Freeman Mbowe: "Mtu anaweza tu akashangiliwa kwenye majukwaa akapigiwa kura, lakini hakuna meritocracy (uwezo)". Je, dawa mujarabu ni ipi?


..gazeti ulilosoma na kulinukuu wamepata habari hiyo kutoka ktk mahojiano / mazungumzo baina ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu.

..Tundu Lissu anajaribu kuanzisha kipindi cha mahojiano na watu mbalimbali, na mtu wa kwanza kuhojiwa nadhani alikuwa ni Freeman Mbowe.

..Sasa ktk mahojiano hayo Lissu alimuuliza Mbowe kuhusu hatua alizopitia mpaka kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Moja ya mambo ambayo Mbowe aliyogusia ni shinikizo alilowapa Chadema kwamba ili awe mwenyekiti wa chama lazima Katibu Mkuu awe Dr.Wilbroad Slaa. Sasa ni ktk muktadha huo ndipo Mbowe akasema wakati mwingine zoezi la kuchagua kwa kura linaweza kupitisha watu wasio na uwezo wa kazi wanayoomba.
 
Amerudi kwa Agustino Mrema aliyetaka wapiga kura kupanga mstari nyuma ya mgombea wanayemhitaji

Kwa hisia hizi nadhani ingefaa Mbowe akaanzisha utaratibu huo mpya kwenye chama chake ambacho anakiongoza kwa miongo kadhaa sasa.
 
Mbowe akasema wakati mwingine zoezi la kuchagua kwa kura linaweza kupitisha watu wasio na uwezo wa kazi wanayoomba.
Na hicho katika bolded letters ndicho ambazo mimi nimekileta humu kwa wadau kwa ajili ya mjadala mpana. Je, Mbowe alikuwa sahihi kwa kusema maneno hayo? Na kama alikuwa sahihi, ni nini dawa mujarabu ya kukabiliana na changamoto hiyo na kuondokana na wanasiasa wasio na uwezo katika utendaji?

Kwani kuna tofauti gani kati ya chaguzi za ndani ya vyama na zile za nje ya vyama (Wabunge na Madiwani)? Michakato mbona ni ni ile ile tu, come-pain (campaign) kwanza kisha box la kura linafuata.
 
Amerudi kwa Agustino Mrema aliyetaka wapiga kura kupanga mstari nyuma ya mgombea wanayemhitaji

Kwa hisia hizi nadhani ingefaa Mbowe akaanzisha utaratibu huo mpya kwenye chama chake ambacho anakiongoza kwa miongo kadhaa sasa.
Mbowe na Mnyika ni mafisadi sana na ndio wamefilisi ile SACCOS yao
 

..unaweza kuchagua kwa kura ukapata mtu asiyefaa.

..unaweza kuteua ukapata mtu asiyefaa.

..vilevile njia zote zinaweza kukupatia watu wanaofaa.
 
..unaweza kuchagua kwa kura ukapata mtu asiyefaa.

..unaweza kuteua ukapata mtu asiyefaa.

..vilevile njia zote zinaweza kukupatia watu wanaofaa.
Tanzania inahitaji viongozi wanaofaa. Full stop. Ndio maana nikauliza, kama Mbowe yupo sahihi, sasa tutumie njia gani ya kupata wanasiasa makini watakaoifaa Tanzania yetu pasipo kucheza kamari ya kisiasa?
 
Tanzania inahitaji viongozi wanaofaa. Full stop. Ndio maana nikauliza, kama Mbowe yupo sahihi, sasa tutumie njia gani ya kupata wanasiasa makini watakaoifaa Tanzania yetu pasipo kucheza kamari ya kisiasa?

..kuna mazingira ambapo KURA zinafaa.

..Na kuna mazingira ambapo UTEUZI unafaa.

..tunatakiwa tujiulize tuwe na mfumo gani wa kupiga kura ili kutuepusha au kupunguza uwezekano wa kuchagua watu wengi wa hovyo-hovyo.

..pia mfumo wetu wa uteuzi uwe na namna gani ili ku-weed out candidates ambapo hawana uwezo au viwango kwa nafasi husika.

..ukiwa na tume ya hovyo na kuhuni ya uchaguzi unakuwa umekaribisha watu wa hovyo au chama cha hovyo kushinda uchaguzi.

..ukiwa na mfumo wa uteuzi wa kificho unaomtegemea mtu mmoja upo then upo uwezekano mkubwa wa watu wasio na sifa kuteuliwa.
 
Sawa mkuu, sasa nimeelewa mawazo yako. Thanks.
 
Gharama sana mkuu. Au gharama ya pesa ndio gharama ya kuwa na demokrasia thabiti?
Possibly. But unaweza kupunguza ukubwa wa bunge lililopo (na unapunguza malipo pia?) na ku create hilo bunge dogo (lakini la juu kimadaraka). Let say hilo bunge la juu, linakuwa na wabunge wa kuteuliwa (au namna nyingine ya kupatikana kwa merit - CV, uwezo?) mmoja kutoka kila mkoa wa Tz.

Unaweza pia kuondoa nafasi za RCs na DCs ili kupunguza gharama kwa nchi.
 
Let say hilo bunge la juu, linakuwa na wabunge wa kuteuliwa (au namna nyingine ya kupatikana kwa merit - CV, uwezo?) mmoja kutoka kila mkoa wa Tz.
Asante mkuu umewaza vema sana na kwa kuongezea tu ni kwamba kwenye comment number 69 hapo juu, ndugu yetu JokaKuu amesema maneno haya;

"pia mfumo wetu wa uteuzi uwe na namna gani ili ku-weed out candidates ambapo hawana uwezo au viwango kwa nafasi husika"
 
Asante kwa maoni yako mazuri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…