Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

..magaidi huwa wanakimbia na kwenda mafichoni iwapo washirika wao watakamatwa.

..sasa inashangaza "magaidi" wenzake na Mbowe walikamatwa tangu sept 2020, lakini mbowe tangu wakati huo alikuwa akisafiri kwenda nje na kurudi.

..kama Mbowe angekuwa ameshiriki njama za ugaidi, dalili ya kwanza ingekuwa ni yeye kukimbia nchi mara baada ya "magaidi" wenzake kukamatwa.

cc tindo, Erythrocyte , Salary Slip
 
Polisi wengi hali zao ngumu kutwa kucha wanatafuta nafuu ya maisha kwa kuombaomba na wengine kuomba wapangiwe vituo vyenye pesa kama Kulinda Ofisi/nyumba za Viongozi na wengine kuomba magepu ya kusafiri na vyombo vya mwaka 2019 kama treni/gari moshi
 
Huwezi juwa mkuu Prof Koboko.

Inawezekana mwanzo kesi ilikuwa inatengenezwa ionekane kifo cha Magufuli kinatokana na mbinu alizofanya Freeman Mbowe, ndizo zilizosababisha kifo hicho; lakini ikashindikana kuonyesha uhusiano wa Magufuli kuwa karibu na vituo vya mafuta na kilichosababisha kifo chake!
Walipoona siyo kazi rahisi kubambikizia hilo, ndiyo ikawa kama hivi tunavyoona sasa, kila mara kesi inafanyiwa marekebisho.

Nchi hii hata rais haoni aibu kutunga uongo mbele za raia zake. Hawa watu wanawadharau sana waTanzania na kuwaona kama mazuzu hivi yanayoweza kuamini kila kitu wanachotunga wao.
 
Rais hatakiwi kufanya siasa kwa kuongea uongo, anatakiwa kuongea facts.
Samia hatufai na katiba ya sasa haitufai. Tutadai katiba mpya usiku na mchana.
 
Members, kwa Mujibu wa msemaji wa Polisi David Misime mbele ya vyombo vya habari alisema Mbowe alikula njama kutaka kuua viongozi wa serikali, Lakini Ghafla siku ya kesi kutajwa mahakamani hati ya mashtaka ikabadilishwa na wa kaamua kukiondoa kipande alichokizungumza msemaji wa Polisi na kuamua kuweka Mbowe alikula njema kulipua vituo vya mafuta

Je? Polisi wanakusanya ushahidi wa kuunga unga

Rais Samia akihojiwa na BBC nae amejichanganya sana Katika Maelezo yake kuhusu suala la Freeman Mbowe, Inaonyesha dhahiri taarifa aliyopewa na wasaidizi wake imejazwa chumvi nyingi sana kwa kuambiwa Mbowe alishtakiwa mwezi septemba mwaka jana 2020.Wakati huo Mbowe ameshtakiwa mwaka huu 2021

Je, Rais Samia anaogopa joto la katiba mpya na Maandamano lililoanzishwa na Freeman Mbowe ndio maana akihojiwa na BBC amechanganya sana majibu kuhusu neno Demokrasia, Ni uhalisia Katika mahojiano yale Rais Samia anafahamu suala la Freeman Mbowe na yeye anaunga mkono ili atawale ufalme wa dunia kwa raha

Viongozi lazima watambue kufa kupo tu, Hata ukalindwa na mitutu na kuamua kwenda kuishi anga za juu au Sayari ya Mars kufa kupo pale pale, Kufa ni Kitendo cha Sekunde moja tu,

Viongozi wengi tulionao hawafanyi mazoezi unaona kabisa wengi wako Overweight hivyo magonjwa kama Pressure na moyo hayakwepeki

Kesi ya Freeman Mbowe inatuonyesha mambo mengi yaliyo sirini, Huku mtaani ukiangalia suala la Tozo la miamala na ishu ya Mbowe wengi wanamuoana Rais alishapoteza uelekeo, ccm na Chadema ni kama wamepigwa ganzi hawajui uelekeo wao ni upi kwa kesho
 
Si hivyo tu.Alisema,yeye pamoja na Sirro,kwamba ushahidi wanao mwingi hadi wakiubeba kwa mikono unamwagika.Ajabu lililojiri:Kila kesi ikisomwa wanaomba udhuru wa kutokukamilika upelelezi.

Nikajiuliza hivi ni kipi hutangulia?Kupeleleza na kupata ushahidi au kupata(kuupokea kutoka uwinguni)ushahidi ndipo unaingia kupeleleza?Hata hivyo yawezekana yasowezekana hasa kwa kizazi cha Kibindankoi.😝😝😝😝😝
 
Chadema sio chama cha siasa ni Genge la wahuni mchanganyiko wa magaidi.

Msajili alipaswa afutilie mbali hili Genge la kihalifu ambalo nia na dhamira yake ni kuvuruga amani ya nchi yetu.

Chadema ni Genge la kihalifu lililo jificha chini ya mwamvuli wa chama cha kisiasa.

vyombo vyetu vya dola vinapaswa vitazame genge hili kwa jicho la tatu.
 
Chadema sio chama cha siasa ni Genge la wahuni mchanganyiko wa magaidi.
Msajili alipaswa afutilie mbali hili Genge la kihalifu ambalo nia na dhamira yake ni kuvuruga amani ya nchi yetu...
Hapo utakuwa unaandika huku umekaza mishipa ya kiuno kwa sonona!
 
CCM ipo imara sana.

CCM haijayumba.

Si kutokuwepo kwa katiba mpya kutakakoiyumbisha CCM.

Si suala la TOZO litakayoiyumbusha CCM.

Tozo imefafanuliwa vyema tu.

Hoja ni kuwa viwango ni VIKUBWA tu.

Ila tunahitaji FEDHA kwa ajili ya MAENDELEO ya nchi.....na fedha hazinyeshi kama mvua huo ndio ukweli.

Kilimo chetu kiko chini.

Wataalamu wetu wamekuja na suluhisho la kilimo bora kwa kuipanga hiyo TOZO.

Mtanzania wa kawaida asiye katika makundi ya siasa mihemko anaelewa umuhimu wake.

#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Mpaka hapa hakuna shaka wala chenga kua mashtaka ya Mbowe ni ya kutunga
 
Rais hatakiwi kufanya siasa kwa kuongea uongo, anatakiwa kuongea facts.
Samia hatufai na katiba ya sasa haitufai. Tutadai katiba mpya usiku na mchana.
Huko mbeleni tuendako ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeweza kusimama na wenye haki.
 
Dada umeongea kwa kuegemea upande mmoja,jitahidi kubalance.
 
Kesi ya Freeman Mbowe inatuonyesha mambo mengi yaliyo sirini, Huku mtaani ukiangalia suala la Tozo la miamala na ishu ya Mbowe wengi wanamuoana Rais alishapoteza uelekeo
 
Baada ya kauli Tata na msumari wa Mama, Sasa tumaini ni kuomba shinikizo Kali Toka jumuia za kimataifa. Hata hivyo serikali imetimiza Lengo kuwapotezea Watanzania kuongelea Tozo, adhabu ya Mbowe inatosha.
 
Chadema sio chama cha siasa ni Genge la wahuni mchanganyiko wa magaidi.
Msajili alipaswa afutilie mbali hili Genge la kihalifu ambalo nia na dhamira yake ni kuvuruga amani ya nchi yetu...
Ndio maana mungu anawanyofoa ibilisi wenu mmoja mmoja ili kuliponya taifa mateso na uhalifu mnaowafanyia chadema Kama wangekuwa wahalifu wangeshalitarite (retaliation) lakini kwa uvumilivu mkubwa chadema wanawageuzia na shavu la upande wa pili. Jiulize ni lipi hamjawafanyia chadema?
1.Mmewabambikia kesi
2.Mmewafilisi kwa Kodi bambikizi
3.Mmeharibu vitegauchumi vyao
4.Mmewateka viongozi wao.
5.Mmewafunga magerezani
6. Mmewapiga risasi
7.Mmewauwa wengine kwa kuwachinja
8.Mmewafanya kuwa wakimbizi.
9.Chaguzi mmewaibia walizoshinda

Ni madhila gani chadema hamjawafanyia? Kama kweli wangekuwa magaidi Kama mnavyowabrand ujinga wote huo mliowafanyia ingekuwa wanasiasa wa nchi nyingine wangesha jibu mapigo kitambo na hii nchi wangeshaitia kiberiti Ila busara za kina mbowe zinailinda Sana amani ya hii nchi.
 
Kwa jinsi cdm walivyoshangalia kile kifo na Mbowe kuanza kumtukana hayati mpaka akina Lisu kuwa watoa taarifa nyeti!!!!!!! Inafikirisha.
My wish mamlaka siziogope kelele mpaka haki itendeke kwa ukamilifu wake.

Madam watakupigia kelele sana usijaribu kugeuka nyuma wanakufanyia distraction tu hawa kwa makusudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…