Freeman Mbowe, Said Issa na Tundu Lissu, washinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu CHADEMA

Freeman Mbowe, Said Issa na Tundu Lissu, washinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu CHADEMA

Mwambe msemo wa waingeleza wasema "if you can't beat them join them......" Kazi kwako.
 
Mbowe hajasoma alama za nyakati ningekua yeye ningeacha uongozi kwasababu ninauhakika mwakani chama kikuu cha upinzani ni ACT.

Huenda akawa na wabunge wachache sana.
Hii itasaidia kutompa lawama yeyote gia aliyobadili angani lazima immalize akiwa anashuhudia mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa naamini pia uwepo wa Mbowe CHADEMA unawanufaisha CCM sana na wenye CCM yao pengine hawawezi kuruhusu Mbowe atoke madarakani kwasababu anahekima ya kuwadhibiti wanaCDM kama alivyo Seif Zenji. Anawadhiti kwa faida ya nani? mimi sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera zao mashujaa wetu Freeman Mbowe na Tundu Lissu na hakika "wishes" za jamaa zetu wa Lumumba za kutupenyezea wasaliti wao zimeshindwa!

Hakika uwepo wa chama cha Chadema ni mpango wa Mungu na yeyote anayetamani kukiua chama hicho atapambana na hasira za Mungu wetu aliye Mkuu kuliko kitu chochote hapa duniani
Hivi mkuu pamoja na maneno yote Mbowe na Lisu wana kipi kipya watakileta ili kuivusha chadema Kwenda Ikulu, kilichoshindika kwa miaka zaidi ya 20?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#NoHateNoFear #CHADEMA ✌🏾✌🏾✌🏾💪🏾💪🏾💪🏾
 
Baada ya CCM (baba lao), chama kinachofuata chenye wafuasi wengi na hata wabunge wengi ni CHADEMA. Ninacho kiona kila siku ni kwamba japo chama kina watu wanao onekana kwa nje kama ni watu machachari wakijinasibu kuwa wao ni akili kubwa kumbe ni waoga wakupindukia, wanaogopa kushika nafasi nyeti ya uenyekiti wa chama, miaka nenda rudi hawajiamini wala kumwamini yeyote zaidi ya Mh Mbowe.

Siku rais wa nchi hii akitokea CHADEMA basi watatamani akae milele maana hawana mbadala kama ilivyo kwa mwenyekiti wao. Kwakutambua kwamba miongoni mwao hakuna mtu mwenye uwezo wa kuongoza taifa ilibidi mwaka 2015 wamtumie mwana CCM mzee Lowassa na mwakani huenda wakamtumia mwana CCM mwingine katika nafasi hiyo maana hawana mtu mwenye sifa ya kugombea nafasi ya u rais.

Nachukua nafasi hii kuwapongeza CCM, naomba sana muwafundishe hawa watoto wenu umuhimu wa kupokezana madaraka.
 
Ushauri mzuri ila hauendani na uhalisia, labda swali kwako kidogo tu; hivi ukiona adui yako mkubwa anataka umuondoe mwenyekiti wa chama chako kwenye nafasi yake, utafanyaje wewe binafsi kama kweli una akili timamu?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hapa ndio unaona utofauti kubwa sana kati ya Raisi wa TANZANIA ndugu Magufuli na yule Dikteta uchwara MBOWE ambaye aliamua kwa matakwa yake na kuendekeza tamaa ya Madaraka kwa kubaka kipande cha katiba na kukinyofolea mbali kipande cha ukomo wa yeye kutoka madarakan ili aendele kula ruzuku na kukiibia chama rasilimali zake kwa manufaa yake.

Raisi Magufuli kashasema yeye Ataeshimu katiba ya nchi na katu ato baka katiba kama alivyo baka katiba M/kiti wa CHADEMA taifa bwana MBOWE ya yeye kujipa madaraka ya kudumu. Hili sasa liwe funzo kwa wanachama wote wa chadema warudi kwenye vikao vyao halali na kurudisha kile kipande kilicho nyofolewa na waroho wa madaraka wanaongozwa na Dikteta MBOWE.

Hapa Mbowe kaumbuka sana maana alijua atajificha kwenye kichaka cha Mh.Raisi kuongeza muda wa kukaa madarakan kwa nafasi ya uraisi na uenyekiti wa chama chake Ccm. Sasa Mbowe kabakia peke yake Kwenye raman ya udikteta na ubakaji wa katiba ya chama chao.
IMG-20191219-WA0000.jpeg
IMG-20191219-WA0001.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila hii nadharia ya 'maridhiano' sijui 'majadiliano' na CCM binafsi inanichefua kabisaa, mwacheni nguruwe ( CCM) avamie shamba la mahindi, wake ni mkuki tuu na si vinginevyo!
 
Back
Top Bottom