Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mission ya kumuengua Lissu kwenye Uongozi!
"Jiuzuru Umakamu Mwenyekiti gombea Uenyekiti tukuangushe"!
Baada ya hapo "Lissu chagua kukiacha Chama au kaa kimya kabisa"!
Hapo ni Vita ya Fedha(Mbowe) na Ukweli (Lissu).
Who will be the winner?
 
Safi sana, mgombea dhaifu na asiye na ushawishi katangaza nia.

Wale waliokuwa wanataka Lisu mgombea mwenye ushawishi, aachiwe nafasi, apite bila kupingwa, wasiopenda demokrasia, mnaumia sana, lakini hili ni muhimu kwa demokrasia nchini.
 
Hahaha mnaogopa Lisu atakosa vyote?
Lissu mwenyekiti chama ajae, binafsi nimefurahi Mbowe kutangaza kugombea ili sanduku la kura liamue ,ccm hawakawii sema lissu alibebwa kwa Mbowe kujitoa, alafu sio sawa Mbowe pia anawakereketwa wake ,sasa angesema agombei wale wanaomuunga mkono angewaacha katika hali gani? Isingekuwa sawa .

Wanaombeza mbowe bado wachanga katika siasa na hawajui Dunia .

Kazi kwa wajumbe Tuleteeni lissu
 
Hili nalifahamu, ni Mbowe ndiye aliyemuomba Lisu amtetee Chacha Wangwe pamoja na wananchi, na ni Mbowe ndiye aliyemshawishi Lisu kujounga Chadema.

Unaposikia Mbowe anaitwa mwamba basi ni mwamba kweli, orodha kwa uchache Mwamba aliwashawishi hawa kujiunga Chadema, Zitto Kabwe, John Mnyika, Halima Mdee, Joseph Mbilinyi Sugu, Joseph Haule Profesa Jay, Godbless Lema kwa uchache hao watu maarufu mwamba ndio kawaingiza Chadema, hii ni talent and charismatic.
Ila sasa miaka 21 inatosha.Hatukatai kuwa kafanya kazi kubwa.Ila kipindi hiki angeachia na wengine.
 
Mbowe hamkutuma lissu kwenda kumtrtea chacha wangwe. Lissu alianza kupambana na kesi zamigodini 2001 kabla hata ya hiyo ya wangwe 2003. Labda useme hiyo 2001 pia alitumwa na mbowe.

Wangwe ndio Alifanya aingie chadema
Kumbe nia yako ni kubishana, mimi ni wrong person, siko tayari kwa hilo, watu wote wenye akili wanajuwa Lisu ameletwa na Mbowe, sasa chuki zako kwa Mbowe zinakutia upofu na kujitoa akili.
 
Kila baada ya miaka 10 CCM tunabadili mwenyekiti ila hawa wapinzani kama hii NGO ya mbowe hahaha yaani eti anaona ana haki ya kuendelea kuwa mwenyekiti wa NGO hahaha yaani CCM tutaendelea kutawala mpaka vitukuu
 
Back
Top Bottom