Wanajamvi, dunia hii huwa ina binadamu wachache wenye sifa za kipekee. Leo naomba nimuongelee Freeman Mbowe. Huyu jamaa anatokea kwenye Familia yenye pesa, inasemekana ni mali za urithi. Wanamiliki Hotel, lakini pia ukumbi wa Bilcanas, tukumbuke enzi hizo Bilcanas ilikuwa inaingiza pesa nyingi kwa mwezi, sijui kwa sasa. Lakini pamoja kwamba huyu jamaa tayari ana maisha bora, alihamua kujitoa Muhanga kwa ajili ya kuwapigania wanyonge angalau nao wapate kidogo.
Mheshimiwa huyu pamoja na pesa zake lakini amekumbana na Mabomu, Risasi, matusi, kuwekwa Rumande, vitisho, kukatishwa tamaa lakini hayo yote hakuyajali, yeye ameendelea kupaza sauti kwa ajili ya wanyonge. Mbowe ni special na ni unique. Mimi baada ya Nyerere huyu ndie Role Model namba mbili.
Ni matajiri wangapi wenye moyo kama wa Mbowe?, au wanaamvi mnasemaje?