Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Baada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM.Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.

View attachment 1862953
Uhuni mtupu. Ipo siku watalipia uonevu huu.
 
Uhuru ni kuwachekea wale majamaa walio tangaza kua wana nyembe ya kumnyolea bim kubwa.
This is logical non sequitur on top of a lazy generalization on top of some sadist Darwinian predator prey dynamics propably perpetuated by some innate systemic Malthusian malfeasance fueled by a societal cognitive dissonance.
 
Kudai katiba mpya ni chokochoko? hizo katiba mpya Huko nyuma zilidaiwa kwa chokochoko?inaelekea wewe ni mnufaika wa uonevu wa mama kwa wapinzani ndiyo maana umejitoa fahamu sasa huoni kuwa manyanyaso uonevu kwa chadema ni udikiteta
Magufuli alikuwa dikteta anawaonea Chadema na sasa Mama samia nae dikteta anawaonea Chadema, atakuja rais mwengine pia atakuwa dikteta atawaonea Chadema.

Tanzania bila rais kuwaonea Chadema basi Chadema haiwezi kufanya siasa Tanzania, watu tulijua tu kwamba lazima tu utafika muda wa Rais Samia kuanza kukosana au kuwaonea Chadema hilo halikwepeki.

Inawezekana mie nafaidika na huu uonevu kwa chadema ila wapo ambao bila huu uonevu wanaona mambo hayajakaa sawa kabisa yani washazoea haya manyanyaso bila wao kujua.
 
Dr ZWAZWA kwa ufinyu wa akili yako huwezi kuelewa hii kitu imekuzidi kimo sana. Endelea kutumia akili ya kushikiwa.
Mhuuuuu! umeshindwa kujibu hoja badala yake unamshambulia mtoa hoja personally. Na Mnyika jana alishindwa kujibu hoja za waandishi wa habari na badala yake akapandisha hasira na kuanza kubwabwaja ovyo. Mbowe naye juzi hivyo hivyo akaanza kuvishambulia vyombo vya habari. Sasa hiyo hoja ya katiba mpya mtaiweza kweli? Hoja ya katiba mpya inajibiwa kwa mrorongo wa makongamano na maandamano ni akili timamu kweli? Unakaribishwa kuja tena kunitukana kwani ndicho akili zenu inachokijua na mlichosomeshwa na huyo mnayemuita Mwamba.
 
Wewe kweli mpuuzi hata kinachoendelea nchini hukijui. Mara ngapi yule Mpango alikuwa akilalamwanalalamikaika kuhusu mchango wa nchi za wafadhili na mashirika ya umma kupunguza misaada na mikopo yao hivyo kuathiri bajeti? Unaishi dunia ipi wewe? Kuandika ujinga ujinga kila leo kumbe hujui hata yanayojiri nchini!!!
Budget yetu tegemezi na inategemea mikopo na misaada toka nchi wahisani. Wabunge walikuwa.Hakujua kwa nini Mwendazake aliwarubuni covid 19 apate fedha za EU hajui?
 
Huna hoja wewe! Unaandika ujinga ujinga tu.



Mhuuuuu! umeshindwa kujibu hoja badala yake unamshambulia mtoa hoja personally. Na Mnyika jana alishindwa kujibu hoja za waandishi wa habari na badala yake akapandisha hasira na kuanza kubwabwaja ovyo. Mbowe naye juzi hivyo hivyo akaanza kuvishambulia vyombo vya habari. Sasa hiyo hoja ya katiba mpya mtaiweza kweli? Hoja ya katiba mpya inajibiwa kwa mrorongo wa makongamano na maandamano ni akili timamu kweli? Unakaribishwa kuja tena kunitukana kwani ndicho akili zenu inachokijua na mlichosomeshwa na huyo mnayemuita Mwamba.
 
Baada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM.Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.

View attachment 1862953

====

UPDATES;

=====

TAARIFA KWA UMMA

JESHI LA POLISI LAMTUHUMU MWENYEKITI WA CHAMA
MHE.FREEMAN MBOWE NA "MAKOSA YA UGAIDI"

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe alifikishwa Dar es
Salaam jana majira ya saa tatu usiku chini ya ulinzi wa Polisi , walimpeleka nyumbani kwake Mikocheni Kwa ajili ya kumfanyia upekuzi ambao ulichukua takribani saa mbili na nusu.

Baada ya upekuzi huo Polisi waliondoka na Kompyuta mpakato (Laptop) na Vishikwambi (tablets) za watoto wake ,Kompyuta mpakato moja ya kwake na modem ya Internet Kwa ajili ya uchunguzi wao.

Leo majira ya saa Saba mchana Polisi walimfikisha Mhe. Freeman Mbowe Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kuchukua maelezo yake.

Polisi walitaka maelezo kutoka Kwa Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na kosa waliloliita 'KULA NJAMA ZA KUTENDA KOSA LA UGAIDI'

Baada ya maelezo hayo ya Polisi Mhe. Freeman Mbowe alitumia haki yake ya kisheria na aliamua kutokutoa maelezo yoyote Polisi kwa mujibu wa Sheria.
Baada ya maelezo hayo Polisi wamemrejesha Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam.

Aidha , viongozi wengine waliokuwa wanashikiliwa Mkoani Mwanza wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na baadhi yao walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na vyumba vya hotel ambako walikuwa wameshukia .

Waraka wa Mbowe Kwa Watanzania
Mwenyekiti Taifa Mhe. Freeman Mbowe ametuma waraka kwa Watanzania kama ifuatavyo;
"Hatimaye madai ya Katiba Mpya yamenisababishia kesi ya ugaidi, nipo tayari kwa mashtaka ya kuchongwa siogopi.
Ninaamini Dunia itaujua ukweli wa kile kinachoendelea Tanzania na kile tunachokipitia Watanzania.
Lakini pia itajua ukweli juu ya makosa haya ya kuchongwa.

Natoa wito kwa watanzania kuendeleza mapambano, haki hutafutwa” Mhe.
Freeman Mbowe.”

Imetolewa leo Alhamisi tarehe 22 Julai, 2021.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Nani atawaamini polisi wajinga kiasi hiki?
 
Rais ameapa kulinda Amani na utulivu wa nchi hii na endapo akitokea mtu au watu wanaleta au kutishia Amani ya nchi lazima wachukuliwe hatu za kisheria, haijalishi ni kiongozi wa kisiasa au kiongozi wa kidini.
Mbowe na genge lake hako juu ya sheria, huwezi kusema eti yeye akifanya makosa basi aachwe tu.
Mbowe na viongozi wenzake wanachochea na kuhamasisha vurugu, hata ange kuwa marekani lazima angekamatwa na kufunguliwa mashitaka.
SHERIA NI MSUMENO.
tusiwe wanafiki, alipo kamatwa DC sabaya tulishangilia kuwa sasa sheria inafuatwa, sasa amekamatwa Mbowe tunaona sheria haifuatwi!! jamani tuache vyombo vyetu vifanye kazi zake bila kuungiliwa au kushinikizwa.
kwa nn sheria ionekane kwa Sabaya tu na sio kwa Mbowe? tuache unafiki.
kama Mbowe anamakosa atafikishwa mahakamani kama walivyo wengine, tujifunze kuheshimu utawala wa sheria.
 
Pia taasisi hizo hizo zitatambua kuwa kumbe jpm hakua anakosea kuhusu huu upinzani uchwara, tatizo ni upinzani njia wanazotumia kumbe sio mfumo
Taja mfumo UPI unataka ,watu 300 kwenye kongamano lakini watu 5000 ruksa waingie uwanjani kutazama mpira
 
Lini awamu ya 5 mashirika haya yalisitisha misaada yao?!!!

1)USAID

2)DANIDA

3)NORAD

4)GTZ

Na mengineyo?!!
Kwani tangu tupate misaada tulisha faidika na nini;kama si taifa kudumbukia katika lindi la umaskini,nieli tusipate hiyo misaada labda tunaweza kujikomboa kifikira,tukaanza kutumia rasmali tulizopewa na Mungu,na tukavuka, misaada imetulemaza akili sana Watanzania, maana pasipo msaada tunaona atuwezi ishi.
 
Hii Taarifa Mbona sio ya Polisi au John Mrema ni Msemaji wa Polisi??? Wao Polisi hawajayoa Taarifa
 
Nchi ilikuwa imeanza kwenda vizuri lakini wajinga wachache kwa masilahi yao badala ya masilahi ya kitaifa wameamua kumshauri mama afanye udikiteta wapate kutimiza lengo lao, mama kuwa makini na washauri wako maana sasa wanaenda kukuharibia sifa zako zote
Ahaaa, nchi kwenda vizuri ni kuwaacha Chadema wapige kelele na kupayuka wqnavyotaka?
 
Back
Top Bottom