Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

We jifariji tuu.unafikiri CHAMUDATA ni chama cha upinzani???ni CDM tuu,wengine wahuni tuu.uyo jpm Mungu kamchukua ili iwe fundisho kwenu.bado wengine wabishi
Mbona mnahangaika sana? mlimchukua enh? hofu ya nini? andamaneni basi nyie watanzania polisi hawawezi kuwaua wote mko wengi sana.
 
Binadamu ni wageukaji wakati wowote.
Yalihotokea South Africa ni fundisho tosha kwa nchi zetu Africa!
Tusishangae na sisi yakatukuta endapo tushaambiwa tuhame twende Rwanda!!
Katiba mpya ni muhimu kwa kizazi kijacho na haikwepeki asilani!.

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
Ila rekebisha kidogo hapo "tuhame twende Rwanda" ni "tuhame twende Burundi"
 
Baada ya kutoka RUMANDE alikokaa kwa miaka 9 kasoro ninayakumbuka vyema maneno ya Sheikh Mselem bin Ali wa Uamsho pale aliposema "tukiambiwa hili msifanye ,hili muache basi hatutofanya kwani huwezi kupambana na mwenye nguvu na mamlaka ya kinchi "

#NchiKwanza
#AmaniKwanza
#JMT4Ever
 
Haki itasimama huyu mvaa ushungi aiambiedunia huu ugaidi wa Mbowe kaudanyia wapi,lini na ni Nani ameadhirika asitusababishie chuki zisizo na maana.
 
Baada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM.Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.

View attachment 1862953

====

UPDATES;

=====

TAARIFA KWA UMMA

JESHI LA POLISI LAMTUHUMU MWENYEKITI WA CHAMA
MHE.FREEMAN MBOWE NA "MAKOSA YA UGAIDI"

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe alifikishwa Dar es Salaam jana majira ya saa tatu usiku chini ya ulinzi wa Polisi , walimpeleka nyumbani kwake Mikocheni Kwa ajili ya kumfanyia upekuzi ambao ulichukua takribani saa mbili na nusu.

Baada ya upekuzi huo Polisi waliondoka na Kompyuta mpakato (Laptop) na Vishikwambi (tablets) za watoto wake, Kompyuta mpakato moja ya kwake na modem ya Internet Kwa ajili ya uchunguzi wao.

Leo majira ya saa Saba mchana Polisi walimfikisha Mhe. Freeman Mbowe Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kuchukua maelezo yake.

Polisi walitaka maelezo kutoka Kwa Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na kosa waliloliita 'KULA NJAMA ZA KUTENDA KOSA LA UGAIDI'

Baada ya maelezo hayo ya Polisi Mhe. Freeman Mbowe alitumia haki yake ya kisheria na aliamua kutokutoa maelezo yoyote Polisi kwa mujibu wa Sheria. Baada ya maelezo hayo Polisi wamemrejesha Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam.

Aidha , viongozi wengine waliokuwa wanashikiliwa Mkoani Mwanza wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na baadhi yao walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na vyumba vya hotel ambako walikuwa wameshukia .

Waraka wa Mbowe kwa Watanzania
Mwenyekiti Taifa Mhe. Freeman Mbowe ametuma waraka kwa Watanzania kama ifuatavyo;
"Hatimaye madai ya Katiba Mpya yamenisababishia kesi ya ugaidi, nipo tayari kwa mashtaka ya kuchongwa siogopi. Ninaamini Dunia itaujua ukweli wa kile kinachoendelea Tanzania na kile tunachokipitia Watanzania. Lakini pia itajua ukweli juu ya makosa haya ya kuchongwa.

Natoa wito kwa watanzania kuendeleza mapambano, haki hutafutwa” Mhe.
Freeman Mbowe.”

Imetolewa leo Alhamisi tarehe 22 Julai, 2021.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

=====

UPDATE:

View attachment 1863559
View attachment 1863560
 
Mamlaka kama ile ya muuaji na mwendawazimu aliyefariki kwa korona ndiyo watu wazitii? Korona ilituondolea uchafu!
Hahaha...chuma kiliwanyoosha, na hakikuwahi vaa barakoa, hiyo corona yenu ya kila aina ilipofail ndo mkaamua kuwatendea uhaini watanzania, takataka kama wewe huwezi jua lolote.
 
'
JamiiForums1120482783.jpg
 
Ulifutiwa KESI zako....

Ukalipwa FEDHA zako....

Bado tu....

We umo tu ....

Tena "umo" kwa vitu visivyo msingi...

Badala ya KULIJENGA TAIFA ,NA KUWAACHA VIJANA WALIJENGE TAIFA na kuwa na uchumi bora ndani ya femili zao Kama ULIVYO WEWE...kinyume chake UNAWAHAMASISHA WAFANYE FUJO NA KUPELEKEA NCHI KUKOSA UTULIVU.....

#KaziIendelee
#NchiKwanzaSiasaBaadae
 
Yaelekea Polisi wetu wana kesi nyingi za kusadikika ambazo wanazo kwenye makabati yao ambazo zinasubiri mtu ambaye wanataka kumwondoa kwenye circulation wambambikie.

Kuna dogo moja mpiga debe walimpa kesi ya armed robbery akawekwa rumande Keko kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka familia ilivyojichangisha kesi ikaisha bila hata kwenda mahakamani.

Polisi pekee atakaenda peponi ni afande Masudi Mohammed ambaye kifo chake enzi za Hutu Immigrants Reign of Terror kilizua utata!
 
Jeshi la Polisi limesema Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anashikiliwa kwa tuhuma za kula njama ya kufanya vitendo vya kigaidi ikiwepo kuua Viongozi wa Serikali ambapo wenzake 6 walishafikishwa Mahakamani.

“Freeman Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa ana tuhuma zinazomkabili zinachunguzwa na kwamba wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua nyingine za kisheria mara tu uchunguzi utakapokamilika hatua ambayo imefikiwa kwa sasa”

“Kama ilivyo kwa baadhi ya Watu kucheza na nyakati na matukio akaona ni vyema akimbilie Mwanza kwa kigezo cha kongamano la Katiba Mpya ili akikamatwa Umma uamini amekamatwa kwasababu hiyo”

“Hata hivyo uchunguzi unaendelea kule Mwanza kutokana na vitendo vya uvunjifu wa amani, ukibaini kuna sheria aliyovunja hatutasita pia kumfikisha Mahakamani pamoja na Viongozi wenzake wanaoshikiliwa kule”———-David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi
Hivi polisi wapo ajili ya wananchi kweli au CCM na genge lake?
 
Hahaha...chuma kiliwanyoosha, na hakikuwahi vaa barakoa, hiyo corona yenu ya kila aina ilipofail ndo mkaamua kuwatendea uhaini watanzania, takataka kama wewe huwezi jua lolote.
Mwendawazimu alishindwa ku-control uwendawazimu wake. Hakutatokea tena rais mshamba kama yule.
 
Back
Top Bottom