Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.

- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.

- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.

- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
Wacha waendelee kusubiria huruma za watawala . 2025 hii hapa soon
 
Pongezi nyingi sana kwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, Pongezi kwa kwa mwenyekiti wa Chadema Mbowe kwa kuweka maslahi ya Tanzania mbele.
hicho ndicho watanzania tunacho kitaka, amani na utulivu.
 
Tindo mbonà unaniweka angle nyingine with regard to your credibility on JF. Mandela alizungumza na De Klerk akiwa gerezani and mazungumzo beared some positive results, ngoja wamsikilize. Mtu hakatai wito hukataa analoitiwa
Mtaitwa hivyo mpaka lini na nyie . hebu jitambueni
 
Unachosema ni sahihi lakini bahati mbaya sana mkuu hutoi alternative wanafanye nini badala yake.
Chadema wanaangalia na aina ya jamii tuliyonayo. Mbali na maridhiano njia pekee ni maandamano na kufanya nchi isitawalike. Yuko wapi mwananchi wa kufanya hayo? Wazee wa nchi wapo kimya,wamejaa unafiki,wananchi wanalalamika kichini chini. Sisi wachache mimi na wewe tumejificha kwenye keyboard. Mbowe afanye nini zaidi ya kutumia fursa ya kukaa meza moja.
Kukaa meza moja pia haimaanishi kusaliti misisimamo bali kueleza misimamo badala ya kutunishiana misuli kwenye majukwaa. Utatuna msuli jukwaani lakini ili unayemtunishia akupate vizuri inabidi akusikilize ukiwa kwenye utulivu na umweleze kwa ufasaha.

Ni kipi ambacho Chadema hawajafanya katika kutunisha misuli. Waliingia barabarani ikapalekea mauaji kesi ikawageuka na wananchi hawakuchukua hatua yeyote. Mbowe kakaa jela,Lissu kapigwa risasi mchana. Uchaguzi kura zimeibwa nk Wananchi walichukua hatua gani kali?

Naunga mkoni maridhiano kwa sababu hayupo raia wa kuingia barabarani kutumia nguvu ya umma
Umemaliza kazi.
 
Mkuu
Wanaccm Lazima tuwe na uwezo wa kufikiri sawasawa!
JIWE alinajisi uchaguzi nini kilimpata!!?Hadi akaingiza covid-19 Bungeni na haikutosha Hadi ikaigharimu serikali take!!!?
Unafikiri Sasa HIVI Kati ya mama na Mbowe nani anamuita mwenziwe IKULU!!?kama SERIKALI haioni umuhimu wa UPINZANI!!? HIVI unajua kesi ya MBOWE ilikuwa inaenda kuigharimu serikali ndio maana watu walitumwa wammbembeleze Mbowe atoke na alipototoka akaitwa ikulu Moja kwa Moja!!?
NAJUA MADARAKA YAMEPOFUSHA WANACCM WENGI NA HAWAONI MAMBO SAWASAWA!!

NIKUJUZE TU KIFUPI NI KWAMBA KUONDOLEWA KWA WABUNGE WA COVID-19 NI MAAGIZO YA THE STATE KWA MAMA SASA MAMA ANAOGOPA WAKIONDOKA NA SERIKALI YAKE ITAKUFA!!
SASA ANATAKA CHADEMA IRIDHIE WABAKI KIBISHI KINYUME NA TARATIBU HAPO NDIO KAZI!
KAMA UNAFIKIRI RAIS ANAWEZA TAWALA BILA UPINZANI BUNGENI NENDA KAMUULIZE JPM CHATO KWANINI ALITAFUTA WABUNGE WA UPINZANI KWA MLANGO WA NYUMA!!!!
I REST MY CASE
Naongezea kuwa uwepo wa covid-19 Bungeni ni kufeli kea Tiss kwenye uchaguzi wa 2020 kwasababu Tiss walicheza tune ya CCM wakati wa uchaguzi wakasahau utaifa SASA Tiss imeikosea NCHI na the state haitokubali ujinga kama huo tena na LAZIMA katiba MPYA ipatikane Ili kuepuka ujinga kama ule mlioubariki uchaguzi 2020!!!TISS ITUBU KWA KUINGIZA TANZANIA MATATIZONI NDIO MAANA WAKABARIKI UHUNI WA COVID 19 ILI KUINUSURU SERIKALI YAKE KISHERIA ZA KIMATAIFA NA UHALALI WAKE!!!
UMENIELEWA!!
Wewe haya umeyatoa wapi?
 
Wakuu,

Muda huu M/Kiti wa CHADEMA na viongozi waandamizi 9 wa chama hicho wapo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Tutarajie jambo gani jipya? Ndo ukurasa mpya wa Siasa za Tanzania?

UPDATE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.

View attachment 2232248View attachment 2232250
View attachment 2232257View attachment 2232258View attachment 2232259

View attachment 2232260
View attachment 2232570
Chadema imeshafika bei kitambo sana toka mbowe akubali kutoka jela kwa sharti la kuwa remote ya mama, hao kina tundu lissu hawana tena midomo wamefika mahali wakaona bora yaishe, Tanganyika kwenye mapambano siku zote si watu wakweli

Watanzania bado wanahitaji upinzani madhubuti wa kuiondoa ccm madarakani., tutamkumbuka na kumuenzi Maalim Seif Sharif Hamad siku zote, jemedari ambaye hakuwahi kutetereka wala kuyumba yumba kwenye mapambano.
 
Je Chadema wametoa taarifa yeyeto kuhusu mazungumzo ya Ikulu?
 
Kesi Iko mahakamani, hakuna mhimili unaweza kuingilia mahakama
Haaaaaa,mbona mhimili mmoja ilishaingilia huku kesi hata haijatajwa/kusomwa.Amiri tunaye.mihimili baadae
 
Bosi hanuniwi, tunajua ukitoka pale lazima kananii ka khaki kanakuhusu, leo John Mrema atarudi nyumbani na mfuko wenye kuku, nyama na pilipili.

Benson Kigaila wasipomwangalia anaweza kuzima, maana mle ndani Kuna Kila aina ya pombe na vinywaji laini. Naomba watu wa ikulu wamfungie tu kwenye mfuko akanywee kwake.

Watatoka humo wamelewa
Acha dharau ndg. Unaweza kufikiri una maisha kumbe huna.
Weka akiba ya maneno.....
 
To open up a new chapter as a nation haijawahi kuwa dhambi...

Hili kama ni kweli bac ni jambo jema kwa kila mwenye pumzi..

Narudia tena Political reconciliation ndiyo njia pekee ya kujenga taifa imara lenye umoja na nguvu kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.

Nchi haiwezi kujengwa na mawazo ya upande mmoja.
Wewe ndg yangu nchi inaongozwa na mifumo sio hizo danganya Toto umeshawahi kuona raia walioweka mifumo ktk nchi zao viongozi wao hukutana kwenye mambo kama hayaa
 
Sikuandika hivyo, isipokuwa wewe ndo umeelewa na kufikiria hivyo. Ukitumia akili iliyohuru utatambua kuwa jamaa anafanya siasa kwa lengo na masilahi ya nani.
Anhaa! Labda hata kwenye ile kesi ya mchongo, kwa akili yako huru, alilipwa!
 
Chadema imeshafika bei kitambo sana toka mbowe akubali kutoka jela kwa sharti la kuwa remote ya mama, hao kina tundu lissu hawana tena midomo wamefika mahali wakaona bora yaishe, Tanganyika kwenye mapambano siku zote si watu wakweli

Watanzania bado wanahitaji upinzani madhubuti wa kuiondoa ccm madarakani., tutamkumbuka na kumuenzi Maalim Seif Sharif Hamad siku zote, jemedari ambaye hakuwahi kutetereka wala kuyumba yumba kwenye mapambano.
Jitoe wewe nyuma ya keyboard ukafanye huo upinzani wa kweli!
 
Rais SSH ni mpango wa Mungu. Hakika baada ya yule Shetani wa Chato ambaye alikuwa anatugawa kiitikadi na kikabila, akiua na kutudanganya, tumepata kiongozi mwenye upendo, mcha Mungu na anayeipenda nchi yetu kwa dhati. Tanzania Iko salama sana mikononi mwa Samia.

Sanasana Magufuli angewapiga risasi au kuwateka
Wewe hata mumeo akishindwa kusimamisha ili akupande utamsingizia magufuli
 
To open up a new chapter as a nation haijawahi kuwa dhambi...

Hili kama ni kweli bac ni jambo jema kwa kila mwenye pumzi..

Narudia tena Political reconciliation ndiyo njia pekee ya kujenga taifa imara lenye umoja na nguvu kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.

Nchi haiwezi kujengwa na mawazo ya upande mmoja.
Co-existence of the opposites is a natural essential phenomenon. "Tusubiri kuona kitakachotokea".
 
Back
Top Bottom