Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wajumbe wananunuliwa kwa pesa au kwa ahadi za kupewa nafasi za kugombea ubunge mwakani au nafasi za viti/u
maalum za ubunge.Hivyo vitu Lissu hawezi kuvifanya kwa sababu sio mnafiki.

Siasa za kiafrika huwezi kuzimudu kwa muda mrefu kama sio mnafiki.Either utaondolewa mapema au utachafuliwa kwa propaganda ambazo jamii ya kinafiki ya kiafrika itazichukua na kukupondea nazo kichwani.Mbowe ni mzuri kwenye hizo negotiations za kimaslahi ya pande zote mbili.

Kwahiyo tegemea kuwa Mbowe kabla ya kuamua kugombea ameshajua kura zake zitatoka wapi.

Mtu msafi kama Lissu ni vigumu kupigiwa kura na watu wanaotaka wafaidike na hizo kura zao kupitia yeye.Mbowe kwakuwa tu maslahi yake yanahakikishwa basi yeye pia
hana nongwa kuwapa maslahi yao watu waliompa maslahi yake.

Tegemea wale covid 19 kurudi/kusamehewa baada ya ushindi wa Mbowe.Ni maslahi maslahi maslahi....
Lissu anashinda mchana, mnaogopa
 
Ukifikiria hoja zinazojengwa na FAM kwenye press pamoja na Wenje ktk interview yake jana nyingi si za kukijenga Chama Chao bali zinalenga kumwangusha TAL ktk uwanja wa siasa. Wemeruhusu DIVIDE & RULE tactic kukidhoofisha chama Chao.
Ulitaka waseme uongo.Aliyeanza kuropoka humlaumu unawalaumu wanaotukanwa?Lisu ni muongo,mzushi na it is time sasa ajibiwe ili wanachadema na watanzania kwa ujumla wajue ukweli.
 
Wakati wowote kuanzia sasa Mhe Freeman Mbowe kutoa tamko rasmi la ama atagombea Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa ama laa.

Mtakumbuka Mhe Freeman Mbowe ameitumikia nafasi hii kwa zaidi ya miongo miwili sawa na miaka 21 mfululizo.

Endapo atatangaza kugombea tena atakuwa ni mgombea wa nne nyuma ya Tundu Lissu na Odero Odero,

Je, kama Taifa tunatarajia nini kutoka Upinzani kuelekea 2025?

Usiondoke hapa Jf kwa habari zaidi

=======================================

Siku ya leo Disemba 12, 2024 Freeman Mbowe ametangaza rasmi kugombea kwa mara nyingine nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Mbowe amsema kuwa kutokana na Uchaguzi mkuu ambao unakuja si vyema kubadilisha "makamanda" na kwamba bado yupo sana kuongoza chama hicho na mara baada ya mkutano anaenda kuchaukua fomu kwenye makao makuu ya chama hicho, Mikocheni.

"Kwa kuzingatia yote haya na mengine mengi ambayo sitaki kuwachosha. Nilisema mara nyingi kuwa nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka katikati ya minyukano iliyopo. Kwa hiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea"

View: https://www.youtube.com/live/8WGa7Xv3hKo?si=JjooipgRmN035_2F

"Nipo,nitakuwepo na anayetaka kugombea tukutane kwa box"Ila sasa box hizi zisiwe za waenguaji na wajaza mabox kabla ya wakati kama kule kwa jirani mwovu.
 
Kwenye hotuba yake Mbowe kasisitiza ya kwamba Wenyeviti wa CHADEMA waliotangulia walistaafu wakiwa na miaka 68 kwa Mtei na 67 kwa Makani. Hivyo yeye bado anamiaka mitano afikishe 68.

Najiuliza swali je, ni kwamba yeye anatumika umri wa miaka 68 kama kigezo cha kugombea uenyekiti au anagombea uenyekiti maana ana mzigo wa kukitumikia chama Cha CHADEMA.
 
Wakati Chacha Wangwe anataka kugombea uenyekiti.Lissu hakuwa Chadema? ILIKUWA MWAKA 2008.Ninakumbuka Lissu alimlalamikia sana Chacha Wangwe hadi kusema kamsaidia case nyingi mno.I wish niupate ule uzi niuperuzi.Lissu alikuwa upande wa Mbowe .
Labda hapa twende sawa, Mbowe ndio alimtuma Lisu kwenda kumtetea Chacha Wangwe ambaye alikuwa ni diwani wa Tarime na alikuwa amebambikwa kesi nyingi lakini Mbowe kipindi hicho alidhani Lisu ni Chadema kumbe Lisu ni mwanachama wa Nccr Mageuzi.

Kwahiyo hizo kesi za Chacha Wangwe ndio zilimfanya Mbowe kuongea na Lisu amtetee Chavha Wangwe pamoja na wananchi, kwahiyo link ya Chacha Wangwe kuwa Karibu na Lisu link ni Mbowe.

Nimeona niweke record sawa.
 
Labda hapa twende sawa, Mbowe ndio alimtuma Lisu kwenda kumtegea Chacha Wangwe ambaye alikuwa ni diwani wa Tarime na alikuwa amebambikwa kesi nyingi lakini Mbowe kipindi hicho alidhani Lisu ni Chadema kumbe Lisu ni mwanachama wa Nccr Mageuzi.

Kwahiyo hizo kesi za Chacha Wangwe ndio zilimfanya Mbowe kuongea na Lisu amtetee Chavha Wangwe pamoja na wananchi, kwahiyo link ya Chacha Wangwe kuwa Karibu na Lisu link ni Mbowe.

Nimeona niweke record sawa.
Hivyo kwenye lile sakata 2008 Lissu alikuwa mwanasheria wa CHADEMA. Believe me ninakumbuka kabisa Lissu kusema kamtetea sana Wangwe.Na anashangaa Wangwe kutaka kumwaga mbonga.
 
Wakati wowote kuanzia sasa Mhe Freeman Mbowe kutoa tamko rasmi la ama atagombea Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa ama laa.

Mtakumbuka Mhe Freeman Mbowe ameitumikia nafasi hii kwa zaidi ya miongo miwili sawa na miaka 21 mfululizo.

Endapo atatangaza kugombea tena atakuwa ni mgombea wa nne nyuma ya Tundu Lissu na Odero Odero,

Je, kama Taifa tunatarajia nini kutoka Upinzani kuelekea 2025?

Usiondoke hapa Jf kwa habari zaidi

=======================================

Siku ya leo Disemba 12, 2024 Freeman Mbowe ametangaza rasmi kugombea kwa mara nyingine nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Mbowe amsema kuwa kutokana na Uchaguzi mkuu ambao unakuja si vyema kubadilisha "makamanda" na kwamba bado yupo sana kuongoza chama hicho na mara baada ya mkutano anaenda kuchaukua fomu kwenye makao makuu ya chama hicho, Mikocheni.

"Kwa kuzingatia yote haya na mengine mengi ambayo sitaki kuwachosha. Nilisema mara nyingi kuwa nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka katikati ya minyukano iliyopo. Kwa hiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea"

View attachment 3181677

View: https://www.youtube.com/live/8WGa7Xv3hKo?si=JjooipgRmN035_2F

Ashazoe kuohngqa wale wahuni
 
Back
Top Bottom