Freeman Mbowe: Nimetolewa gerezani kwasababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi nguvu ya vyombo vyao vya dola

Freeman Mbowe: Nimetolewa gerezani kwasababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi nguvu ya vyombo vyao vya dola

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Sikutolewa gerezani kwasababu kuna mtu ananipenda, nimetolewa gerezani kwasababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi sana.

========

Freeman Mbowe: Tulianza kama chama kidogo, leo ni chama kikubwa dunia inakitambua hata CCM waliokuwa hawatutambui kupitia kesi hii wametambua kwamba CHADEMA ni jeshi kubwa na hilo jeshi kubwa limekuwepo kwasababu kuna mmoja, wapili, watatu, wanne kwahiyo pamoja na matatizo na hofu mliyonayo tuwe wazito sana kuwapoteza wenzetu, isiwe ndio utamaduni wetu, utamaduni wetu tukumbatiane kama watoto wa maam mmoja kwasababu nguvu ya CHADEMA ni upendo na umoja wetu.

Hatuna majeshi, hatuna silaha lakini umoja wetu umekuwa ni silaha yetu kubwa sana na silaha hii ya umoja huu ndio imenitoa mimi gerezani, sikutoka gerezani eti kwasababu mtu ananipenda, nimetolewa gerezani kwasababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi sana nguvu ya vyombo vyao vya dola ndio sababu nikatoka ndani, kwasababu ya wingi na umoja wetu.

Hakuna anayepinga hilo, hata CCM wanaojielewa walikuwa upande wa haki kwenye issue ya Mbowe ndio maana pressure ikazidi kwa mamlaka.

Laiti kama moto ule wangeuelekeza kwenye Katiba Mpya leo tungekuwa na Tanzania mpya kabisa isiyo na matabaka ya aina yoyote huku wote tukiwa kitu kimoja kwenye taifa moja.

Sasa asubiriwe Mbowe na viongozi wa chama chake waje kuongea na waandishi wa habari na watz kwa ujumla kama alivyosema juzi, yeye ndie atatoa "a way forward" juu ya nini kinafuata kwenye harakati za kudai haki.

Sio kuokoteza maneno ya mitaani Mbowe amejisalimisha kwa watawala, wengine eti CCM wanajua michezo ya siasa, wangeijua hiyo michezo wasingeiba kura kila uchaguzi mkuu unapofika, wamezeeka hakuna wanachojua tusidanganyane.
 
Huyu jamaa ni zero brain,ndo maana alipata zero kwenye mtihani wa kidato Cha sita,na Wala asitake kuudanganya umma kuwa eti nguvu ya umma imemtoa kutokana na kupendwa kwake,huyu Ni muuongo mkubwa,watanzania wapi hao wanaompenda ikiwa huku niliko wakazi wake wote wanawaza CCM tu.

Aache Mara moja kuupotosha umma,auambie umma pamoja na wafusi wake kuwa isingekuwa huruma na busara za mama Samia angekufia jela!!
 
Wanasiasa makosa yao mengi ni ya kisiasa
Wanafanya kweli makosa ila wanatumia mwamvuli wa kisiasa kupata huruma kama hivi.

We chukulia mfano tu wa kesi hii ya Mbowe angekua mwananchi wa kawaida.

Kuna ambaye angeliga kelele asamehewe??

Au baada ya kusamehewa aitwe ikulu??

Hawa wanasiasa wanajua kucheza tu na akili za wafuasi wao ila kimsingi sio watu safi sana kama tunavyofikiri.
 
Huyu jamaa ni zero brain,ndo maana alipata zero kwenye mtihani wa kidato Cha sita,na Wala asitake kuudanganya umma kuwa eti nguvu ya umma imemtoa kutokana na kupendwa kwake,huyu Ni muuongo mkubwa,watanzania wapi hao wanaompenda ikiwa huku niliko wakazi wake wote wanawaza CCM tu.

Aache Mara moja kuupotosha umma,auambie umma pamoja na wafusi wake kuwa isingekuwa huruma na busara za mama Samia angekufia jela!!
Gingi, baba sijakusoma chuki Yako Kwa mwamba ni katika mambo binafsi TU au uusehemu ya lililokuwa team/kundi bambikizi🤔
 
Back
Top Bottom