Freeman Mbowe: "Mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo)". Je, dawa mujarabu ni ipi?

Baba yako bora angemwaga nje au mama yako bora angefanya abortion
 
Masuala ya clouds yanahusiana vipi na mada hii mkuu?
 
Mwenyekiti ndio mfano hai wa wanasiasa wasio na uwezo yaani katumia fursa ya UDJ na akawa mwanasiasa.
Kuna mijitu inampa sifa huyu mwenyekiti wa saccos Mr. Faru John asizo stahili kabisa. Saccos imemfia mikononi.
 
1.Makada wa vyama vya siasa wasiwe makamishina na watendaji wa tume ya taifa ya uchaguzi, iwe na marufuku kwa mtu aliyewahi kuwa kada wa chama kuwa mtendaji katika tume.

2.MaDED wasiwe watendaji wa tume katika ngazi za majimbo. Hata mahakama kuu ilikubaliana na hii hoja kabla ya watendaji wa jiwe kwenda kupindua katika mahakama ya rufaa.

3.Matoke ya Urais yapingwe mahakamani pia na kuwepo na mahakama ya kikatiba itakayoshughulikia kesi za uchaguzi na ukiukwaji wa katiba na viongozi.

4.Ubunge wa mbunge au spika usikome pale anapohama chama au kufukuzwa na chama chake ili kulifanya bunge kuwa huru.

5.Ubunge wa viti maalum na wa kuteuliwa uondolwe. Wabunge wote wawe ni watu waliopigiwa kura katika majimbo yao na watu wote. Ni fedhea kuwa na watu waliopigiwa kura na 'wanachama' wa vyama vyao tu. Pia hakupaswi kuwa na jimbo la Ikulu bungeni. Hata katibu wa bunge anapaswa kuwajiriwa na bunge sio kuteuliwa na Rais kama ilivyo sasa.

6.Rais aondolewe mamlaka ya kulivunja bunge.

7.Wagombea binafsi waruhusiwe kwa ngazi zote.Mwinyi amekiri kwamba ugombea binafsi ulipingwa kwa maslahi ya chama chake na sio maslahi ya taifa.
Mwambieni ndugu mwenyekiti ametuacha hewani kwa kutuambia tatizo linalokabili siasa zetu bila kutoa suggestions ya nini kifanyike. Mifumo bora ya kisiasa ina manufaa kwa wote chama tawala na upinzani.
 
Nyanoko ngikulu nogi
 
8.Makada wa vyama na watu walio nje ya mfumo wa utumishi wa umma wasipewe nafasi kubwa za juu katika uongozi wa umma.

Nafasi za katibu mkuu Kiongozi, makatibu wa wizara, ukurugenzi wa halmshauri na mashirika ya umma, wakuu wa mikoa na wilaya zipatikane kwa kupanda ngazi za utumishi kutoka ngazi ya chini kabisa badala ya kupachika pachika watu tu kutoka kusikojulikana.

Hii ni muhimu sana ukizingatia nchi yetu ni de facto monoparty state(nchi ya chama kimoja pasipo kuwa ni sheria) hivyo ni muhimu tukajaribu kuuiga mfumo wa upatikanaji wa viongozi wa china iliyofanikiwa chini ya chama kimoja.
Mwambieni ndugu mwenyekiti ametuacha hewani kwa kutuambia tatizo linalokabili siasa zetu bila kutoa suggestions ya nini kifanyike. Mifumo bora ya kisiasa ina manufaa kwa wote chama tawala na upinzani.
 
Mkuu, CCM inadeserve kukosolewa kwa kuwa inadhika Dola. Chama Cha Democrasia na Maendeleo na vyama vingine utavikosoa kwenye uendeshaji wa taasisi zao, ambapo hiyo ni kaxi ya wanachama. Kumkosoa Lema au Mbowe, hukosoi Chama. Unakosoa mtu mmoja mmoja. Lema, Mbowe au Lisu hao Ni watu sio taasisi Shekh. Kuishi uhamishoni ni sirika ya binadamu yeyote anapohisi hatari eneo analoishi, sio eti kulelewa na mwanaume mwenzio. Unaongea hivyo kwakuwa hujawahi kutishiwa maisha na Dola iliyopaswa kukulinda.
 
hivi umeandikiwa na nani hii ? maana uzi wa tano huu nakutana nayo una copy na ku paste.
 
CHADEMA utopolo tu
 
Weka ufuasi pembeni kwa muda tujadili suala la kitaifa kwanza.
 
Katibu huwa ni mteuliwa kwa sifa na utendaji wake. Bora mtu mwingine awe easy going lakini katibu awe technocrats. Hili suala la COVID - 19 pale bungeni ni danadana tu ilihali Freeman mbowe Aikael anafahamu kinachoendelea. Kama wale wabunge ni haramu ni kwa nini akina mbowe wapokee (kama wanapokea) na kutumia ruzuku haramu inayotokana wa watu haramu wanaovunja ibara ya 78(e) ya Katiba ya JMT?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…