Baada ya CCM (baba lao), chama kinachofuata chenye wafuasi wengi na hata wabunge wengi ni CHADEMA. Ninacho kiona kila siku ni kwamba japo chama kina watu wanao onekana kwa nje kama ni watu machachari wakijinasibu kuwa wao ni akili kubwa kumbe ni waoga wakupindukia, wanaogopa kushika nafasi nyeti ya uenyekiti wa chama, miaka nenda rudi hawajiamini wala kumwamini yeyote zaidi ya Mh Mbowe.
Siku rais wa nchi hii akitokea CHADEMA basi watatamani akae milele maana hawana mbadala kama ilivyo kwa mwenyekiti wao. Kwakutambua kwamba miongoni mwao hakuna mtu mwenye uwezo wa kuongoza taifa ilibidi mwaka 2015 wamtumie mwana CCM mzee Lowassa na mwakani huenda wakamtumia mwana CCM mwingine katika nafasi hiyo maana hawana mtu mwenye sifa ya kugombea nafasi ya u rais.
Nachukua nafasi hii kuwapongeza CCM, naomba sana muwafundishe hawa watoto wenu umuhimu wa kupokezana madaraka.