tu kila kitu ilimradi tu kinatekelezwa na Serikali

Upinzani wa Tanzania hauna dira Wala Sera Wala ajenda yoyote Ile wanayosimana, wao wanaendeshwa na vimatuikio tukio tu ,Wao Ni kupinga kila kitu tu na ukisema umsikilize kila mtu utajikuta unakosa muelekeo Kama wao,

Mkuu Tanzania hatuna upinzani wenye kuleta ushawishii kwa wananchi ndio maana unaona wamepuuzwa kwa Sasa na Wala hawatiliwi maanani Kama enzi hizo za Dr slaa ulipokuwa upinzani wa hoja nzito nzito, ajenda kwa Sasa zimebebwa na kufanyiwa kazi na mh Rais,

Hivi mkuu mwandishi nguli unaweza ukasema kwa Sasa Kuna mbadala wa CCm hapa Tanzania? Hapana haupo ndugu yangu, angalia tu hata safu yao ya uongozi ndio utajuwa na kupata picha, angalia tu hata muundo wa baraza kimvuli walilokuwa nalo awamu iliyopita ambayo ndio Taswira yake ya klimu waliyokuwa wanaitegemea,, Sasa nikuulize je unaona ndio baraza lingetuvusha lile Kama nchi?

Wao kushambulia na kutukana kwao Ni kawaida, kwani wewe ni Mara ngapi wamekushambulia na kukutukana kwa kutumia Uhuru wako tu kueleza mtizamo wako? Wamekuvunjia heshima mara ngapi? Hata vitoto vidogo vimekutusi, je ndio misingi ya demokrasia hiyo ya kutukanana? Je hatufundishani kuvumiliana na kukosoana kwa heshima na staha hata kwa tunaotofautiana nao? Je unaona upinzani wakilifanya Hilo? Mara ngapi wamewadhalilisha watu bila sababu, wangapi manguli wa mijadara wameamua kukaa kimya humu kwa kuogopa kuogeshwa matusi na watoto wadogo kiumri?
 
Acha unafiki wewe, ulikaa na Nani au umekosa hoja
 
Samahani mkuu naomba uangalie namba 134 nimekujibu kule
 
Nimekujibu naomba uangalie post #134
 
Sisi tunachangia kupitia vipato vyetu ili tijijengea nchi yetu na hatutaki tuweke nchi yetu rehani kwa madeni, Hukusikia habari za mchina kuchukua baadhi ya miradi katika baadhi ya nchi hapa Afrika Kama sehemu ya kufidia madeni anayodai? Sisi hatutaki tufike huko Wala kusogelea huko maana Ni hatari kwa usalama wetu Kama nchi
 
Kama we ndio mjinga kabisa Mbowe alitakiwa akutumie kama mfano kwa huu utumbo ulioandika hapa.
 
Kuna post namba 134 nimekujibu wewe Ila nilidhamiria kumjibu mayala na Ni jibu kwa mwandishi wetu huyu wa habari, naomba uelewe hivyo usije ukaona Kama sijaeleweka ukilinganisha na ulichokuwa umeandika
Mleta uzi ni msomi wa hali ya juu,unachambua hoja,na wananchi tumekuelewa,Mungu akubariki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…