Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

It is only chadema who can see this, wengine ni Rubbish minds
Mbona CCM mmeanza kulalamika tena Kama watoto wa kambo? Si mlisema Mbowe ni gaidi ninyi mkishirikiana na genge lenu la akina Kingai na Mahita.
Subirini mfunzwe siasa ninyi buku7 wapiga deki na kubrashi viatu hapo Lumumba.
Ndio maana Polepole alikuwa anawauliza mnaijua VX ninyi buku7?
 
Katiba mpya itoke wapi? We endelea kufanywa mpira wa dana dana huku mwenyekiti na genge lake wakiendelea kuupiga mwingi kupitia mialiko ya raisi. Mmeshaambiwa siku zote hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Jamaa anatengeneza pesa ndefu kupitia siasa uchwara, huku akiwaacha watu wenye misimamo thabiti na chama wakiendelea kutokwa mapovu huko belgium na canada. Endelea na kazi ya kuwarubuni wana mbeya ili itapokuwa inaanzishwa michango ya chama wawe mstari wa mbele kukichangia.
Ukiambiwa mimi ni miongoni mwa Timu ya Chadema inayokutana na Samia utakufa au utaishi ?
 
Bosi hanuniwi, tunajua ukitoka pale lazima kananii ka khaki kanakuhusu, leo John Mrema atarudi nyumbani na mfuko wenye kuku, nyama na pilipili.

Benson Kigaila wasipomwangalia anaweza kuzima, maana mle ndani Kuna Kila aina ya pombe na vinywaji laini. Naomba watu wa ikulu wamfungie tu kwenye mfuko akanywee kwake.

Watatoka humo wamelewa
 
Hata mi nawashangaa. Wachochee Watanzania wa kawaida ili kuilazimisha CCM kuleta mabadiliko. CCM walimfanyia hadaa mpaka Maalim Seif. Walijifanya kupatana lakini alipowashindwa kwenye sanduku la kura, wakafuta matokeo ya uchaguzi. Hivi Mbowe na wenzie wamesahau yote haya? CCM wana kawaida ya kujifanya wanapoona mambo hayaendi vizuri ili tu wakati wao wa kuiba kura ufike kukiwa na hali ya utulivu ktk nchi.
Wanafuata nini ikulu kila mara kama sio kupotezeana muda?
 
Ukiambiwa mimi ni miongoni mwa Timu ya Chadema inayokutana na Samia utakufa au utaishi ?
Kweli siasa za Tanzania zinaendeshwa kwa njia ya ulaghai 😂😂🤣🤣🤣

IMG-20220520-WA0015.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Mei 2022 ameongoza kikao cha majadiliano ya pamoja kati ya ujumbe wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Baadhi ya viongozi wa CCM ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa - Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu shaka.

Na viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.​


ikulu_mawasiliano-20220520-0002.jpg


ikulu_mawasiliano-20220520-0001.jpg


FB_IMG_1653070823516.jpg


FB_IMG_1653070916756.jpg
 
Mbowe awe makini, CCM sio wa kuamini kuwa wanaweza kuweka mazingira yatayoruhusu wao kuachia dola kwa amani.

Anyway, inawezekana strategy ya CHADEMA ni kwanza kutumia meza ya mazungumzo(wasije kulaumiwa kuwa walikataa hiyo fursa), ili kesho na keshokutwa wakitumia mbinu mbadala, wasilaumiwe.

Kwa maneno mengine, watayokubaliana yatakuwa documented na kuwa public, hivyo ataenda kinyume, ndio atalaumiwa.

Ni mtazamo wangu.
 
Ni suala la muda tu. Yetu macho tuone, masikio tusikie, midomo tucheke, vidole tuwasimange humu.
 
Huyu Maza ana jambo lake kwa mustakabari wa taifa letu

Mi nilisema toka mwanzo kwamba ana nafasi kubwa saana tena ya wazi ya kuzoa marks zoote za watangulizi wake

Anaweza kutoa katiba mpya...kumbukeni JK alitishwa na wana CCM akagwaya...

Wacha tusubiri....kwani subira huvuta kheri...ila sharti ni moja kwamba kheri yenyewe iwe na dalili ya kuja.

Tunasubiri - watanzania sisi tuna sifa hii.
 
Back
Top Bottom