Pre GE2025 Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Pre GE2025 Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Dr Slaa nilikuwa naye Kamati ya Mapokezi ya Papa Yohanne Paul Mimi nilikuwa kituo cha Luhuwiko Songea

Ni Mtu makini Sana 😂😂😂
Wakati uleee kabla Slaa hajasaliti kiapo chake cha u~ padre ambacho kinamtafuna hadi keshokutwa
 
Duh!...yaani Lissu anatumika tu?... tuhuma nzito hizi.

Fundi Mchundo Retired Quinine JokaKuu
Kweli tupu. Kuna pia wale ambao kwa namna moja au nyingine wanaamini kuwa hawajatendewa haki katika uongozi wake. Hii ni pamoja na Lissu mwenyewe ambae amesema wazi kuwa Mbowe alitaka kumtilia kauzibe kupitia Wenje. Kuna wale walioshindwa au mtu wao alishindwa ( k.m. Msigwa)chaguzi tofauti.

Na pia wako ambao kwa dhati kabisa wanaamini kuwa kuna haja ya kuibadilisha Chadema ili ionekane kuwa inampambania mtanzania wa kawaida. Hawa wa mwisho hawataki kabisa CDM ipasuke ila hawana jinsi.

Amandla...
 
Unajua ubelgiji anaenda sababu ya matibabu? Ule mwili bado hauko sawa ? Kila mwez lazima akafanye check up ulikuwa unajua?
Kwa hiyo chadema inahitaji mgonjwa anayeshinda ubelgiji hospitali kuwa mwenyekiti ambaye muda mwingi anakuwa hospitali ubelgiji?
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA @chadematzofficial Freeman Mbowe amesema kuna makundi yanayoratibu kufanyika mapinduzi ndani ya chama hicho na makundi hayo ndiyo yanayomsukuma Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu kugombea nafasi ya Uenyekiti.


“Kuna kundi linaloitwa diaspora (watanzania waishio ughaibuni) ni kundi dogo tu wala sio kusema ni diaspora wote wa Tanzania hili kundi dogo linalojaribu kupanga mapinduzi ndani ya CHADEMA wengine hata hatuwajui tunawaona tu kwenye majina ya mitandaoni wanajiita Tanzania Diaspora ni kundi ndani ya Diaspora”

Mbowe ameeleza kuwa zaidi ya kundi hilo kuna kikundi kingine kinachoitwa Sauti ya Watanzania ambacho kinachoongozwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbroad Silaa

“Kuna makundi ya watu kama Dkt. Silaa na kikundi kinachojiita Sauti ya Watanzania, Dkt. Silaa alikimbia CHADEMA mwenyewe akaenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) akafungiwa Serena pale(Serena Hotel) baadae akahamishiwa Canada akapewa zawadi ya ubalozi.”

Mbowe ameongeza kuwa amekuwa akishangazwa na wanaomuunga mkono Lissu kuwa sio watu ambao ni wanachama kweli kweli hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini Dkt. Silaa hawekezi nguvu kwenye chama chake bali anawekeza muda na nguvu CHADEMA.

“Kazi aliyoifanya muda wote akiwa balozi(Dkt.Silaa) chini ya utawala wa Magufuli(Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) ni kujaribu kuichonganisha CHADEMA na kutoa taarifa na mpaka kuandika kitabu cha uongo eti leo Dkt.Silaa ndiye anafanya kampeni ya Lissu kuchukua uongozi wa chama alisahau nini Dkt Silaa ambacho leo anakitaka”

Hata hivyo Mbowe ameongeza kuwa wengine wanaomuunga mkono Lissu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa ni kada wa CCM.

Source: Jambo TV
Haahaa Mbowe kaanza kulialia eti mapinduzi, haahaa
 
Jaribu nawewe uwe kibaraka,uwaambie wabaokufanya kibaraka wakupige hata risasi mbili
Sihitaji kuishi maisha ya kutumikia watu wengine na kuhatarisha mustakabli wangu na kizazi changu.

Huyo kibaraka anawatumikia hao diaspora Kwa sababu familia yake Iko huko Ubeberuni.
 
Dr. Slaa naye ni njaa nyingine, katumiwa na Jiwe hadi kupewa ubalozi sasa hivi ni damped person anahangaika njaa ni kali kaona ajiunge Team Lissu walau apate chochote kitu.

Wazee wengine bana ni matatizo sana.
 
Diaspora tena ? Haoni anaua harakati za uraia pacha🐼
 
Wanachadema wataamua, kama waliweza kumpa umakamu akiwa kitandani, sembuse now?
Kashayatimba yule - kasome historia ya yule mwanapunda aliyembeba Yesu....ilikuwaje alivyoamua kurudi mwenyewe kesho yake tena kwa madoido...
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTz Freeman Mbowe @freemanmbowetz amesema kuna makundi yanayoratibu kufanyika mapinduzi ndani ya chama hicho na makundi hayo ndiyo yanayomsukuma Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu @TunduALissu kugombea nafasi ya Uenyekiti.

Mbowe ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na mtangazaji wa Crown Media, Salim Kikeke Salym na kueleza kuwa “Kuna kundi linaloitwa diaspora (watanzania waishio ughaibuni) ni kundi dogo tu wala sio kusema ni diaspora wote wa Tanzania hili kundi dogo linalojaribu kupanga mapinduzi ndani ya CHADEMA wengine hata hatuwajui tunawaona tu kwenye majina ya mitandaoni wanajiita Tanzania Diaspora ni kundi ndani ya Diaspora”

Mbowe ameeleza kuwa zaidi ya kundi hilo kuna kikundi kingine kinachoitwa Sauti ya Watanzania ambacho kinachoongozwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Silaa “kuna makundi ya watu kama Dkt. Silaa na kikundi kinachojiita Sauti ya Watanzania, Dkt. Silaa alikimbia CHADEMA mwenyewe akaenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) @CCMTanzania akafungiwa Serena pale(Serena Hotel) baadae akahamishiwa Canada akapewa zawadi ya ubalozi.”

Mbowe ameongeza kuwa amekuwa akishangazwa na wanaomuunga mkono Lissu kuwa sio watu ambao ni wanachama wa CHADEMA na hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini Dkt. Silaa hawekezi nguvu kwenye chama chake bali anawekeza muda na nguvu CHADEMA.

“Kazi aliyoifanya muda wote akiwa balozi(Dkt. Silaa) chini ya utawala wa Magufuli(Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) ni kujaribu kuichonganisha CHADEMA na kutoa taarifa na mpaka kuandika kitabu cha uongo eti leo Dkt. Silaa ndiye anafanya kampeni ya Lissu kuchukua uongozi wa chama alisahau nini Dkt. Silaa ambacho leo anakitaka”

Hata hivyo Mbowe ameongeza kuwa wengine wanaomuunga mkono Lissu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa Msigwapeter ambaye kwa sasa ni kada wa CCM

Chanzo : Jambo TV
 
Katika hili sakata la uchaguzi unaona kabisa Mbowe hakutegemea upinzani kwenye nafasi yake. Hii inaonesha alikuwa amejiandaa na business as usual sababu ukimsikiliza hana hoja zinazoshawishi yeye kuendelea kuwa mwenyekiti zaidi ya kulalamika tu.
Kila wakati anapokuwepo mtu wa kuchallenge nafasi yake anakimbilia watu wanataka kufanya mapinduzi.
 
Back
Top Bottom